Saturday 28 December 2013

JAIRO,NYONI WASAMBALATISHWA KIMYAKIMYA

Filled under:




Serikali imewasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo huku ikimpandisha cheo aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa.

Nyoni alisimamishwa kazi pamoja na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa  na wote kwa pamoja walikuwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma.

Jairo kwa upande wake alisimamishwa kazi kutokana na kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bajeti ya wizara yake, katika mwaka wa fedha 2011/2012 na sasa ameondolewa kwenye utumishi wa umma, huku Bunge likiwa bado halijapata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yanayomuhusu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.

“Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa kuazima watumishi wa umma.

Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na kule TRA hakuwa na tatizo,” alisema Balozi Sefue.

Kuhusu Dk Mtasiwa alisema: Uteuzi wa Dk Mtasiwa ulikuwa wazi na hata alipoapishwa mambo yote yalitangazwa hadharani.” Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: “Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma.” Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.

“Siyo kwamba ameajiriwa TRA, amerudi tu kwenye ajira yake ya zamani, alikuwa akifanya kazi hapa akaazimwa na sasa amerudi,” alisema Kayombo na kuongeza: “Kwani amefanya kosa gani? Kuna mashtaka yoyote aliyofanya unaweza kuyathibitisha?”

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bernard Mchomvu ambaye alisema Nyoni alishasafishwa na Serikali ndiyo maana wamempokea. “Yule aliazimwa tu na Serikali…Sasa kama Serikali imesham-clear sisi tutamkataaje?” alihoji na kuongeza:

“Kwa sababu sikumwomba huyo mtu, nimeambiwa kwamba huyo yuko safi mimi nifanyeje? Unajua watu wanafurahia wengine wakipata matatizo, hata kama mtu ameua, basi walete ushahidi. Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu.”

Jitihada za kumpata Nyoni kupitia simu yake ya mkononi hazikuzaa matunda, baada ya simu yake kupokelewa na sauti ya kiume iliyosema kuwa namba imekosewa.

Hata alipotafutwa kwa namba nyingine, simu ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa Wizara ya Afya na kwamba namba hiyo kwa sasa haitumii tena. Alipotafutwa kwa njia ya simu, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah, alisema suala hilo aulizwe msemaji wa Serikali juu ya Bunge.

“Ongea na msemaji wa Serikali juu ya mambo ya Bunge,” alijibu kwa njia ya ujumbe wa simu.
Lukuvi
Naye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hayuko ofisini.
“Niko ‘airport’ nasafiri kwenda South Africa, msinipigie simu, siko ofisini hadi mwezi ujao (Januari),” alisema Lukuvi na kukata simu yake.
Awali alipoulizwa kwa njia ya simu baada ya mwandishi kuelezea suala hilo alisema ana kazi nyingi na kwamba apigiwe baadaye.

Makani azungumza
Mwenye wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza tuhuma hizo, Ramo Makani, ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, akizungumza na gazeti hili kuwa: “Ni kweli mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza suala hilo, kwa utaratibu kamati kama hiyo huundwa kwa kanuni za Bunge kwa kupewa majukumu maalumu… Kama mbunge tu ningefurahi kusikia taarifa ya Serikali bungeni baada ya kupata taarifa ya Bunge,” alisema Makani na kuongeza:

“Serikali iliahidi kuleta taarifa bungeni ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge. Mimi sikumbuki kama taarifa hiyo imeshasomwa bungeni, labda wewe mwenzangu umebahatika kuisikia. Kwa hiyo bado tunasubiri… Kama Serikali imechukua hatua, mimi sijui.”

Tuhuma za Nyoni
Nyoni alituhumiwa kutenda makosa saba ambayo yaliainishwa wakati wa mgomo wa madaktari ulioanza Januari mwaka jana, hali iliyomlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutangaza kumsimamisha kazi ili uchunguzi uweze kufanyika.

Baadhi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili ni pamoja na kujilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) nje ya mshahara aliokuwa akilipwa na Serikali, kutengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na ofisa ununuzi wake kwa kujiweka yeye mwenyewe.

Tuhuma nyingine zilikuwa kulazimisha Wizara ya Afya kununua sare za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za ununuzi.

Katika mikutano yote inayofanyika wizarani, alikuwa akilazimisha Kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa zabuni ya kutoa huduma ya chakula kwa washiriki tangu alipotua wizarani kama Katibu Mkuu.

Sakata la Jairo
Hatua ya kumwondoa Jairo katika utumishi wa umma nayo imefanyika kimyakimya kwani Serikali hadi sasa haijawasilisha bungeni majibu ya maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo ambalo pia liliwagusa watumishi wengine wa Wizara ya Nishati na Madini. 

Maazimio hayo ni yale yaliyotokana na matokeo ya uchunguzi  wa Kamati Teule ya Bunge   iliyoongozwa na Makani na kubainisha kuwapo kwa makosa ya kiutumishi na kijinai ambayo yangewafikisha baadhi ya watumishi hao katika vyombo vya sheria.

Mbali na Jairo, kamati hiyo ilipendekeza kuwajibishwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Hata hivyo, ni Jairo pekee kati ya hao aliyewajibishwa kwa kusimamishwa kazi na baadaye kuondolewa katika wadhifa wake. Luhanjo alistaafu utumishi wa umma bila kuchukuliwa hatua zozote wakati Utouh anaendelea na wadhifa wake.

Pia katika taarifa yake, Kamati Teule ilisema utaratibu wa uchangishaji wa fedha Sh418.081 milioni uliofanyika katika Wizara ya Nishati na Madini haukuwa na uhalali kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni za Fedha za Umma.

Pamoja na mambo mengine, Bunge liliazimia kwamba ufanyike ukaguzi wa kiuchunguzi (forensic audit) kwa matumizi ya Sh214 milioni, ambazo kati ya hizo Sh126 milioni Kamati Teule ilikataa maelezo ya matumizi yake na Sh88 milioni ni zile zinaotajwa kwamba zilitumika katika kugharimia semina kwa wabunge.

Azimio jingine ni lile lililoitaka Serikali iviagize vyombo vya dola kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kughushi na ubadhirifu zilizoelezwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kama ilivyoelekezwa.

Baada ya kufikiwa kwa maazimio hayo, Serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe iliahidi kuyafanyia kazi na kuwasilisha majibu bungeni.

“Kwa sababu ya ukubwa na uzito wa taarifa hii, ni vigumu kuitolea majibu yote hapa hapa, ninachoweza kufanya ni kuipokea pia tutakapokuja katika Mkutano wa Sita, tunatarajia kuleta majibu ya hoja zilizomo kwenye taarifa hii,” alisema Chakawe ambaye sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria.

Posted By Unknown09:22

Monday 23 December 2013

MGOGORO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYANI KITETO WANNE WAPOTEZA MAISHA

Filled under:



Mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto, Manyara umeingia sura mpya baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuwavamia wakulima na kusababisha vifo vya watu wanne.

Taarifa ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akilimali Mpwapwa, ilieleza kati ya watu hao, watatu walikufa hapo hapo na mmoja akiwa njiani kupelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma na majeruhi saba.

Alisema usiku wa kuamkia Jumamosi, wafugaji waliingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima katika eneo la Kijiji cha Olupoponyi, Kitongoji cha Kalakala.

Alisema kitendo hicho ndicho kilichosababisha wakulima nao kuanza kuwazuia wafugaji na mifugo yao kutolisha mimea yao, lakini baada ya hapo wafugaji walionekana kuwa wabishi na kuanza kuwashambulia.

“Kutokana na majibishano kati ya wafugaji na wakulima ilisababisha wakulima watatu kupoteza maisha na majeruhi saba ambao walilazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto,” alisema.

Mauaji hayo yalitokea Kijiji cha Olupoponyi, Kitongoji cha Kalakala ambapo Mbunge wa Kiteto na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Benedict Ole-Nangoro (CCM) anaishi.

Imeelezwa jamii ya wafugaji wa Kimasai waliwavamia wakulima wakiwa katika vibanda vyao wamelala, saa 7 usiku na kuanza kuwashambulia kwa mapanga, sime, mikuki, visu na risasi.

Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema kitendo ambacho kinafanywa na wafugaji dhidi ya wakulima ni cha kinyama zaidi.

Hata hivyo, alieleza kushangazwa na serikali kufumbia macho mgogoro huo ambao kimsingi ni wa miaka mingi.

“Wafugaji wa jamii ya Kimasai wamekuwa wakiwaua wakulima mara kwa mara na wala suala hili si geni, viongozi wa ngazi ya juu wamekuwa wakiambiwa masuala haya, lakini kinachoshangaza ni kuona ukimya wa viongozi,” alisema.

Mbali na hilo, alimshambulia mbunge wa Kiteto, Ole-Nangoro kuwa ni kati ya viongozi wanaochochea chuki na kukuza ukabila katika Wilaya ya Kiteto.

Hivi karibuni, Ndugai alifanya mkutano na wakulima katika mji mdogo wa Kibaigwa, wilayani Kongwa na kuwaeleza kuwa Wilaya ya Kiteto kwa sasa imechafuka kutokana na viongozi wake kuwa na tabia ya kuendekeza ukabila.

Mbali na kuwepo na vitendo vya ukabila na ubaguzi, aliwataja Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Elaston Mbwilo kuwa wanahusika kwa kiasi kikubwa kuchochea mgogoro kutokana na kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji.

Posted By Unknown11:23

DK.MGIMWA AZUSHIWA KIFO

Filled under:



WAKATI mawaziri wanne wameng’olewa na wengine walioitwa mizigo wanatarajiwa kutimuliwa wakati wowote, Rais Jakaya Kikwete yupo katika wakati mgumu wa kusaka warithi wa nafasi hizo,

Ugumu wa kusaka warithi wa mawaziri hao, umeongezeka zaidi jana baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa kuzushiwa kifo kutokana na afya yake kuzorota.

Hata hivyo, uvumi huo ulioenezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi na kupitia mitandao ya kijamii, haukuwa sahihi, lakini taarifa zaidi kuhusu afya za Waziri Mgimwa zinasema kuwa atahitaji muda mrefu kupumzika, hivyo nafasi yake lazima izibwe na waziri mwingine kutokana na unyeti wake.

Mawaziri walioondolewa madarakani ni Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi).

Kuondolewa kwa mawaziri hao pia kunaelezwa kumelenga kumnusuru Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amekuwa akitajwa kwa kushindwa kuwasimamia mawaziri walio chini yake.

Kuondoka kwa mawaziri hao, kutamsaidia au kumwongezea mzigo Rais Kikwete kutimiza mapendekezo ya Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyotaka awaondoe mawaziri saba iliyowaita ‘mizigo’.

Wadadisi wa mambo ya siasa, wanasema kuwa mazingira ya kupata baraza jipya la mawaziri, yanampa wakati mgumu sana Rais Kikwete kufanya uamuzi wa nani aingie na nani atoke.

Jina la mbunge mpya wa kuteuliwa na rais, Dk. Asha Rose Migiro, limekuwa likitajwa mara nyingi kwamba hatua ya kuingizwa ndani ya Bunge hivi karibuni, huenda kuna nia ya kutaka kumteua kuwa mmoja wa mawaziri, na sasa baada ya kutemwa kwa mawaziri hao wanne turufu inaelekezwa kwake kuwa miongoni mwa watakaoziba moja ya nafasi.

Hata hivyo, duru nyingine za siasa zinasema nafasi ya Dk. Migiro kuteuliwa kushika wizara yoyote ni finyu kutokana na ukweli kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinamhitaji sana kwenye sekretarieti ambako anaongoza Idara ya Mambo ya Nje.

Chini ya utaratibu mpya, mjumbe wa sekretarieti, haruhusiwi kuwa waziri na ndiyo maana Januari Makamba, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, alilazimika kuachia nafasi ya ujumbe wa sekretarieti mara baada ya kuteuliwa kuingia katika Baraza la Mawaziri.

Inaelezwa kuwa tangu alipoingia kwenye sekretarieti, Dk. Migiro kwa kutumia uzoefu wake mambo ya kimataifa amekuwa kiungo kikubwa kwa CCM na mataifa ya nje.

Mjumbe mwingine wa sekretarieti anayetajwa kuwamo kwenye baraza jipya ni Mwigulu Nchemba ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.

Majina mengine yanayotajwa miongoni mwa wabunge ni pamoja na Dk. Khamis Kigwangala, Peter Serukamba ambaye ameonyesha uwezo mkubwa tangu alipochaguliwa kuongoza Kamati ya Bunge ya Miundombinu, ingawa nafasi yake kwenye baraza jipya inaelezwa kuathiriwa na uhusiano wake na Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Katika majina hayo, yapo pia majina ya waliojiita wapambanaji wa ufisadi kama Anne Kilango Malecela, James Lembeli na wabunge wengine mwiba kwa CCM kama Kangi Lugola na Deo Filikunjombe.

Posted By Unknown11:11

INTERNATIONAL AMBASADOR SCHOLARSHIP AT UNIVERSITY OF WEST LONDON IN UK, 2014

Filled under:



University of West London is offering 100 international ambassador scholarships. Students are eligible to apply for the scholarship if they have been offered a place to study on a full-time undergraduate or postgraduate course at the University of West London, commencing in September 2014. Scholarship will be awarded on a competitive basis to candidates who demonstrate enthusiasm and the ability to be an excellent International Student Ambassador. The deadline for applications for September 2014 is Friday 15 August 2014.

Study Subject(s): Scholarships are provided to learn any of the courses offered by the University of West London.
Course Level: 
Scholarships are available for pursuing undergraduate or postgraduate degree level at University of West London.
 

Scholarship Provider: University of West London, UK
Scholarship can be taken at:
 UK

Eligibility: Students are eligible to apply for the scholarship if they have been offered a place to study on a full-time undergraduate or postgraduate course at the University of West London, commencing in September 2014.

Scholarship Open for International Students: International Students can apply for these scholarships.

Scholarship Description: The International Ambassador Scholarship has made a big difference to my life. It reduces the financial burden, but most importantly, it makes me and my family proud.’ The International Ambassador Scholarship recognizes and provides financial support for outstanding students who wish to act as ambassadors for the University of West London.
Number of award(s): 100 scholarships are offered.
Duration of award(s): Scholarships are offered for the duration of the program.

What does it cover? For applicants applying to start in September 2014, University is offering 100 scholarships worth up to £5,000.
Selection Criteria: The International Ambassador Scholarship will be awarded on a competitive basis to candidates who demonstrate enthusiasm and the ability to be an excellent International Student Ambassador.
Notification: Not Known

How to Apply: Students can apply for our International Ambassador Scholarships by completing a scholarship application form (158 kb).

Scholarship Application Deadline: The deadline for applications for September 2014 is 5pm on Friday 15 August 2014.
Further Official Scholarship Information and Application

Posted By Unknown09:40

SHANDONG PROVINCIAL GOVERNMENT SCHOLARSHIP FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN CHINA, 2014/15

Filled under:



Shandong Provincial Government offers full scholarship for international students. This scholarship is available for pursuing undergraduate and language program at Qingdao University in China

Applicants shall be foreigners who are sound and age from 18 to 40. Government scholarship will include full tuition Fee, Accommodation Fee, Fee of Comprehensive Insurance for international students in China. The deadline for sending documents to the recommending institute is May 30th, 2014, to International Students’ Office is June 13th, 2014 and Applicants can directly submit documents to International Students’ Office before June 13th, 2014.

Study Subject(s): Scholarship is provided to learn any of the courses offered by the Qingdao University.  
Course Level: Scholarship is available for undergraduate and language program at Qingdao University in China.  
Scholarship Provider: Shandong Provincial Government  
Scholarship can be taken at: China

Eligibility: -Applicants shall be foreigners who are sound and age from 18 to 40.
-Applicants shall have gotten good marks and not been awarded with other scholarships.
-Applicants shall be students, who will enroll in September, 2014.


Scholarship Open for International Students: International students can apply for this scholarship.

Scholarship Description: Tuition Fee (2014-2015), Accommodation Fee, Fee of Comprehensive Insurance for International Students in China. Applicants shall be foreigners who are sound and age from 18 to 40.Applicants shall have gotten good marks and not been awarded with other scholarships and shall be students who will enroll in September, 2014.

Number of award(s): Not Known

Duration of award(s): Scholarship is awarded for one academic year (2014/15).

What does it cover? Government scholarship will provide full tuition Fee (2014-2015), Accommodation Fee, Fee of Comprehensive Insurance for International Students in China.

Notification: Not Known
How to Apply: Applicants should submit the application form by post.
Scholarship Application Deadline: The application deadline for submitting student’s application documents to the recommending institute is May 30th, 2014. The application deadline for submitting documents to International Students’ Office is June 13th, 2014. Applicants without recommending institute can directly submit documents to International Students’ Office before 17:00 pm on June 13th, 2014.
Further Official Scholarship Information and Application

Posted By Unknown09:32

WABUNGE WANG'ANG'ANA KUMNG'OA PINDA

Filled under:



 Baadhi ya wabunge wameanzisha mkakati wa kumwondoa madarakani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kile wanachodai kuwa hawaridhishwi na utendaji wake serikalini.

Hiyo ni dalili kwamba kung’oka kwa mawaziri wanne kutokana na matokeo ya ripoti ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili hakujamnusuru Pinda, kwani baadhi ya wabunge wanaendelea na msimamo kwamba naye ajiuzulu kwa kushindwa kuwasimamia wenzake.

Mawaziri waliong’oka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao kutokana na ripoti iliyowasilishwa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni Mawaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete inatafsiriwa na wengi kama njia ya kuwapoza wabunge na kumwokoa Pinda ambaye ikiwa atang’oka itamaanisha kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili jana zinasema wabunge 26 wametia saini fomu maalumu ya kutaka Bunge litumie mamlaka yake ya kikatiba kumng’oa Pinda kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.

Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alisema hili jana kuwa ukusanyaji saini za wabunge aliouanzisha Ijumaa jioni unakwenda vizuri.

“Kung’oka kwa mawaziri wale wanne inatosha kuthibitisha kuwa Pinda amepoteza uhalali wa kuwa Waziri Mkuu kutokana na kushindwa kuwasimamia walio chini yake,” alisema Machali.

“Rais tunaweza kumuacha, lakini Pinda ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali. Kama wapo mawaziri wameboronga ni wazi na yeye anaingia moja kwa moja katika hilo kapu,” alisema na kuongeza:

“Kama kweli tunataka taifa lisonge mbele kutoka hapa tulipo ni lazima tumuondoe Pinda…….. amekuwa mpole mno, mzito kufanya uamuzi na analea matatizo.”

Hata hivyo, alisema wabunge waliosaini fomu hiyo, wote wanatoka kambi ya upinzani na kusema wabunge wengi wa CCM aliowafuata kuwaomba watie saini wanaogopa au wanasita kufanya hivyo.

“Nataka niwaambie wabunge wa CCM hebu tusimame katika masilahi ya umma… Serikali inapofanya vibaya wanaoumia ni wananchi wetu bila kujali ni mwanachama wa chama gani,” alisema.

Pinda tayari amesema wazi kwamba yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake iwapo Rais Kikwete ataamua kumuondoa na kwamba hata Rais asipochukua hatua hiyo ni ruksa kwa wabunge kutumia mamlaka yao ya kikatiba ya kumuondoa kwa njia ya kura ya kutokuwa na imani naye.

Wabunge wengine
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola ambaye alikuwa mwiba kwa Pinda bungeni alisema: “Haya ni mambo ya ajabu sana, tutaendelea kubadilisha glasi lakini mvinyo ni uleule”.
Alisema uwajibikaji wa Serikali unaanzia kwa Waziri Mkuu na kusema anamuomba Rais atafakari ombi lake la kumfuta kazi Pinda.

“Tufike mahali tuambiane ukweli bila kumung’unya maneno kama kweli tunataka kuisaidia nchi yetu na Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi ambayo inapendwa na kuaminiwa na Watanzania,” alisema Lugola.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa  alisema anavyomuona Pinda na kutafsiri utendaji wake, anadhani kuwa viatu vya uwaziri mkuu vinampwaya.

“Haiwezekani mara mbili ndani ya Bunge mawaziri wang’oke halafu wewe ubaki… wanapoboronga katika utendaji wao lazima pia umguse kiranja wao (Pinda) na hili bado tutalia nalo,” alisema Msigwa na kuongeza:

“Tulitarajia Waziri Mkuu awe wa kwanza kutafakari na kujipima kama kweli anastahili kubaki hasa baada ya madudu yale ambayo yameichafua Serikali mbele ya umma.”
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisema wakati umefika kwa Waziri Mkuu, Pinda kukaa pembeni na kumwachia Rais Kikwete aunde safu nyingine.

“Pinda ni mtu wangu. Tunaheshimiana na sina chuki naye. Kwanza yeye ni mmoja wa watu ninaotuhumiwa kuwapa jimbo apite bila kupingwa na kuniletea matatizo kwenye chama changu.

“Hivyo sina chuki naye maana pia anatoka kanda yetu. Hata hivyo, hali ya sasa ya nchi inahitaji kupumua. Ampe nafasi Rais aunde Serikali upya.”

Alisema kuna tatizo kubwa la uongozi ndani ya nchi na kuwa mambo hayaendi licha ya juhudi mbalimbali pamoja na Bajeti ya Serikali kuongezeka kila kukicha.

“Huduma hazifiki kwa wananchi. Serikali ni kama haipo, nchi imevimba na inahitaji kupumua. Mwaka 1990 Rais Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi,) alikumbwa na hali kama hii na Warioba alijiuzulu ili kumpa nafasi kuunda upya Serikali. Alimrudisha Warioba lakini mawaziri wengi waliondoka,” alisema Zitto.

Aprili mwaka jana katika mazingira yanayofanana na ya mkutano wa 14 wa Bunge uliomalizika Jumamosi, wabunge 74 wakiwamo wa CCM walitia saini fomu ya kutaka kumng’oa Pinda.

Hata hivyo, aliepuka zahama hiyo, baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri mwezi mmoja baadaye na kuwaondoa mawaziri sita na manaibu waziri wawili waliokuwa wakishinikizwa kuachia ngazi.

Mawaziri hao walikuwa William Ngeleja (Nishati na Madini), Mustafa Mkulo (Fedha), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Omar Nungu (Mawasiliano), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara) Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii). Manaibu walikuwa Dk Athuman Mfutakamba (Uchukuzi) na Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii).

Posted By Unknown09:11

LOWASA AKANA KUWA RAIS

Filled under:



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa amewataka waendesha bodaboda na watu wengine wasimwite Rais kwa sababu wanamtengenezea chuki na uhusiano mbaya na watu.

“Mbona mnataka kuniletea uchuro! Mnanitengenezea ugomvi na watu jamani…,” alisema wakati akizindua Shirikisho la Bodaboda Tanzania jana kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.

Lowassa amekuwa akitajwa kuwania urais katika uchaguzi ujao wa Rais na wabunge utakofanyika 2015. Hatua hiyo imekuja baada ya Lowassa kuwaeleza kuwa atafanya harambee ya kuchangisha fedha ili kila aliyeingia kwenye shirikisho la waendesha bodaboda aweze kupata pikipiki yake.

Baada ya kauli hiyo waendesha bodaboda hao walipaza sauti zao wakiimba rais,rais …..wa mwaka 2015 huku wakidai amepita hana mshindani. Aliwataka kuacha  kumwita rais kwa sababu wanamtengenezea ugomvi na watu.

Alisema asilimia 50 ya madereva wanaoendesha  bodaboda hizo siyo pikipiki zao hivyo kutokana na hilo atafanya harambee ili kila mmoja kumiliki  pikipiki yake ili waweze kujiajiri wenyewe.

“Tumeona kuna tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini hivyo nimeona kwenye shirikisho hili asilimia 50 siyo za kwenu.  

Nimekusudia kuanzisha  harambee ya madereva ambao hawana pikipiki ili nao  wawe nazo waweze kujiajiri,” alisema Lowasa.

Lowasa aliitaka Kamati ya Shirikisho la Bodaboda kukutana naye Januari 15 mwaka 2014 ili kupanga harambee hiyo ifanyike lini na wapi.

Alisema matajiri nchini wapo wengi nitawafuata na kuwachangisha harambee wakiwemo Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi na mfanyabiashara maarufu Said Salum Bakhresa.

Posted By Unknown08:47

Tuesday 17 December 2013

MANGARIBA NA WAZAZI WA WATOTO WALIOKEKETWA WAKAMATWA KILIMANJARO

Filled under:



Kamishna wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,) amesema kuwa watu 38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa wasichana waliokuwa wanakeketwa.

Alisema kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.

Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata wanawake 38 mnamo siku ya Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.


Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.


Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida kutokea mjini Moshi.


Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.


Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.


Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.

Posted By Unknown10:13

LEMA AIKALI KIDEDEA KAMATI YA BUNGE KUTOKANA NA KUTOZUNGUMZIA SUALA LA BOMU KWENYE MKUTANO CHADEMA

Filled under:



Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ameeleza kushangazwa na hatua ya kamati ya Bunge kukwepa kuzungumzia suala la kurushwa bomu kwenye mkutano wa chama chake huko Arusha, Julai 15, mwaka huu.

Akichangia mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ulinzi na ya Mambo ya Nje, bungeni jana, Lema alisema kamati hizo ziligusia suala la bomu lililorushwa kwenye Kanisa Katoliki Olasiti, Arusha na kuachana kuzungumzia lile la mkutano wa Chadema uliofanyika kwenye Viwanja vya Soweto.

Alisisitiza msimamo wa Chadema kuwa kinao mkanda wa video unaoonyesha mtu aliyelipua bomu Uwanja wa Soweto na kushangaa taarifa ya kamati hizo mbili kutokuzungumzia tukio hilo.
Alisema ushahidi huo ungewezesha vyombo vya ulinzi na usalama kumbaini mtu aliyerusha bomu hilo na kusisitiza kuwa wako tayari kukabidhi mkanda huo kwa tume huru itakayoundwa na Serikali kuchunguza tukio hilo.

Lakini bahati mbaya alikamatwa jambazi kule Nzega akapigwa ili anitaje mimi ndiye niliyerusha bomu Olasiti na nilipigiwa simu na mmoja wa ndugu wa jambazi huyo akaniambia kuhusu suala hilo... Tunao ushahidi nani alitaka kutuua, Serikali iunde tume tupeleke ushahidi wetu,” alisema.

Bomu katika uwanja huo lililipuka wakati Chadema kikihitimisha kampeni zake za udiwani katika Kata ya Kaloleni.
Mei 5, mwaka huu, watu wasiojulikana walirusha bomu katika mkusanyiko wa kidini katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kusababisha vifo vya watu watatu.

Posted By Unknown06:15

AMATUSI LIYUMBA ASAKAMWA NA KESI YA KUKUTWA NA SIMU GEREZANI

Filled under:



Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na simu gerezani, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imfutie shtaka hilo na kumuachia huru kwa madai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kumkomoa.

Liyumba aliyaeleza hayo jana wakati akijitete mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando anayetarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, Januari 15, mwaka na kuzitaka pande zote mbili kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho kama mshtakiwa ana hatia ama la, Desemba 30, mwaka huu .

“Kesi hii imepangwa kwa ajili ya kunikomoa, wakati natumikia kifungo sijawahi kuvunja sheria, kupewa adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote, simu yenye namba 0653004662 siijui nimeiona hapa na kama imesajiliwa ni lazima mhusika atajulikana.” alieleza Liyumba.

Alidai kuwa, Julai 2011 alikuwa mfungwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na unapofikishwa huko ni lazima upekuliwe mara tatu kwa kuvuliwa nguo zote.

Kutokana na utaratibu wa ulinzi gerezani, siyo rahisi kwa mfungwa ama mahabusu kuingia na simu

Julai 27, 2011 mchana nikiwa kwenye selo yangu na mtu mmoja ambaye ni mahabusu, tukisoma magazeti ghafla askari wawili akiwamo shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, waliingia na kuniambia kuwa hii simu umeipataje wakati wakiwa wameishika mkononi.

Aliongeza kuwa tukio hilo kwake lilikuwa ni mshtuko na aliona ni kitu kilichopangwa na kwamba, wakati huo ilikuwa bado mwezi mmoja na nusu amalize kutumikia kifungo chake.

“Naamini walikuwa wananingojea, nilitafakari mlolongo wa matukio yanayonikuta, nilishtakiwa kwa kuambiwa nimesababisha harasa ya Sh261 bilioni shtaka ambalo liliondolewa na kupewa la kutumia madaraka vibaya, madaraka ambayo sina wala sijapewa huu ni uonevu.” alisema Liyumba.

Alibainisha kuwa wakati akiwa gerezani muda mfupi kabla ya kutoka watu wa Takukuru walimfuata na wakitaka kuandaa kesi dhidi yake, lakini aliwapinga kwa madai ya kutaka kuwasiliana na mwanasheria wake.

Alidai kuwa watu hao walimfuata tena na kwamba baada ya dulu hilo, akaona tukio hili la Julai 27,2011 la kubambikiwa kesi ya kukutwa na simu gerezani.

Alisisitiza kuwa simu na namba ya 0653004662 haifahamu, kama imesajiliwa mhusika atajulikana na iwapo atakuja mtaalamu ataeleza angalau ilipigwa kwa nani.

Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ya mkononi akiwa gerezani Ukonga, Dar es Salaam, wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili.

Posted By Unknown06:01

SANAMU YA NELSON MANDELA YAZINDULIWA

Filled under:

Rais Jacob Zuma amezindua sanamu ya shaba ya shujaa wa Afrika, Nelson Mandela kwenye jengo la Muungano lililopo mji wa Pretoria.

Sanamu hiyo yenye urefu wa mita tisa humuonyesha Mandela akitabasamu, huku akiwa ameonyesha ishara ya kukumbatia.

Wakati akizindua sanamu hiyo jana, Rais Zuma alisema kwamba sanamu nyingi za Mandela zinamuonyesha akinyoosha mkono wake mmoja juu kama ishara ya mapambano iliyokuwa ikitumiwa na Chama cha ANC.

Lakini, ishara ya kukumbatia iliyokuwa ikitumika katika sanamu hii ni tofauti, kwasababu inamuonyesha Madiba akikumbatia nchi nzima na watu wake wote bila kujali rangi, itikadi wala tabaka. Zuma aliizindua sanamu hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi ya kiongozi huyo yaliyoshuhudiwa na umati mkubwa watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa nchi tofauti yaliyofanyika katika Kijiji cha Qunu.

Katika uzinduzi huo alikuwapo Waziri wa Utamaduni, Paul Mashatile na familia ya Madiba ambapo Zuma alikuwa na mkewe, Thobeka Madiba Zuma.

Pia, alikuwapo Makamu wa Rais, Kgalema Motlanthe na viongozi wengine nchini humo wakishuhudia kuzinduliwa kwa sanamu hiyo ya historia.

Uzinduzi huo uliofanyika katika jengo hilo, pia ulishuhudiwa na waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali.
Mandela alizikwa juzi katika kijiji ambacho alizaliwa cha Qunu, mazishi yake yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwamo viongozi mbalimbali duniani.

Posted By Unknown05:46

Sunday 15 December 2013

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA AUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

Filled under:

 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza CLEMENT MABINA ameuawa na wananchi wenye hasira kali muda mfupi uliopita katika mgogoro wa ardhi nje kidogo ya jiji la mwanza eneo la kisesa.


Inadaiwa kuwa kulikuwa na kesi mahakamani kuhusiana na eneo hilo lakini kinyume chake Mabina alifikaeneo hilo   leo na kuanza kupanda miti,wananchi walifika eneo hilo na kuanza kumuuliza kulikoni? ndipo alipoanza kurusha risasi hewani na kumjeruhi mwananchi mmoja baada ya risasi hizo kuisha ndipo wananchi walimvamia nakuanza kumpiga na mawe mpaka mauti yakamfika.

Posted By Unknown04:42

ONLINE DISTANCE LEARNING SCHOLARSHIPS, 2014

Filled under:



Online distance learning enables various students to get quality education with their busy schedule from anywhere. Today various students are accessing massive online courses of various international universities. Some students also apply for online education as they cannot afford for the conventional courses. Many universities and institutes are offering scholarship programmes for those students to continue their studies in a distance mode. Here is the list of various institutes and organizations offering online distance learning scholarships for national and international students. Have a look below to avail the scholarships for online distance learning and bring the desired education at your door.



Edinburgh Global Online Distance Learning Master’s Scholarships in UK, 2014
University of Edinburgh is offering 6 masters scholarships for eligible distance learning master’s programmes in the field of Science, Engineering and Medicine & veterinary. Each scholarship will have a total value of £5,000 which will be deducted from the tuition fee for the entire part-time programme of study. A selection committee will meet in June 2014 to select the scholarship holders. The winners of the scholarships will be announced in July 2014. The application deadline is 30 May 2014.
2014 Edinburgh Global Health Academy Distance Learning Master’s Scholarships in UK
The University of Edinburgh will offer 4 Master’s scholarships for eligible distance learning Master’s programmes offered by the University. This scholarship is being offered in various areas related to health. Scholarship will be awarded to students who are accepted for admission onto an eligible Global Health Academy programme at the University of Edinburgh. The application deadline is 30th May 2014.
Open Society Presidential Fellowship in USA, 2014
Open Society Foundation is offering one year residence fellowship for recent JD, LLM, MPA, MPP and MBA graduates from accredited U.S. law, public policy and business schools. Fellows pursue work related to human rights, good governance and justice through a one-year residence within the Office of the President at the Open Society Foundations. Fellows will receive a salary of $60,000 plus benefits. Finalists will be notified in January 2014 and interviews will be conducted in February 2014. The MBA, MPP and MPA graduate materials are due on January 3, 2014.
The Distance Learner Online MPH Scholarship for International Students, 2014
Online MPHDegree.net is offering two online MPH scholarships for international students in USA. The purpose of the merit-based Distance Learner Online MPH Scholarship is to help public health students pay for the costs of their education. It may be awarded to anyone who is currently enrolled or will enroll in the next six months in a graduate level, online master of public health program. Total offer is of  $1000. 00. These are merit-based scholarships to deserving online MPH candidates for each calendar year. The application deadline is January 15th, 2014.

Distance Education and off Campus Scholarship in USA, 2014
Southern Illinois University is offering scholarships for distant learner in any course. Applicant needs to write two paragraph essay on “Outlining your financial need and how your SIU education will help you accomplish your career goals”. The programme is offering two $250 scholarships at each SIU off-campus locations. The application deadline is 31st January, 2014.
Blackhawks Breakaway Scholarships at University of Phoenix, 2014
University of Phoenix is offering number of institutional scholarships to help those candidates who want to pursue their higher education via online service. Through this scholarship program, two (2) full-tuition scholarships will be offered. Each scholarship will allow a prospective student the opportunity to complete an undergraduate or master’s degree program at University of Phoenix. Only the first 200 eligible applications will be considered. The application deadline is 14th January, 2014.

Focus to the Finish Scholarship at University of Phoenix, 2014
University of Phoenix has created the Focus to the Finish Scholarship for those candidates who want to complete their course. It is offering 16 full-tuition scholarships to deserving students. Each scholarship will allow a prospective student the opportunity to complete an undergraduate or master’s degree at University of Phoenix. The application deadline is 8th January, 2014.
Scholarships for Prospective Students at Uppsala University, 2014
Uppsala University is offering several scholarships for fee-paying students applying for Master’s programmes commencing in the autumn of 2014. These scholarships cover the total cost of tuition fees for all courses within the programme, i.e. 30 credits per semester. The application deadline for scholarships is 15th January 2014.
Abbott & Fenner Scholarships at Johns Hopkins University, 2014
Abbott & Fenner are committed to continuing their efforts at helping those who have the desire and ambition to succeed. This Scholarship is available for all high school juniors and seniors as well as all students who are currently registered in any accredited post secondary institution. The award is of $1,000. The application deadline is 14th June, 2014.

Scholarships for Distant Learning MBA at University of Bradford, 2014
University of Bradford offers a number of specific awards and scholarships to help students in funding their tuition fees. University is offering 20 Accelerated MBA Merit awards, worth up to £11,225. This award is only available for January 2014 entry. It is not transferable to other programmes. The applications are open for January, 2014 entry.
Wishing you success.
Scholarship Tags: , , , , ,

Posted By Unknown03:54

MBOWE KUNENA MACHACHE NA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MWANZA

Filled under:

Katika kuzindua Mkoa wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Mwanza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza mambo mazito ambayo yanaweza kutafsiriwa kama somo kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, vijana na wanachama wa chadema kwa ujumla wake. Akihutubia mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika kiwanja kilichopo ofisi za Kanda ya Ziwa Magharibi eneo la Bwiru, mwenyekiti huyo wa CHADEMA ambaye pia ni mbunge wa Hai aliongea mambo kadhaa yaliyokuwa chini ya kichwa cha habari Historia ya CHADEMA.

CHADEMA imejengwa na watu kwa maumivu makubwa. Ndugu mbowe alitanabaisha kwamba kuna watu wamemwaga damu zao, kuna watu wamekuwa vilema,kuna watu wamefilisiwa na kuna watu wengine wamepoteza uhai wao kwa sababu ya kuanzisha na kukijenga chama cha CHADEMA. Katika kulifafanua hilo aliwachallenge vijana wa vyuo vikuu kama wanafahamu hata majina ya watu waliopoteza uhai wao au kuvurugiwa maisha yao kwa sababu ya CHADEMA. Akitoa mifano ya watu hao Mbowe alimtaja aliyekuwa balozi maalumu wa Tanzania UN ndugu Antoni Nyaki alivyovuliwa mara moja nafasi yake awamu ya mwinyi kwa kosa moja tu la kuwa mwenyeji wa Edwin Mtei alipokwenda Marekani katika harakati za kum-recruit Kabouru aliyekuwa huko Marekani kwa wakati huo. Pia Mbowe alimtaja ndugu Costa Shinganya kama victim aliyefilisiwa na kuamua kukimbilia Kongo kwa kosa la kusimama upande wa CHADEMA. Mifano mingine aliyotaja ni wafuasi wa CHADEMA kuuwawa katika maandamano, na mikutano kwa kurushiwa mabomu ya kivita kwa mfano pale Arusha.

Kuhusu elimu yake Mbowe ameeleza namna alivyofika Form 6 na kukwama kuendelea kutokana na mfumo wa elimu na ajira kwa wakati huo. Anasema alivyomaliza kidato cha sita alikwenda kufanya kazi BOT kabla ya kwenda chuo kwani kwa wakati huo mtu asingeweza kwenda chuo moja kwa moja bila kufanya kazi kwanza. Baada ya miaka mitano alipoomba kwenda chuo Governor wa BOT wa wakati huo Bob Makani marehemu hakumpa ruhusa ndipo alipoamua kuacha kazi na rasmi kuanza kujihusisha na mambo mengine ikiwemo siasa.

Historia ya CHADEMA, chama kilianza rasmi miaka ya tisini kipindi cha vuguvugu la uanzishwaji wa demokrasia ya vyama vingi.Ilipofika mwaka 1991 yeye na waasisi wengine 7 na baadae wakawa 14 wakaanzisha rasmi chama cha CHADEMA mkoani Dar-es-salaam kabla ya kukipeleka chama mikoani na visiwani Zanzibar. Akitaja majina ya waasisi wa CHADEMA,Mbowe alimtaja Edwin Mtei (mwenyekiti),Bob Makani (katibu mkuu), Costa Shinganya, Brown Ngwilupi, Edward Barongo(mwenezi), Mary Kabigi (kiongozi wanawake), Freeman Mbowe (Vijana), mama Marios (mwenyekiti wa kwanza Morogoro) Ndesamburo na wengine. Pia alidokeza kwamba mpaka uchaguzi wa mwaka 2000, CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea wa uraisi.

Chanzo cha yeye kuwa mwenyekiti wa CHADEMA. Mbowe pia alisema kwa kipindi cha miaka ya 2000 hakuwa na wazo la kuwa mwenyekiti wala kugombea uraisi bali ni msukumo wa viongozi wa juu wa chama na vijana ndio uliochangia yeye kugombea nafasi hizo. Na yeye kwa kuheshimu hao viongozi aliafiki kuwa mwenyekiti lakini kwa masharti ya kupewa Dr. Slaa awe katibu mkuu wake na aruhusiwe kuanzisha reforms mbalimbali mdani ya chama, na huo ndio uliokuwa mwanzo wa uenyekiti wake.Akifafanua kwanini wenyeviti 2 wa mwanzo walijitoa mara baada ya awamu zao za kwanza tuu kuisha alibainisha kwamba umri wa wazee hao pia ulichangia.Alisema wote, Mtei na Bomani walianza uenyekiti wao wakiwa na miaka 60+ kwahiyo ilikuwa ni natural kwa wao kujitoa kwenye cheo hicho pengine kwa kuona wapumzike.

Onyo kuhusu "demokrasia". Mbowe pia alionyesha changamoto inayoweza kuletwa na dhana ya demokrasia kama busara haitatumika. Akitoa sababu za chama chake kutoweka wagombea uraisi hususani kwa mwaka 1995, Mbowe alisema kwanza ndugu mtei alichukua fomu ya kugombea uraisi, lakini siku chache kabla ya zoezi la kuchukua fomu halijasitishwa,kwa mshtuko, mzee Makani marehemu nae akachukua fomu hali iliyoleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama ukizingatia chama kilikuwa bado ni kichanga mno. Waliposhauriwa mmoja amwaachie mwingine,wote walikataa na hatimae kamati kuu ikaamua kuwaondoa wote na kutoweka mgombea katika kiti cha uraisi ili kukinusuru chama.Chanzo kikubwa kilikuwa ni demokrasia,kwamba kila mtu ana haki ya kugombea nafasi za uongozi chamani.

Pia alifafanua umuhimu wa kufanya kazi ndani ya chama kama timu akitolea mfano wa Lionel Messi wa Barcelona namna alivyo tofauti na Lionel Messi wa Argentina sababu tu ya 'team work' na ugumu wa kucheza pekee yako kwenye ulingo wa siasa. 

Mbowe na CHADEMA.Anasema akijua, na wanachama wenzake wakijua kwamba CHADEMA hawawezi kushinda mbio za uraisi mwaka 2005 wote hawakutaka kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huo.Hali hiyo pia ilichagizwa na mvuto wa kisiasa aliokuwa nao mgombea wa CCM kwa wakati huo, yaani Jk. Pamoja na hayo yote chama kilitambua umuhimu wa kumsimamisha mgombea wa uraisi ili kukifanya kiwe maarufu zaidi na kisikimbiwe na wanachama.Yeye akiwa hana mpango wa kugombea, na hakutaka kabisa, kamati ya vijana CHADEMA wakiwemo akina Mnyika,Mdee,Kigaila na Zito na viongozi wa ngazi za juu wa chama walimshindikiza agombee nafasi ya uraisi vinginevyo wangejivua nafasi zao chamani.Hapo ndipo alipoamua kujituma ndani kinyang'anyiro hicho cha uraisi alichoambulia nafasi ya tatu nyuma ya Lipumba na Kikwete.Pia katika uchaguzi huo alikuwa na mawakala 4000 tu kati 40000 walioitajika kwahiyo huwezi kuondoa uwezekano wa kuibiwa kura. Katika uchaguzi huo ndugu Mbowe ameeleza kwamba alitumia rasilimali fedha na rasilimali vitu vya kwake binafsi.

Ubunifu ndani ya chama. "Nilitafakari sana,nivae nini katika kampeni zangu ili nionekane tofauti na wagombea wengine,nikaenda Marekani, nikapita madukani na nikaona gwanda nikasema nitavaa hizi nguo,kipindi hicho hata wazee wa CHADEMA walikuwa hawataki kuvaa kabisa gwanda''. Pamoja na hilo, pia Mbowe anadokeza namna alivyoanzisha matumizi ya Helkopta katika kampeni zake,na anasema pamoja na kujua hatashinda lakini alitumia mbinu zote hizo ili CHADEMA iingie kwenye mioyo ya Watanzania.

Uhuru wa kugombea nafasi yoyote katika chama.Mbowe amesema kila mwanachama ana haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama ikiwamo uenyekiti lakini kwa mbinu za kistaarabu.Akimtolea mfano Wenye,amesema unaweza kugombea nafasi ya kuwa mbunge wa CHADEMA kwenye jimbo lake lakini endapo utatumia kashfa,matusi na mbinu chafu kumchafua chama hakitakuvumilia.Pamoja na hilo alitoa onyo kwa mfano wa namna mtu mnayesafiri naye katika ziwa victoria ndani ya boti na aanze kubomoa na kuvunja mbao za boti alafu atazamwe tuu, huo utakuwa ni wendawazimu. ''Kama sasa hivi hatupo madarakani tunagombea madaraka, jee tukiingia madarakani?huu ni uchizi'' mbowe alihoji.Kwa wale wanaopima maji,amewambia wapime tuu ili waone, lakini wakiumia wasimlaumu mtu. Akaonya pia CHADEMA ni taasisi kubwa kuliko mtu yoyote.

Dhana ya udini na ukabila.(Kwa mtazamoa wangu)Akijibu hoja za uanzishwaji wa CHADEMA kwa misingi ya udini na ukabila Mbowe alitaja waasisi wa CHADEMA kwa majina na mikoa wanayotokea. Alimtaja marehemu Bob Makani kama mmoja wa waasisi wa CHADEMA, msukuma pia muisilamu. Wengine ni Brown Ngwilulupi kutoka Mbeya,Mama Mary Kabigi Mbeya (Kiongozi wa wanawake), mwenezi Edward Barongo Kagera, Shaibu...Katibu mkuu awmu ya pili n.k.

Katika kuhitimisha mwenyekiti huyo alisema, mwaka ujao utakuwa ni wakuwavuta akina mama wengi kadiri iwezekanavyo na kazi hiyo itafanywa na wanaume wa chama na wanawake waliopo ili kuondoa lawama za mambo ya viti maalumu.Lengo kubwa ni kuondoa taswira ya chama kuonekana ni cha wanaume zaidi kuliko cha jinsia zote.

MWISHO:Kesho ndugu Mbowe atakuwa katika viwanja vya shule ya msingi vya Shekilango karibu na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino ambapo anatazamiwa kuongea na wanafunzi wa chuo hicho,wakazi wa maeneo jirani na wananchi wa Mwanza kiujumla.

Posted By Unknown03:20

KAULI YA PINDA HAINA MASHIKO

Filled under:



Baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wamemkosoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kutamani kung’olewa kwenye nafasi, wakidai kuwa kauli yake inaonyesha jinsi alivyo mpole na dhaifu kiutendaji .

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba ayezungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu alisema kuwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda imeonyesha kwamba ana tatizo la kutokujiamini.

“Kazi za Waziri Mkuu zinajulikana wazi kwamba ni majukumu mazito ikiwemo kusimamia utendaji wa Serikali kwa kila wizara, hivyo kusema asihukumiwe kwa sababu ya wizara chache zisizofanya vizuri, inaonyesha ameshindwa majukumu yake. Alichotakiwa kufanya kwa wizara hizo ni kumshauri Rais awaondoe madarakani wasiowajibika,” alisema.

Alisisitiza: “ Hatutegemei kumwona Waziri Mkuu akiingia kufanya kazi kwenye kila wizara, isipokuwa anatakiwa kumshauri Rais ili mambo yaende sawa.”

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema kuwa amekuwa akifuatilia kauli za Waziri Mkuu Pinda hata anapokuwa kwenye ziara za kikazi, ambapo amekuwa akitoa kauli za kuwabembeleza watendaji, hata wanapoboronga.

“Waziri Pinda ni mpole, amepatikana kutokana na mfumo mbaya wa upatikanaji wa mawaziri uliopo nchini. Kwa wenzetu, waziri mkuu huchaguliwa mtu aliye jasiri, anayeweza kuongoza nchi kwa kusimamia shughuli mbalimbali Rais ananapokuwa nje ya nchi,”alisema na kuongeza:

“Waziri Mkuu akiwa dhaifu ni tatizo, hatujawahi kuwa na waziri mkuu mzuri tangu alipokufa Moringe Sokoine mwaka 1984, yeye alikuwa tofauti. Huu ni wakati mzuri wa kuweka hata kwenye marekebisho ya Katiba, kiwepo kipengele cha sifa za mawaziri, kwa sababu, wapo wengine unashangaa hata kigezo kilichotumika kumpa nafasi hiyo lakini ukifuatilia ni urafiki.”

Naye Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema anaona alichozungumza Waziri Mkuu Pinda ni sawa kwa kuwa angeweza kutangaza kujiuzulu, lakini ametoa nafasi kwamba kama Rais atamwondoa au wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani naye atashukuru.

Juzi, akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma, Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa yupo tayari kuachia ngazi endapo tu Rais Jakaya Kikwete ataamua kumwondoa na kama itatokea hivyo, atamshukuru Rais kwa kumwambia, ahsante.

Pinda aliliambia Bunge kwamba endapo Rais hatafanya hivyo, bado wabunge wanayo mamlaka ya kikatiba ya kumwondoa kwa njia ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kasim Ahmed (CUF) katika utaratibu wa Bunge wa Waziri Mkuu kujibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.

Katika swali lake, Mbunge huyo alisema; Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikaririwa akiwa jijini Mbeya kuwa wapo mawaziri mzigo katika Baraza la Mawaziri.

Katika swali lake la nyongeza, Rukia alisema wakati wanachangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa, yupo Mbunge wa CCM alisema kuwa Pinda ni mzigo namba moja.

“Kuna mbunge, tena wa CCM, alinukuu kauli ya Katibu Mkuu wa CCM na akasema kama ni mawaziri mzigo basi mzigo nambari moja ni wewe Waziri Mkuu, unawaambiaje Watanzania?” aliuliza Rukia.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema yeye anasimamia wizara 20, hivyo kama wapo watakaomhukumu kwa wizara moja ama mbili kwa kutofanya vizuri basi watu hao watakuwa hawamtendei haki

Posted By Unknown02:49

Friday 13 December 2013

LUKUVI AJA NA SHERIA MPYA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Filled under:




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amesema sheria mpya dhidi ya dawa za kulevya ambayo Serikali inatarajia kuifikisha bungeni mwakani, itahamasisha watumiaji/wafanyabiashara wadogo wa dawa za kulevya kuwataja wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo.
Aidha alisema sheria hiyo inatarajiwa kuanzisha kitengo maalum cha mahakama ambacho kitakuwa na kazi ya kusikiliza kesi zinazohusu dawa za kulevya ili kuharakisha usikilizaji wake.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari bungeni juzi kuhusu taarifa aliyoiwasilisha bungeni ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2012.

“Wafanyabiashara hawa wakubwa wa dawa za kulevya ni lazima wafichuliwe, ni hatari lakini lazima wafichuliwe,” alisema na kuongeza, “tunategemea zaidi ushirikiano wa wananchi kufanikisha azma hiyo.

Akizungumzia taarifa hiyo, Lukuvi alisema tatizo la dawa za kulevya limeendelea kuwapo nchini ambako ukamataji wa kiasi kikubwa cha heroine kwa mkupuo umeendelea.

Alisema kwa Januari mwaka jana, mkoani Lindi walishuhudia kukamatwa kwa kilo 211 za heroine ambacho ni kiasi kikubwa kabisa cha dawa hiyo kuwahi kukamatwa hapa nchini kwa mkupuo.

Alisema tukio hilo pamoja na mengine yanaashiria kuwa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya huingizwa nchini kupitia vipenyo mbalimbali vikiwamo vilivyo kwenye ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,400.

Posted By Unknown10:53

ZITTO AMTAKA WAZIRI ANAYEHUSIKA NA KUSIMAMIA( NEC) ACHUKULIWE HATUA KUTOKANA NA RUSHWA

Filled under:



Wakati Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akitaka waziri anayehusika na kusimamia Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) achukuliwe hatua kutokana na zabuni yenye harufu ya rushwa, imebainika kuwa hukumu iliyotolewa na Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), imesema kampuni iliyoshinda zabuni hiyo ilishiriki kuandaa nyaraka za zabuni.

Hukumu hiyo, ni ile inayohusu kampuni ya zabuni za kuandaa vifaa vya uchaguzi vya kielektroniki, ambayo Nec iliipa kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation na M/S Invu IT Solution, tenda hiyo iliyokuwa na thamani ya Sh126 bilioni.

Hukumu hiyo ya PPAA imefikiwa baada ya kampuni za M/S Morpho na M/S IRIS Corporation Technology kukata rufaa kupinga uamuzi wa NEC.

Akizungumza bungeni jana, Zitto alisema kuwa kampuni iliyoshinda zabuni hiyo, gharama yake kwa kutoa huduma hiyo ilikuwa juu ilihali kuna kampuni nyingine zilizokuwa na bei ya chini pamoja na sifa za kufanya kazi hiyo.

Zitto alisema hayo wakati wa kuchangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala iliyowasilishwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Gosbert Blandess.

Akijibu hoja za zabuni hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Uratibu na Bunge) William Lukuvi alisema kuwa, PPAA ilibaini kuwa mchakato wa utoaji wa tenda hiyo ulikuwa na upungufu mkubwa na ndiyo maana ilibatilisha tenda hiyo na kuamuru mchakato wa kumpata mzabuni urudiwe.

“Hivi vifaa siyo vya kupigia kura, ni vya uandikishaji, mchakato wa kumpata mzabuni ndiyo uliobainika kuwa na tatizo, tume ya uchaguzi itachunguza kujua chanzo cha tatizo na ikibidi ichukue hatua,” alisema Lukuvi.

Mapema akitoa maelezo yake, Zitto alisema kuwa “Serikali itoe taarifa ndani ya Bunge, nini kilichotokea na ni moja ya pendekezo ambalo ninataka kamati ichukue ili wafanyie azimio ili waziri anayehusika na uchaguzi aje alitolee ufafanuzi nini kimetokea na hatua gani zimechukuliwa,” alisema Zitto.

Alisema wanafahamu mfumo huo uliowahi kutumika katika nchi za Malawi, Kenya na Ghana, umeleta matatizo kwenye nchi hizo.
Alitaka waziri anayehusika kuwajibika kwa kuleta taarifa bungeni ili wabunge waijadili na kuona nini kilichotokea.

Alisema ni vizuri katika mchakato wa jambo kama hilo, wadau wote ambao ni pamoja na vyama vya siasa washirikishwe katika hatua ya tathmini ili kuweza kujenga kuaminiana na kuleta mfumo mzuri.
Katika hatua nyingine, Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, ametaka majina ya watu walioficha fedha nje yatajwe.

Posted By Unknown10:08

PINDA ASEMA YUPO TAYARI KUACHIA NGAZI

Filled under:



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amevunja ukimya na kusema yuko tayari kuachia ngazi endapo tu Rais Jakaya Kikwete ataamua kumwondoa na kama itatokea hivyo, atamshukuru Rais kwa kumwambia, ahsante.

Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma jana kwamba endapo Rais hatafanya hivyo, bado wabunge wanayo mamlaka ya kikatiba ya kumwondoa kwa njia ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977

Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kasim Ahmed (CUF) katika utaratibu wa Bunge wa Waziri Mkuu kujibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.

Katika swali lake, Mbunge huyo alisema; Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikaririwa akiwa jijini Mbeya kuwa wapo mawaziri mzigo katika Baraza la Mawaziri.

Mbunge huyo alisema, katika ziara hiyo, Kinana alifuatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro.

“Walipokuwa Mbeya wakifuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM, Kinana alisema kuna baadhi ya mawaziri ni mzigo, wewe kama kiongozi mkuu wa shughuli za Serikali unachukuliaje kauli hii?” aliuliza.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema hata yeye ameyasikia hayo kwenye vyombo vya habari na kusema, kiutu uzima hawezi kutoa maoni yake kwa kuzingatia yale yanayosemwa kwenye magazeti.

“Sisi tunangoja arudi (Kinana) tukae naye ili tujue alichokuwa anasema hasa ni nini na ninaamini alikuwa na baadhi ya wizara kichwani kwake,” alisema Pinda bungeni jana.

Katika swali lake la nyongeza, Rukia alisema wakati wanachangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa, yupo Mbunge wa CCM alisema kuwa Pinda ni mzigo namba moja.

“Kuna mbunge, tena wa CCM, alinukuu kauli ya Katibu Mkuu wa CCM na akasema kama ni mawaziri mzigo basi mzigo nambari moja ni wewe Waziri Mkuu, unawaambiaje Watanzania?” aliuliza Rukia.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema yeye anasimamia wizara 20 hivyo kama wapo watakaomhukumu kwa wizara moja ama mbili kwa kutofanya vizuri basi watu hao watakuwa hawamtendei haki.

Posted By Unknown09:43