Saturday 15 February 2014

TUMIA UNGA WA DENGU,YAI,MANJANO KUIWEKA NGOZI YAKO NYORORO NA YENYE KUVUTIA

Filled under:



Ni ukweli usiopingika kuwa kila mmoja anahitaji kuonekana mrembo au mwenye mvuto mbele ya watu wengine. Ukweli huu huwafanya wengi kuhangaika kutafuta urembo na vipodozi vitakavyowapendezesha.
Tatizo linakuja ni aina gani ya vipodozi wanavyopaka watu, kwani wengi hukimbilia vipodozi vyenye kemikali vinavyosababisha kupotea kwa rangi asilia hata ugojwa wa saratani ya ngozi, ambayo mwisho wake husababisha kifo.
Wengi bado hawajapata uelewa kuwa urembo wa asili unaweza kutumiwa na watu wa rika zote kwa kuwa haudhuru ngozi na kutokusababisha magojwa ya ngozi.
Wapo wanawake wanaotumia vipodozi vya asili na ukiwaona sura zao huwa ni nzuri wakati wote na wanakuwa hawabadili uasili wa ngozi yao.
Kama ni mweupe utakuwa ni mweupe vilevile ila atakuwa anaufanya uwe na thamani kwani wakati wote atakuwa aking’ara na kupendeza.
Kama mweusi atabaki na rangi yake hiyo hiyo bali atakuwa ni mweusi wa kupendeza na kila wakati atatamanisha kwa sababu ya rangi yake ya asili.
Leo tutaangalia namna unga wa dengu unavyosaidia kupendezesha na kung’arisha sura yako hata ukaonekana mwenye mvuto mbele za watu.
Mahitaji
1.Unga wa dengu vijiko viwili vya chai
2.Yai moja la kienyeji
3.Mtindi mweupe
4.manjano kijiko kimoja
Namna ya kuandaa
Weka unga wa dengu katika kibakuli au chombo kisafi, kisha vunja yai pembeni na utoe kiini ambacho utakichanganya na unga vichanganye vyote kwa ujumla mpaka viwiane,
Koroga mpaka uhakikishe mchanganyiko huo umechanganyika na kulainika kabisa. Baada ya hapo safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha jikaushe kwa taulo au kitambaa kisafi.
Baada ya kuhakikisha uso wako uko safi paka mchanganyiko huo kwa kuusambaza uso mzima, ikiwezekana pia katika maeneo ya shingoni na pembezoni mwa masikio ili kuzifanya pia sehemu hizo kuwa zenye mvuto wa aina yake.

0 comments:

Post a Comment