Monday 31 March 2014

SHAMBULIZI LA KIGAIDI LAUWA 6 NCHINI KENYA

Filled under:



Watu sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.

Polisi wamesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika mkahawa mdogo ulio karibu na kituo cha mabasi mtaani humo.
Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.

Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.

Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.

Posted By Unknown12:18

WALIMU YA AJIRA MPYA WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO 2014

Filled under:

WALIMU YA AJIRA MPYA WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO 2014

Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala  za Mikoa na Serikari za Mitaa imebadilishia vituo  kwa walimu wapya mwaka 2014 hii ni kutokana na maombi mbalimbali ya walimu hao,walimu waliokubaliwa ni pamoja na ngazi ya cheti,stashahada na shahada.

Walimu wote walioomba kubadilishwa vituo waangalie majina yao katika orodha iliyotolewa na kama baadhi yao majina yao hawajayaona basi watambue kama maombi yao yajakubalika hivyo basi wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao walivyopangiwa mnamo  tarehe  15/03/2013.

Imesisitizwa kuwa tarehe ya kuripoti katika vituo elekezi ni tarehe  10/04/2014 ambaye hataripoti katika kituo chake cha kazi atakuwa amepoteza ajira yake.

Bofya hapa:-











Posted By Unknown11:24

JK AKIONGEA NA MAMIA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

Filled under:



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya Watanzania waishio Uingereza alipokutana nao usiku wa Machi 30, 2014 katika ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Wembley, London, Rais yupo katika ziara ya kiserikali ya  siku tatu kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe David Cameron

Posted By Unknown06:24

KAMILI:MWENYEKITI WA CCM ALIHUSIKA KUNITESA

Filled under:



Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili, aliyedai ametekwa na kuteswa wakati wa uchaguzi mdogo mkoani Iringa, amemtuhumu Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Jessica Msambatavangu kuwa anahusika na mashambulizi dhidi yake.

Kamili alidai alitekwa, kupigwa na kujeruhiwa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga uliofanyika mapema mwezi huu.

 Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari  mjini Dodoma, siku moja baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba, alisema akiwa vijijini alikokwenda kusambaza mawakala wa  kusimamia uchaguzi wa  Kalenga, alitekwa na watu asiowafahamu ambao walimwingiza kwenye gari na hadi ofisi za CCM mkoani  Iringa.

“Nilipofikishwa katika ofisi hizo nilianza kushushiwa kipigo kikali hata kabla sijashushwa kwenye gari. Nilipelekwa  katika moja ya ofisi na kukutana  Mwenyekiti wa CCM Msambatavangu na kumtambua,”alisema.

Alieleza kusikitishwa na hatua ya mwanamke mwenzake  akimfanyia visa hivyo.
Alisema kuwa Msambatavangu aliamuru aletwe baunsa ambaye ndiye aliyeanza kumpa kipigo kikali huku kiongozi huyo akisisitiza apigwe  zaidi.

Alisema  baada ya kupigwa kwa zaidi ya dakika 20, lilikuja gari la polisi na  wakamweleza kuwa wamefika mahali hapo kwa ajili ya kumwokoa na kumchukua kumpeleka kituoni.

Kamili alisema  alipofikishwa polisi hali yake ilianza kuwa mbaya  ndipo  walipomwandikia fomu namba tatu  (PF3) na kumkimbiza  kwenye  matibabu.

Alisema anasikitishwa kuwa hata baada ya kumtaja mbaya wake polisi, mwenyekiti huyo hajakamatwa na badala yake yupo ndani ya bunge la katiba huku kukiwa hakuna hata jalada alilofunguliwa dhidi ya kiongozi huyo.

Aidha Kamili alilituhumu Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa upendeleo wa dhahiri na kutojali madhila yaliyompata.

“Tangu nijeruhiwe hakuna tamko lolote  lililotolewa na uongozi wa Bunge kuhusiana tatizo lililonikuta, licha ya kuwa Spika ni mwanamke.”

Alisema mbali na kutoa tamko, hakuna msaada wowote wa kitabibu alioupata kutoka bungeni, lakini wabunge wa CCM wanapougua  bunge linakuwa mstari wa mbele kutoa huduma.

Umoja wa wabunge wanawake wa vyama vya Upinzani wametoa tamko la kulaani kitendo hicho na kuitaka Serikali ichukue hatua haraka kushungulikia tatizo hilo.

Akitoa tamko hilo mbele ya wandishi wa Habari, Mwenyekiti wa wabunge hao, Suzan Lyimo alisema kuwa kitendo alichofanyiwa mwanamke mwenzao ni kibaya kinachowakatisha  wanawake tamaa.

Posted By Unknown06:16

WATU WAWILI WAAMBUKIZWA EBOLA

Filled under:

 
Ugonjwa huo umesemekana kutokana na Popo wanaoliwa kama kitoweo nchini Guinea 
Watu wawili wameambukizwa ugonjwa hatari ya Ebola nchini Liberia ulioenezwa kutoka nchini Guinea ambako umewaua watu 78.

Walioambukizana ugonjwa huo ni madada wawili, mmoja wao akiwa tu ndio amerejea kutoka nchini Guinea.
Maafisa wanasema kuna wasiwasi kuwa ugonjwa huo unaendelea kuenea.
Ugonjwa wa Ebola, huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine na huua kati ya 25% na 90% ya waathiriwa.

Muimbaji mashuhuri Youssou Ndour amelazimika kukatiza ziara yake kwenda mjini Conakry kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Ingawa alikuwa amesafiri hadi mji mkuu,aliambia BBC sio wazo zuri kuleta maelfu ya watu katika sehemu moja wakati ugonjwa huo umeanza kuenea kwa kasi.

Mlipuko ulianza nchini Guinea wiki jana na kuenea hadi mji mkuu ambao una watu milioni mbili.
Waziri wa afya nchini Senegal, Awa Marie Coll-Seck, alisema kuwa serikali imeamua kufunga mpaka wake na Guinea, baada ya kuthibitisha kuwa ugonjwa huo umeenea hadi mjini Conakry.

Pia kumekuwa na taarifa ya ugonjwa huo kuwepo nchini Sierra Leone, lakini taarifa hiyo haijathibitishwa.
Ugonjwa wenyewe unaaminika kuenea kutoka kwa Popo wanaoishi mitini na ambao huliwa na watu Kusini Mashariki mwa Guinea.

Posted By Unknown06:02

Friday 28 March 2014

TAARIFA YA MBUNGE WA NZEGA KWA UMMA KUHUSIANA NA UPOTOSHAJI ULIOFANYWA NA TCME

Filled under:

Taarifa ya Mbunge wa Nzega kwa Umma Kuhusiana na Upotoshaji Uliofanywa na Taasisi ya Tanzania Chamber of Minerals and Energy (TCME)

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega imesikitishwa na kufadhaishwa na taarifa ya uongo na isiyo na uzalendo hata chembe, iliyotolewa na taasisi ya TCME siku ya tarehe 26, Machi, 2014. Hii imedhihirisha kuwa, hawajui wanalolifanya ama wanatumiwa vibaya na watu wenye maslahi ovu kwa wachimbaji wadogo wadogo wa Nzega na wa Tanzania kwa Ujumla.
Taarifa za namna hii hazina maksudi mengine zaidi ya kusababisha chuki na mfarakano usio na sababu za msingi baina ya makundi ambayo yangepaswa kufanya kazi pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huu. 
Mbunge wa Nzega amekuwa ni mtu anayependa kutoa fursa ya mazungumzo na
wabia wote wa maendeleo jimboni kwake na yuko tayari kusikilizana na yeyote yule, inashangaza ni kwa nini wadaua hawatumii vizuri fursa hizi kwa faida ya wote. 
Mbunge wa Nzega ni muwekezaji yeye mwenyewe binafsi na anatambua umuhimu wa wawekezaji kwa ukuaji uchumi na maendeleo ya jamii ya watu wake, na ndiyo maana amekuwa siku zote mstari wa mbele kuvutia wawekezaji mbalimbali katika jimbo lake. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) si mchukia wawekezaji hata kidogo. Yeye ni mtetezi wa haki za kila mtu, hata za askari polisi na magereza.

Tamko la Shrikisho la Wachimbaji na Watafutaji Madini na Nishati Tanzania (TCME) lingepaswa kuwa la ukweli na lenye weledi wa kutosha, lakini inasikitisha limekuwa ni tamko lisilo na uadilifu na hata chembe ya ukweli. Hata kama taasisi hii inawawakilisha na kuwatetea mabepari, isitetee uongo na dhulma ya wazi. Inapaswa ifahamu kuwa, Ubepari utakaoweza kufanya kazi Tanzania ni ubepari wenye sura ya kijamaa, unaothamini utu, udugu na umoja wetu.

Kwanza, Kwamba, Mbunge aliongoza maandamano haramu kuelekea eneo la Mwanshina, si kweli. Ukweli ni kwamba, Mbunge wa Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI, Dr. Hamisi Kigwangalla, hakuongoza maandamano yoyote yale siku ile bali alifanya mkutano halali, na alikuwa na ratiba ya mikutano miwili jimboni mwake katika Kata zake mbili, Kata ya Nzega Ndogo (Kijiji cha Zogolo) na Kata ya Lusu(Kitongoji cha Mwashina), ambayo ni maeneo yanayohusisha mgodi wa wachimbaji wadogo wadogo wa Mwanshina. 
Mikutano hii ilitolewa taarifa polisi na mamlaka nyingine mbali mbali wilayani Nzega, kwa mujibu wa Sheria, na Ofisi ya Mbunge iliomba na kupewa ulinzi halali wa polisi. Baada ya kumaliza Mkutano mmoja, wananchi pamoja na Mbunge wao waliazimia waelekee kwenye Mkutano wa pili, yaani eneo la Mwanshina, na walitembea kwa miguu wakiongozwa na polisi, na hakukuwa na vurugu, matusi na wala dalili yoyote ile ya uvunjifu wa amani ama uharibifu wa mali za watu. Kama kwenu watu wa Shrikisho kutembea kwa miguu ni Maandamano basi hamuelewi mfanyalo, maana hata waendao mazishini, harusini, watokao uwanjani kuangalia mpira, ama watokao misikitini ama makanisani, ama kwenye mikutano ya mahubiri, ama jaji/hakimu anavyotoka na mahakama kwenda kuangalia eneo la tukio huwa ni kwa makundi, basi na wao ni waandamanaji!

Pili, Kwamba “Ni vizuri jamii ikajulishwa kwamba eneo lililovamiwa na wachimbaji wadogo linamilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafiti wa madini ya Resolute (Tanzania) Limited, ambao wana leseni halali ya kuchimba madini katika eneo hilo, leseni namba SML19/97)”, inasema taarifa yao. Kauli hii ni ya mtu asiyejua sheria ya ardhi ya Tanzania, na kama huu ndiyo uelewa wenu haishangazi kwa ninyi kutoa tamko la uongo na upotoshaji namna hii. Resolute ‘hamiliki’ eneo la Mwanshina, anamiliki leseni ya kuchimba dhahabu tu! Eneo la Mwanshina ni mali ya wananchi wakazi wa eneo lile, waliozaliwa pale na ndiyo maana hata yeye hakuliweka kwenye uzio wa maeneo yake. Na ndiyo maana hata leo hii akitaka kuchimba pale hawezi kufanya hivyo zaidi ya kutumia nguvu za jeshi la polisi tu. Na hichi ndicho kitakachopingwa na wananchi siku zote.

Tatu, katika taarifa ya TCME wanasema “Kitendo cha Kiongozi cha kuhamasisha wachimbaji wadogo kuvunja sheria ni mfano mbaya sana kwa jamii yetu na ni kitendo hatarishi kwa amani na utulivu”. Ni vema TCME wakataja ni kiongozi gani amehamasisha wachimbaji wadogo wadogo wavunje sheria? 
Ni lini, wapi na kwa kauli ipi alihamasisha uvunjani huo wa sheria? Ni Mbunge aliyeenda kuwasikiliza wananchi waliofukuzwa kuchimba ama ni Naibu Waziri Nishati na Madini, Mhe. Stephen Massele, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ndg. Fatma Mwassa, na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Ndg. Bituni Msangi, waliowarudisha wachimbaji hawa katika eneo lile na baada ya wiki 2 tu kuwaondoa? Wananchi hawa walianza kuchimba dhahabu eneo lile mwezi Desemba mwaka 2013, wakazuiliwa na serikali mwezi wa kwanza na walitii agizo hilo. Mbunge aliongea na Naibu Waziri na wakakubaliana kuwa atazungumza na Resolute wazirudishe leseni za eneo la Mwanshina kwa serikali hata kabla hazijamaliza muda wake, kwa kuwa wao wanaondoka na hawachimbi tena dhahabu pale, ili Serikali iwakatie wananchi leseni zao na kwamba wajiunge kwenye vikundi na SACCOS ili muda ukifika tu wapewe! 
Je, ni nani hasa aliyewarudisha wachimbaji hawa kwenye eneo la ‘Resolute’ kabla ya utaratibu huu kukamilika? Na wakati anawarudisha aliwasiliana na Mbunge? Wakati anawarudisha hakujua kuwa hawana leseni na kwamba eneo lile ‘linamilikiwa na Resolute’? Ni kwa nini tena aliyewarudisha, akawaacha wakawekeza ‘vijisenti’ vyao, na baada ya muda wa wiki mbili hata hawajafika popote anakuja anawaondoa tena? Ni nani atawalipa fidia ya nguvu, muda, na mitaji yao waliyowekeza pale? Ama uwekezaji wa watanzania maskini hauna maana kabisa kwenu? Wenye maana ni utafiti wa Resolute tu? Resolute mwenyewe alipokuja takriban miaka 15 iliyopita alikuta wenyeji wakichimba, mbona wao hawakulindwa dhidi yake? Maana na wao si walitafiti na kugundua uwepo wa dhahabu eneo lile na wakaanza kuchimba kabla yake?

Hivi ni wapi wachimbaji wadogo wadogo wamepewa maeneo yao na wanachimba dhahabu nchini mwao huku wakiwa na leseni? Ni kule Rwamgasa, Mwime ama Mwabomba? Kule wametumia vigezo gani kuwaruhusu watumie leseni za Barrick na mashirika mengine, na hapa Nzega wanawakataliaje? Ama ni kudhirisha madai kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wana maslahi yao na hili eneo la Mwanshina?

Hakuna anayekataa uwekezaji mkubwa kwenye maeneo yetu bali hakuna atakayekubali wawekezaji wachukue kila kitu na wenyeji wakose kabisa. Hakuna atakayekubali wenyeji wanyanyaswe na wapoteze mali yao kwa sababu kuna maslahi ya viongozi wachache. Miaka 15 iliyopita walipoteza mali yao na hawakulipwa fidia, leo hii hatutakubali wadhulumiwe tena!

Mwisho, rai yetu ni kwamba, viongozi wa Serikali watumie busara na hekima ya hali ya juu mara zote panapotokea migogoro baina ya wawekezaji na walalahoi ili kuondoa dhana kwamba wawekezaji wana thamani zaidi ya wenyeji, badala ya nguvu za kijeshi, uonevu, mabavu na vitisho, hususan kwenye mgogoro kama huu ambapo kwa kiasi kikubwa ni viongozi wa Serikali waliouanzisha kwa kuzuia uchimbaji pale awali, na kisha kuruhusu bila kufuata sheria. 
Aidha Serikali iwafutie kesi wachimbaji wote wadogo wadogo na Raia waliokamatwa wakipita eneo lile siku hiyo bila kujua nini kimetokea pale, kwa vile tunaamini hakuna kosa walilofanya na pengine ni uonevu kuwashitaki hao wachache waliokamatwa. Pia, ni busara Serikali ikaongeza kasi ya kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kuwapatia wachimbaji wadogo wadogo leseni kama makubaliano ya awali yalivyokuwa na pia mwongozo wa uchimbaji wenye tija na ufanisi.

Imetolewa na,

Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Nzega.
Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB).
Machi 28, 2014.

Posted By Unknown08:43

NDEGE YA MALAYSIA KUTAFUTWA KATIKA ENEO JIPYA

Filled under:

 
Ndege 9 za kijeshi na Moja ya kiraiya zinatafuta mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370
Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita , wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.

Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.

Mamlaka ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.

Eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia

Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa na abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika mwendo wa kasi kinyume na ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.
Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za juu ya Australia John Young, amesema utafiti mpya unaonesha kuwa ndege hiyo ya MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza kuwa

sababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika haraka.
Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari Hindi .

Posted By Unknown08:21

Tuesday 25 March 2014

TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Filled under:


TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA


Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya
kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.

25 Machi,2014


Posted By Unknown08:37

MKURUGENZI WA BODI YA ATALII AVULIWA MADARAKA

Filled under:



Serikali imemvua wadhifa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Dk Aloyce Nzuki kutokana na utendaji usioridhisha.

Akitangaza uamuzi huo jana mbele ya waandishi wa habari, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema kuwa ameridhia uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo ambao walipendekeza mkurugenzi huyo aondolewe.
Katika barua waliyomwandikia Waziri ikiwa imesainiwa na Mwenyekiti wa Bodi, Charles Sanga na kuridhiwa na wajumbe wote, walidai Nzuki alishindwa kuutangaza utalii ambalo ndilo jukumu la bodi hiyo.

“Nilipata barua kutoka TTB ikinishauri kumwondoa Bwana Nzuki na baada ya kushauriana na naibu wangu na katibu mkuu nikaona ni vyema kukubaliana na ushauri wa bodi,” alisema Nyalandu jana, huku akiwa na naibu wake, Mahamoud Mgimwa na wajumbe wa Bodi ya TTB.
Nyalandu alisema Dk Nzuki atapangiwa kazi nyingine ndani ya wizara hiyo .
Aliwaomba Watanzania wenye uwezo kuomba nafasi hiyo hata wale walio nje ya nchi ili kuweza kusaidia kukuza utalii wa nchi, uwe mbele ya mataifa mengine duniani.
“Nategemea katika siku 21 nafasi hiyo iwe imezibwa, kwani nimewashauri watumie kampuni inayoheshimika ili kufanya mchakato huo ,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya mchujo kufanyika, bodi hiyo itampa majina ya watu watatu ambayo baadaye atayapeleka kwa Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya moja kuteuliwa kujaza nafasi hiyo.

Posted By Unknown08:31

KINGWANGALLA AKAMATWA NA POLISI KISA!!

Filled under:



JESHI la Polisi wilayani Nzega, mkoani Tabora limemkamata na kumuachia kwa masharti Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangallah, kwa madai ya kuongoza maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao wanapinga kufungwa kwa machimbo ya Mwashina, yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited.

Mbunge huyo alikamatwa majira ya saa 10:00 jioni juzi baada ya kufanya maandamano yasiyo na kibali yaliyoanza saa saba mchana.
Kabla ya hapo mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara na wachimbaji hao katika Kijiji cha Nzega Ndogo wilayani humo ambapo alielezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na Kamishna wa Madini nchini, Paulo Masanja, bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao.

Katika mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vema serikali iangalie haki zao zilizotumika kwenye uendeshaji na uchimbaji wa mashimo hayo kuliko kuwafungia bila kujali ingawa eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa Resolute.

Hata hivyo katika hoja hiyo mbunge huyo aliwataka wachimbaji hao kudai haki yao kwa kufuata taratibu bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja.

Dk. Kigwangallah aliwaambia wachimbaji hao haki zao ziko mikononi mwao hivyo ni uamuzi wao kudai haki na yeye kama mwakilishi wao yuko nyuma yao mpaka pale haki yao itakapopatikana.

Aidha, wachimbaji hao walimwomba mbunge huyo kuambatana nao kwenye maandamano ya amani kutoka Kijiji cha Nzega Ndogo kwenda Mwashina yalipo machimbo yaliyofukiwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu kujionea hali halisi.

Kufuata hali hiyo, wachimbaji hao walianza maandamano ambayo yaliungwa mkono na mbunge huyo hadi Kijiji cha Mkwajuni kabla ya kufika Mwashina, ambapo polisi waliibuka na kuyasambaratisha kwa mabomu ya machozi.

Katika  purukushani hizo polisi walimkamata Dk.  Kigwanhallah   na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso, ambapo waliondoka naye kwenye gari pamoja na mbunge huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda, alisema Dk. Kigwangallah alikamatwa na kuachiwa huru ili akamalizie kazi zake kama mjumbe wa Bunge la Katiba.

Posted By Unknown08:22

Monday 24 March 2014

KINGUNGE:NILIWAHI KUVULIWA WADHIFU WA UKUU WA MKOA

Filled under:



MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombere-Mwiru, alisema kuwa aliwahi kuvuliwa wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa sababu ya kutofautia kimtazamo na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kingunge ambaye anawakilisha kundi la waganga wa tiba asili, alikumbushia tukio hilo juzi katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika mjini hapa katika Ukumbi wa Msekwa, naye akiwa mmoja wa watoa mada.

Akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili la kwanini amegeuka mlalamishi wa kukosoa viongozi wenzake wa sasa wakati amekuwa sehemu ya serikali kwa awamu zote nne bila kutimiza wajibu wake, Kingunge alisema kuwa amekuwa akikosoa na wakati fulani iliwahi kumgharimu.

“Wakati fulani nikiwa mkuu wa mkoa, nilipingana na Mwalimu Nyerere nikikataa katiba isibadilishwe kwa manufaa ya watu fulani, basi nikafukuzwa ukuu wa mkoa. Hivyo si kweli kwamba sikukosoa, hata sasa naendelea,” alisema.

Katika mada yake kuhusu mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya, alisema kuwa nchi zinazopata fursa ya kuandika upya katiba zake, zinapaswa kujikita kuandika katiba bora zitakazoweza kuwa na misingi ya kukuza uchumi wa kujitegemea.

“Maisha yetu yameegemea uamuzi wa wenzetu. Tumepigania uhuru ili tujitawale lakini bado ni tegemezi na kama nchi iko hivyo halafu nafasi ya kuandika Katiba mpya inakuja mnapanga safu za vyeo haina maana,” alisema

Posted By Unknown21:23

MKUMBO:UHALALI WA KITAFITI WA MAONI YA WANANCHI TUME YA WARIOBA

Filled under:



BUNGE la Katiba linatarajiwa kuanza kazi yake wiki hii baada ya kukamilisha na kupitisha kanuni zake na hatimaye kuchagua Mwenyekiti atakayeliongoza. Kazi kubwa ya Bunge hili ni kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba ambayo hatimaye itapigiwa kura na wananchi.

Wabunge wana vigezo viwili vya kuwasaidia kufanya uamuzi wao katika ibara mbalimbali za rasimu inayopendekezwa na Tume ya Warioba. Kigezo cha kwanza ni kutumia kile tunachoweza kukiita uamuzi kwa mujibu wa utashi wa kisiasa (political based decision making). Kigezo cha pili ni kile tunachoweza kukiita uamuzi kwa mujibu wa ushahidi wa kisayansi (evidence based decision making). Vigezo vyote vinapatikana kikamilifu katika ripoti na nyaraka mbalimbali za Tume ya
Warioba. Ni matumaini yangu kwamba kila mjumbe katika Bunge hili atazisoma nyaraka zote zilizomo katika Tume ya Warioba kwa ukamilifu wake kabla hajaanza kuchangia. Kwa kweli ningekuwa Mwenyekiti wa Bunge hili ningehimiza kila mjumbe asitoe mchango wake kabla hajasoma nyaraka hizi, ambazo kwa ujumla wake zipo zaidi ya saba.

Katika makala haya ninatoa mchango wangu kwa kuanisha uhalali wa kisayansi kuhusu maoni ya wananchi yaliyopo katika ripoti ya Tume ya Warioba. Kuna nyaraka mbili katika Ripoti ya Tume ya Warioba kuhusu maoni ya wananchi. Nyaraka ya kwanza ni ile inayoanisha maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyaraka ya pili ni ile inayoanisha maoni ya Mabaraza ya Katiba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika maoni yote haya umetolewa uchambuzi wa kitakwimu (quantitative analysis) na uchambuzi wa kihoja (qualitative analysis). Ninajadili uhalali wa kitafiti juu ya aina mbili hizi za maoni, nikianza na uhalali wa kitafiti kuhusu matokeo ya kitakwimu.

Msingi wa utafiti wa kitakwimu (quantitative research) ni idadi ya walioshiriki katika utafiti husika na jinsi washiriki hawa walivyopatikana. Kikubwa kabisa kinachoangaliwa katika utafiti wa kitakwimu ni jinsi wa washiriki walivyopatikana. Ili matokeo ya utafiti wa kitakwimu yaweze kuheshimika na kukubalika, na yaonekana kwamba yanawakilisha maoni ya watu katika eneo husika ambao hawakushiriki katika utafiti huo, ni sharti kwamba washiriki wapatikane kwa njia ya kinasibu (random sampling). Sasa kwa vigezo hivi tuangalie uhalali wa takwimu zilizopo katika ripoti ya Tume ya Warioba katika suala la muundo wa Muungano, ambalo ndilo suala tata kuliko yote katika Rasimu ya Katiba.

Kwa mujibu wa takwimu za ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (nyaraka ya nne katika ripoti ya Tume), idadi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu jambo hili ni 47,820, wakiwemo 26,625 kutoka Tanzania Bara na 19,351 kutoka Zanzibar. Waliotaka serikali tatu walikuwa ni asilimia 37.2 (takribani watu 17,789), waliotaka serikali mbili walikuwa ni asilimia 29.8 (takribani watu 14,250) na waliotaka Muungano wa mkataba walikuwa ni asilimia 25.3 (takribani watu 12,098). Kwa upande wa Zanzibar, asilimia 60.2 ya watu wote waliotoa maoni (takribani watu 11,649) walitaka Muungano wa mkataba na kwa upande wa Tanzania Bara asilimia 61.3 (takribani watu 16,321) walitaka serikali tatu. Kwa takwimu hizi wananchi walio wengi wa pande zote mbili za Muungano walioshiriki kutoa maoni kuhusu muundo wa Muungano walikuwa hawataki serikali mbili.

Sasa ni nini uhalali wa takwimu hizi kitafiti? Kama nilivyoeleza hapo juu, katika kupata uhalali wa matokeo ya utafiti takwimu (quantitative research) tunaangalia idadi ya walioshiriki na jinsi ambavyo washiriki hawa walipatikana. Pamoja na kwamba idadi ya walioshiriki kutoa maoni kuhusu Muungano inaonekana kuwa ni ndogo, kitafiti idadi hii ni kubwa sana. Sampuli nyingi duniani katika utafiti wa maoni (opinion poll) huwa na idadi isiyozidi watu 5,000. Kwa hiyo kwa Tume kuwafikia watu zaidi ya 40,000 ni idadi kubwa sana.

Tatizo kubwa kuhusu maoni ya wananchi katika ripoti ya Tume ya Warioba ni ukweli kwamba washiriki hawakupatikana kwa njia ya kinasibu (random sampling). Hawa ni watu waliojitolea kwenda kutoa maoni kwa hiari yao na kwa sababu zao na hawakuchaguliwa kama inavyofanyika katika tafiti za kimaoni (opinion polls). Njia hii ya kupata washiriki katika lugha ya kitafiti inaitwa ‘convenience sampling’. Hii ndio njia ya kupata washiriki ambayo inadharaulika kuliko zote katika utafiti takwimu na matokeo yatokanayo na njia hii huwa hayakubaliki kisayansi, na hakuna jarida la kitafiti makini linaloweza kukubali kuchapisha matokeo yatokanayo na maoni ya washiriki waliopatikana kwa njia hii. Ndio kusema, kisayansi, maoni ya wananchi katika ripoti ya Tume ya Warioba ni kiashiria tu (indicative) na hayawezi kutiliwa manani katika kufikia uamuzi wa maana na mkubwa.

Tungekuwa makini katika mchakato huu, tungeitisha kura ya maoni ya wananchi wote kuhusu Muungano kabla ya kuandika Katiba. Aidha, kama Tume ya Warioba ilihitaji kutumia matokeo ya utafiti takwimu katika kujenga hoja yake wangefanya utafiti wa kisayansi katika utaratibu wa ‘opinion poll’. Takwimu zilizopo katika ripoti ya Tume kwa sasa hazina uhalali wa kisayansi katika ulimwengu wa utafiti wa kitakwimu.

Ndio kusema msingi mkubwa wa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu katika ripoti ya Tume ya Warioba unapaswa kutokana na uzito wa sababu ambazo wananchi walizitoa kuhusu kwa nini wanataka muundo wa serikali tatu na sio wa serikali mbili uliozoeleka. Hivi ndiyo uhalali wa utafiti hoja (qualitative research) unavyojengwa. Utafiti hoja hauangalii idadi ya watu bali uzito wa hoja husika. Kwa maoni ya Tume, ambayo nami nakubaliana nayo, ili tuendelee na muundo wa serikali mbili itahitajika kufanyika ukarabati mkubwa sana. Serikali ya CCM ilifanya makosa makubwa kuiruhusu Zanzibar kufanya mabadiliko makubwa sana katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, ambayo kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya Muungano, wanadhani kwamba, kwa marekebisho haya ya Katiba ya Zanzibar, ilikuwa ni tangazo la Zanzibar kujitoa katika Muungano. Hili lilikuwa ni kosa kubwa la kisiasa, kiutawala na kisheria. Sasa hatuwezi kula keki na hapo hapo tuendelee kuwa nayo. Wataalamu wa mambo ya Muungano wanaeleza kwamba huwezi tena kuendelea na muundo wa serikali mbili bila kuifanyia ukarabati mkubwa Katiba ya Zanzibar, jambo ambalo linaonekana haliwezekani kwa sasa.

Katika ripoti yake, Tume ya Warioba imeainisha vizuri sana mlolongo wa matatizo ya muundo wa Muungano tangu enzi za kile kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa kisiasa Zanzibar” mwaka 1984. Tume imeeleza pia sababu zilizoainishwa na Tume zingine kuanzia na Tume ya Nyalali ya Mwaka 1991 na baadaye Tume ya Kisanga ya mwaka 1998 ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu. Tukumbuke kwamba Tume zote hizi ziliundwa na Serikali ya CCM na ziliongozwa na majaji walioteuliwa na Rais atokanaye na serikali hiyo. Kikubwa zaidi, Tume ya Warioba iliongozwa na kada wa CCM na ndani yake walijaa makada nguli wa chama hicho, akiwemo Mzee Salim Ahmed Salim na Mzee Joseph Butiku. Ukada wa wazee hawa hautiliki shaka, lakini pia ni watu ambao utaifa na uzalendo wao kwa nchi haujawahi kutetereka. Kwa hiyo, huu msimamo wa CCM wa kung’ang’ania serikali mbili sio msimamo wa CCM ya Nyerere. Kazi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba.

- Imeandikwa na Dk Kitila Mkumbo, imenukuliwa kutoka gazeti la Raia Mwema

Posted By Unknown21:12

MAMLAKA YA USALAMA WA SAFARI ZA BAHARINI YASITISHA SHUGHULI YA KITAFUTA MH370

Filled under:

 
Jamaa za abiria wa ndege hiyo wamekumbwa na majonzi makubwa.

                  
Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali baharini.


Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.


Dr Erik van Sebille, ambaye ni mtaalam wa maswala ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini Sydney, amefanya utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua ni wapi na vipi vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa vigumu sana kupata mabaki ya ndege hiyo.

Shughuli ya kuitafuta MH370 imesitishwa


" Ni eneo lisiloweza kukalika duniani, acha niseme. Upepo unaovuma ni mkali sana, mawimbi ni makubwa, ni mojawepo wa mawimbi makubwa zaidi baharini. Unapofika katika eneo hili la kusini, unaanza kuhisi athari za eneo la Antactica kwenye bahari. Hapa tunazungumzia dhoruba kali kali sana hususan wakati huu tunapoingia majira ya kupukutika," anasema Dr. Erik van Sebille.



Kadhalika amesema kuwa vifusi vilivyoenekana hapo jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi makali.


"Haitakuwa rahisi kabisa kupata kijisanduku cha kunasa habari. Mawimbi ya eneo hili ni makali na kwa hiyo vifusi ambavyo wametambua kwa sasa huenda vimehamishwa katika kipindi cha majuma mawili au matatu tangu ndege hiyo ianguka-na huenda vimesafiri kilomita alfu moja tayari. Na hii inaifanya vigumu kurejelea utafutaji kwa sababu bahari inabadilika sana hapa-ina vurugu ukipenda."


Hapo awali naibu waziri wa mashauri ya nchi za Kigeni wa China Xie Hangsheng, aliitaka serikali ya Malaysia kutoka ushahidi unaoelezea kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo la Kusini mwa bahari Hindi. Ndege hiyo ilitoweka kwenye mtambo wa Radar zaidi ya majuma mawili yaliyopita.


Posted By Unknown20:56

WAZIRI WA MALAYSIA ASEMA NDEGE ILIDONDOKA BAHARI YA HINDI,HAKUNA ABIRIA ALIYESALIA

Filled under:

 
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak
Shirika la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.

Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.

Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko.

Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.

Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.

Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.

Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.

Posted By Unknown11:49

ZIFAHAMU ATHARI ZA SABUNI ZITUMIKAZO KURUDISHA BIKIRA

Filled under:

KUWA mrembo ni pamoja na kujikubali jinsi ulivyo na jinsi utakavyojiweka soap soap Hata mtu akikupenda akupende  jinsi ulivyo. 

Pamoja na hayo kumekuwa na mambo mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya wanawake au wasichana kwa lengo la kufanikisha azma mbalimbali. Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.

Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.

Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa mwanamke na hata kuwa na mnato.

Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa  sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.

Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.

Mtaalam huyo Anasema  Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji  yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano  kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.

Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni  lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.

Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Dodoma, Fredrick  Luyangi anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.

Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.
Jamani wanawake wenzangu tubadilike Kuna wengine wameshazaa zaidi ya mara mbili lakini bado wanahangaika kurudisha maumbile yao yawe madogo na kuhangaika na kila aina ya sabuni inawezekana kweli katika hilo?





Chanzo;sifa yetu

Posted By Unknown04:51

UMOJA WA WAKULIMA WA CHAI WAMBURUZA MAHAKAMANI JANUARY MAKAMBA

Filled under:



UMOJA wa Wakulima wa Chai (UTEGA) Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto, Tanga unatarajia kumburuza mahakamani Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

Uamuzi wa UTEGA ulitolewa hivi karibuni katika mkutano mkuu maalumu wa UTEGA ulioitishwa kwa nia ya kutathmini njia bora za kisheria za kuhakikisha kiwanda cha chai kinafunguliwa na kudai fidia ya athari walizopata kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu kufungwa.

Kwa mujibu wa UTEGA uamuzi huo unatokana na hatua ya mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknelojia, kuitisha mkutano wa hadhara  uliotoa azimio la kufungwa kwa Kiwanda cha Mponde Tea Estates kinyume cha sheria za nchi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa UTEGA, William Shelukindo, alisema kwa mwaka mmoja tangu kiwanda kifungwe jitihada mbalimbali zimechukuliwa za kukinusuru zikiwemo kufanya kikao na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga.

Shelukindo alisema katika mkutano huo, Kamati ya Siasa iliagiza kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Usambara Tea Growers Association (UTEGA) kama ilivyopendekezwa na Makamba.

Shelukindo alisema kikao cha kamati ya utendaji ya UTEGA cha Septemba 14, 2013 hakikuafikiana na maagizo hayo.

“Kamati yetu ya utendaji ilipingana na wazo la Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa kwa sababu kubwa kwamba, endapo tutafanya  uchaguzi kabla ya wakati, tutakuwa tumekiuka Katiba ya UTEGA,” alisema Shelukindo.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa walifanya kikao kingine kati ya uongozi wa UTEGA, na maofisa wa Hazina (Msajili wa Hazina), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na Msimamizi wa mali za serikali zilizouzwa (CHC) Consolidated Holdings Cooperation.

Akifafanua zaidi Shelukindo alisema kuwa kikao kilibainisha wazi kwamba suala la Kiwanda cha Chai cha Mponde ni la kisheria kwa vile kiwanda pamoja na shamba la Sakare viliuzwa na serikali kwa UTEGA, na hakuna upande wowote wenye tatizo na umoja huo.

Mwenyekiti aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, Mwenyekiti wa Lushoto Tea Company, Nawab Mulla, alifanya kikao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, Februari 23, mwaka huu, mkoani Dodoma.

Alisema kuwa katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alishauri kwamba kiwanda kifunguliwe kwani wakulima wa chai wanateseka sana na suala hilo linamuumiza kichwa chake.

Katika hoja hizo, ilibainika wazi kuwa kiwanda hicho kilifungwa kwa madai ya kuchochewa na Mbunge wa Bumbuli kwenye mkutano wa hadhara wa Mei  26 mwaka jana uliofanyika ndani ya kiwanja kilichopo kiwandani hapo.

Mara baada ya mkutano huo msaidizi wa mbunge alianza kusambaza fomu kwa wakulima wa chai ili wazijaze kumuunga mkono, hatua aliyoichukua ya kufunga kiwanda hicho kinachotoa huduma kwa wakulima wa chai wa vituo vya Lushoto na Korogwe.

Wajumbe hao waliiagiza Mponde Tea Estates Company Ltd, iende mahakama kupata kibali cha kufungua kiwanda ili wakulima wasiendelee kuteseka.

Kwa mujibu wa mkutano huo, mashitaka mengine ambayo wanakusudia kufungua mahakamani ni kudai fidia iliyotokana na kufungwa kiwanda hicho na kukisababishia hasara kubwa.

Posted By Unknown04:31

BAADA YA KUBWAGANA NA RAY ,MAINDA APATA UJAUZITO

Filled under:

Siku chache baada ya kuliambia gazeti ndugu la hili, Amani kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa chango hivyo inambidi azae, super lady wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ anadaiwa kuwa mjamzito, Ijumaa Wikienda limechimba kila ‘engo’.

MUONEKANO
Habari zilieleza kwamba kimuonekano, Mainda aliyezoeleka kuonekana mwembamba, sasa ameanza kunenepa huku kitumbo nacho kikianza kuwa kikubwa.

Habari kutoka kwa mmoja wa mashosti zake aliyeomba hifadhi ya jina, zilidai kwamba kila amuonapo Mainda anagundua kuwa ana mabadiliko fulani ndani ya mwili wake hasa tumbo lake kuongezeka ukubwa.
“Unajua Mainda ni msiri sana hasa katika kipengele cha kuzungumzia mwili wake, kila tukimuuliza shosti wetu kama ni mjamzito anakataa.

“Anadai eti ana matatizo ya ugonjwa wa chango lakini ukimwangalia tumbo unaona linazidi kukua, binafsi mimi naamini ni mjamzito ila yeye anafanya siri,” alidai rafiki huyo.

APELEKWA HOSPITALI
Habari zilizotufikia zilidai kuwa mwanadada huyo alipelekwa kwenye Hospitali ya Kinondoni maarufu kwa jina la kwa Dokta Mvungi jijini Dar.

Siku hiyohiyo mwanahabari wetu alizama hospitalini hapo ambapo alikutana na vizuizi vingi kwa kuwa moja ya masharti huruhusiwi kuingia wodini bila kufuatana na ndugu wa mgonjwa.

Katika jitihada za kuthibitisha kama Mainda kalazwa hapo na kujua kinachomsumbua, mmoja wa madaktari (jina linahifadhiwa) ambaye anamfahamu mwandishi wetu alimtonya kuwa ni kweli Mainda alifikishwa hospitalini hapo.

UGONJWA, UJAUZITO
Kuhusu ugonjwa uliompeleka hospitalini hapo na habari kuwa ni mjamzito, dokta huyo alisema: “Ninavyojua mimi, ugonjwa ni siri ya daktari na mgonjwa au na ndugu. Nadhani muulize mwenyewe, akipenda atakwambia. Ni kweli alikuwepo na amesharuhusiwa.”

Baadaye mwandishi wetu alikwenda hadi nyumbani kwa Mainda, Kijitonyama, Dar lakini alijibiwa na majirani kuwa hayupo kwa muda mrefu.
h 

APOKEA SIMU
Hata hivyo, juhudi za kumpata, ziliendelea ambapo alitumiwa ujumbe mfupi, alipopigiwa akapokea.
Katika mazungumzo yake na mwandishi, Mainda alikiri kuwa anasumbuliwa na chango na kwenda hospitali lakini alikataa kuzungumzia ishu ya ujauzito.
“Mimi nilishasema nasumbuliwa na chango, huo ujauzito unaosema, hata kama upo, tusubiri kwani huwa haufichiki,” alisema Mainda.

UTATA
Baada ya habari kuwa ya mjini, ishu hiyo iliibua utata kuwa kama ni ugonjwa wa chango, inawezekana mtu akazidiwa kiasi hicho hadi kukimbiza hospitali?
Pia ilihojiwa kuwa kama kweli ni mjamzito, je, baba wa kiumbe hicho ni nani?

NI MIMBA YA PILI?
Kama kweli Mainda atakuwa mjamzito basi itakuwa ni mimba ya pili baada ya kukiri kuwa aliwahi kuchoropoa ya aliyekuwa mtu wake, mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye walishamwagana.

Chanzo :Global Publisher

Posted By Unknown03:32

HATUTAKUBALI KUJADILI RASIMU NYINGINE

Filled under:

 
Bunge Maalumu la Katiba sasa lipo katika hati hati ya kuendelea kutokana na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutangaza kuwa hawatakuwa tayari kujadili rasimu tofauti na iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba bungeni.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni, viongozi wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, walisema wataitetea rasimu hiyo, ndani ya Bunge na kwenye Kamati.
“Rais Jakaya Kikwete amekuja bungeni siyo kufungua Bunge la Katiba bali kaja na mapendekezo ya rasimu ya CCM, sisi tutajadili rasimu ya wananchi ya Jaji Joseph Warioba ambayo inazungumzia muundo wa Muungano wa Serikali tatu,” alisema Profesa Lipumba.
Kutokana na msimamo huu wa Ukawa huenda Bunge litakwama kwani kwa mapendekezo ya CCM yenye Muundo wa Muungano wa Serikali mbili ni lazima kuandikwa upya Rasimu ya Katiba au kufanyika mabadiliko makubwa.
Profesa Lipumba alisema katika majadiliano juu ya rasimu, Ukawa watajikita kutumia Rasimu ya Katiba waliyopewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo imeeleza mapendekezo kwa nini yamefikiwa katika kila hoja,” alisema.
Hata hivyo, alisema wamesikitishwa sana na Rais Jakaya Kikwete, badala ya kufungua Bunge alijikita katika kuchambua rasimu na kuikosoa tume aliyoiunda mwenyewe.
“Rais Jakaya Kikwete siyo tu amemdhalilisha Jaji Warioba pamoja na wajumbe wa Tume, bali amewadhalilisha wananchi waliotoa maoni kwani hata takwimu alizotoa za kupinga rasimu siyo za kweli,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema muundo wa Serikali tatu ndio mawazo ya wananchi ambayo yamekusanywa na watu wenye heshma wakiwapo Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na Jaji Augustino Ramadhani ambaye pia amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Alisema kauli za Rais badala ya kuimarisha umoja zimewagawa Watanzania kwani ametoa vitisho ambavyo havina sababu hasa kwa Wapemba bila kujua kuna Wanyamwezi wanaoishi Zanzibar.
Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema kwa kauli ya juzi ya Rais Kikwete, kutangaza kuwapatia Zanzibar; watu, ardhi, mamlaka kamili na kusimamia uhusiano wa kimataifa ni kuvunja rasmi Muungano,
Mbatia alisema Rais Kikwete pia amewagawa Watanzania katika kauli zake ikiwa ni pamoja na ile ya Wapemba kwa kulima vitunguu katika Jimbo la Kibakwe kana kwamba ni makosa.
Alisema wamesikitishwa na Rais kuacha kufungua Bunge badala yake katumia taarifa potofu za mitaani kuligawa Bunge na kuwadhalilisha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Hakuna asiyejua sasa tupo katika mgogoro mkubwa wa kikatiba, Zanzibar tayari ni nchi kamili kutokana na mabadiliko ya 10 ya katiba yao waliyoyafanya mwaka 2010 baada ya kupitisha dhana ya kuwa Zanzibar ni nchi,” alisema.
Mbowe
Mbowe alisema Rais amevunja maridhiano na hata kushindwa kusikiliza maoni ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Seneta Amos Wako kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwe.
Alisema Serikali ya Kenya ilichakachua maoni, ilichakachua rasimu na kusababisha vurugu kubwa jambo ambalo linaweza kutokea kwa Tanzania.
“CCM wasijidanganye kwa wingi wao bungeni hakika katika hili tutatetea madai na maoni ya wananchi hadi mwisho,” alisema

Posted By Unknown03:02

BUNGE LA KATIBA KIZUNGUMKUTI

Filled under:



Kwa neno moja unaweza kusema kwamba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa ujumla wako “njiapanda”.

Hii ni baada ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge hilo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuibua mambo mazito ambayo kimsingi yanatofautiana na mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Huku wananchi wakijiuliza nini hatima ya Bunge hilo baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wajumbe ambao wiki hii ndiyo wanaanza kujadili rasimu hiyo, watakuwa katika wakati mgumu wa kuamua wafuate maoni ya nani, kati ya viongozi hao wawili.
Ingawa Rais Kikwete amesema mara kadhaa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba ndiyo waamuzi. Mambo mengi aliyoibua yanaonyesha kutokubaliana kwake na baadhi ya maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu, ambayo Jaji Warioba amewahi kusema kuwa yanatakiwa kuheshimiwa.
Wakizungumzia tofauti hizo, mjumbe wa Bunge la Katiba, Ezekiah Oluoch alisema kauli za Rais Kikwete na Jaji Warioba zimezidi kuwagawa wajumbe wa Bunge hilo kwa maelezo kuwa tangu awali wajumbe hao walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili; ya wanaotaka muundo wa Muungano uwe wa serikali tatu na wale wanaotaka serikali mbili.
Alisema kama suala la muundo wa Serikali likishindikana kupatiwa mwafaka ni vyema likarudishwa kwa wananchi ili wapige kura ya maoni kuchagua aina wanayoitaka, kisha suala hilo lirejeshwe tena katika Bunge la Katiba kwa ajili ya kuboreshwa.
“Rais alipoanza kuzungumza alikuwa kama mkuu wa nchi lakini mwisho wa hotuba yake aligeuka kuwa mwenyekiti wa CCM. Kifupi alichokizungumza kimekwenda tofauti na wadhifa wake,” alisema.
Naye Deo Filikunjombe alisema: “Nadhani kwa hotuba hizi mbili, kazi ya wajumbe wa Bunge la Katiba itakuwa rahisi. Maana sasa wameshajua uzuri na ubaya wa serikali tatu na mbili.
“Hata kama kutakuwa na tofauti, wananchi ndiyo watakuwa wa mwisho kuamua kama Katiba hii ipite au isipite. Tunachotakiwa wajumbe ni kuwa makini na uamuzi wetu.”
Naye Yusuf Manyanga alisema: “Bunge la Katiba limejaa watu wenye busara. Sidhani kama tutashindwa kuelewana maana hata katika biashara ya utumbo inzi ni wengi lakini utumbo unauzika.”
Katika hotuba yake aliyoitoa Ijumaa iliyopita Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka.

Muundo wa Serikali
Jambo kubwa pengine kuliko yote linaloliweka Bunge na wananchi njiapanda ni kuhusu muundo wa Serikali na Rais Kikwete ameweka wazi kuegemea katika muundo wa serikali mbili, wakati rasimu inayojadiliwa imependekeza serikali tatu.
Rais Kikwete akisema iwapo mfumo wa serikali tatu ukipita ni lazima serikali ya tatu ijengewe msingi imara kwa sababu haitakuwa na chanzo cha uhakika cha mapato yake yatakayoiwezesha kusimama yenyewe. Rasimu inasema Serikali ya Muungano itakuwa na mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa, mapato yasiyo ya kodi, michango ya nchi washirika na mikopo ya ndani na nje.
Kuhusu ulinzi, Rais Kikwete alisema: “Kama tunataka serikali ya tatu lazima tuitengenezee misingi ya uhakika na kuhoji nani atayeidhamini serikali ya tatu virungu, pingu, magari ya kuwasha, majeshi au bunduki.”
Lakini Jaji Warioba, ambaye tayari alishasema msimamo huo ni maoni binafsi ya Rais Kikwete na hawezi kuyazungumzia, aliwatoa hofu wananchi na wajumbe akisema muundo wowote wa Serikali utakuwa na changamoto zake, kwamba hata muundo wa serikali tatu utakuwa na changamoto zake, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama ingawa hazitakuwa kubwa kama inavyofikiriwa.
Warioba alifafanua kuwa gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika eneo la ulinzi na usalama, yaani Jeshi la Wananchi, Polisi, Usalama wa Taifa na mambo ya nje na kwamba gharama hizo hazibadiliki. Alisema zitabaki kama zilivyo bila kujali kama ni muundo wa serikali mbili au serikali tatu.
Alisema tangu Muungano uundwe, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimekuwa zikiongeza wizara, mikoa, wilaya na taasisi mbalimbali za kiutawala ili kuongeza ufanisi na hivyo kuongeza matumizi ya Serikali, lakini gharama zinazoonekana ni hizo za serikali ya tatu.

Mambo yasiyotekelezeka
Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema baadhi ya vifungu vya Katiba vinayopendekezwa vimekuwa na mambo mengi ambayo hayapaswi kuwemo katika Katiba, bali yangekuwa katika sheria zinazotafsiri utekelezaji wa Katiba yenyewe. Kwa mfano, alisema ikiwa kila jambo likiwekwa katika Katiba kuna hatari ya Serikali kujikuta inalaumiwa au hata kufikishwa mahakamani kila wakati kwa madai ya jambo moja au jingine ambayo haina uwezo nayo.
Lakini Warioba alisema katika nchi yoyote, msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba ambayo ni sheria kuu au sheria mama. Hivyo sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa Katiba. Aliongeza kuwa Katiba ni makubaliano ya wananchi kuhusu utaratibu na kanuni za uendeshaji wa mambo mbalimbali katika nchi yao, inaweka mfumo wa uendeshaji wa nchi kwa kuainisha misingi ya taifa, mgawanyo wa madaraka na majukumu ya mihimili mikuu ya dola, usimamizi wake, mgawanyo na ukomo wa mamlaka ya vyombo mbalimbali vya dola.

Mipaka ya nchi
Kuhusu mipaka ya nchi, Rais Kikwete alisema si sahihi rasimu ya Katiba kusema tu “eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari”.
Alisema maelezo hayo yameacha kutambua, kwa upande wa Tanzania Bara, sehemu ya maziwa na mito ambayo ni kubwa na ni lazima mipaka hiyo ya maziwa na mito iwekwe katika Katiba ili kuzuia nchi fulani kudai ziwa au mto fulani ni wao.

Kuhusu suala hilo, Rasimu ya Tume imependekeza eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lijumuishe eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari, kama ilivyoainishwa katika Katiba za Uhuru za nchi hizo mbili.
Kupoteza ubunge
Jambo jingine ambalo linaonekana halikumfurahisha Rais Kikwete katika Rasimu ni suala la mtu kupoteza ubunge kwa sababu ya kuugua kwa miezi sita mfululizo.
“Kwa maoni ya watu wengi suala hilo ni ukatili ambao haustahili kufanywa na Katiba,” alisema Kikwete.
Alisema kuugua ndiyo ubinadamu na wakati mwingine mbunge anaweza kupata ajali wakati akiwatumikia wananchi wa jimbo lake.
Kauli hiyo ni tofauti na inavyoelezwa katika Ibara ya 128(1)(d) ya Rasimu ya Katiba ambayo inasema: ‘Mbunge atakoma kuwa mbunge ikiwa atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa muda wa miezi sita mfululizo kutokana na maradhi au kizuizi ndani ya gereza.

Vipindi vitatu vya ubunge
Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema ni mapema mno kuanzisha utaratibu wa ukomo wa vipindi vitatu vya mtu kugombea ubunge na kusisitiza kuwa jambo hilo litawanyima watu wenye maarifa na uzoefu mzuri wa uongozi katika nafasi ya ubunge.
Hata hivyo, Jaji Warioba alisema pendekezo hilo linatokana na maoni ya wananchi waliotaka kuwapo ukomo wa ubunge ili kuondoa dhana ya umiliki wa jimbo la uchaguzi, kutoa fursa kwa wananchi wengine wenye uwezo kugombea nafasi ya ubunge na kuongeza uwajibikaji wa wabunge katika majimbo.

Kumwondoa mbunge
Rais Kikwete alisema kitendo cha kumwondoa mbunge katikati ya kipindi chake cha uongozi kuna athari na kuwataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuzitafakari
Alisema jambo hilo linaweza kuanzisha misuguano kwenye majimbo na kuwaacha wabunge wasifanye kazi zao kwa utulivu bali wawe wanajihami dhidi ya wapinzani wao kuwatengenezea fitna za kuwatoa.

Kuhusu suala hilo, Jaji Warioba alisema wananchi wanaweza kumwondoa mbunge madarakani iwapo atakwenda kinyume na masilahi ya wapigakura, kushindwa kutetea kero zao na kuacha kuishi au kuhamisha makazi katika jimbo husika.
Mawaziri kutokuwa wabunge
Katika maelezo yake Rais Kikwete alisema ni vigumu kutenganisha uwaziri na ubunge kwa maelezo kuwa mawaziri wanatakiwa kuwepo bungeni ili kujibu hoja za Serikali, lakini Jaji Warioba alisema nia ya pendekezo hili ni kutenganisha mamlaka na madaraka ya mihimili na kuliwezesha Bunge kufanya kazi yake ya  
kuisimamia Serikali.
Wakati huohuo, Bunge la Maalumu la Katiba leo litafanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati ikiwamo Kamati ya Uongozi itakayoshauri suala la upigaji kura ambalo liliwekwa kiporo kutokana na mgawanyiko wa wajumbe wa ama iwe ya siri au ya wazi
.
Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alisema leo Mwenyekiti wa Bunge Samuel Sitta atatangaza kamati 12.

Posted By Unknown02:50