Saturday 15 February 2014

JE WAJUA PARACHICHI NI TIBA YA CHUNUSI NA PIA HUIWEKA NGOZI YAKO IWE KAVU NA NYORORO

Filled under:


Parachichi ni tunda kama walivyozoea watu wengi,lakini linaweza kukuondolea tatizo la ngozi kukauka na kukuifanya iwe nyororo na ya kupendeza zaidi?
Kama bado ngoja leo nikujuze kuwa tunda hili ni moja kati ya matunda muhimu ambayo unaweza kuyatumia ukiwa nyumbani kutengeneza “homemade facial masks” kwa ajili ya uso

Wataalamu wa ngozi wanaeleza kuwa parachichi lina viini vinavoitwa ‘glutathione’ ambazo zina nguvu ya kukabiliana na ukavu katika ngozi yako.

Kwa mujibu wa mtandao unaofahamika kama www.dry-skin-guide.com, tunda hili lina uwezo wa kung’arisha sio pamoja na nywele zako.

Mtandao huo unaendelea kueleza kuwa tunda hili pia lina mafuta pamoja na vitamin B na E ambavyo ni virutubisho muhimu katika kuboresha ngozi iliyochoka na kavu.
 
Pia unabainisha kuwa tunda hili lina uwezo wa kupambana na bacteria na mikunjo katika ngozi yako na kurekebisha matatizo yanayochangia ukavu katika ngozi yako.
Mpaka hapo naweza kukwambia kwamba, katika suala la urembo si lazima kutumia vipodozi vya gharama ili kukidhi mahitaji ya ngozi yako. Kwa kifupi unaweza kujenga ngozi bora na yenye afya kwa kutumia matunda ambayo yanapatikana kirahisi katika mazingira yako.

Kama huwezi kuisusa ngozi yako kwa kuhofia gharama za kununua vipodozi na kama umejaribu vipodozi vya dukani bila ya mafanikio jaribu kutumia parachichi na utaona tofauti.

MAHITAJI Parachichi moja liloiva
 
JINSI YA KUTUMIA Osha ngozi yako kwa kutumia  na ikaushe kwa kitambaa safi kisha menya parachichi lako na lisage kisha lipake katika ngozi yako. Baada ya hapo acha lifanye kazi kwa muda wa dakika 15, kisha osha ngozi yako utaiona mabadliko ya ngozi yako kuwa laini na nyororo.
Waweza kutumia pia katika michirizi inayotokana na unene. Wataalamu wanaelezea kuwa matumizi ya tunda hili hayana.

Vipodozi vyenye kemikali mara nyingi husababisha kupotea kwa rangi yako asilia na vilevile husababisha ugojwa wa saratani ya ngozi ambayo mwisho wake husababisha kifo.

0 comments:

Post a Comment