Saturday 8 February 2014

JINSI YA KUTENGENEZA MASK ASILIA YA KAROTI NA ASALI ILI KUWEKA NGOZI NYORORO

Filled under:



Ngozi za watu hutofautiana,kuna wenye ngozi yenye mafuta,wengine ngozi kavu,wengine ngozi yenye unyevu nk
Maski ya Asali na karoti ni nzuri kwa aina yoyote ya ngozi.Inasaidio kuondoa mikunjo kwenye ngozi,na hufanya ngozi iwe laini na inayong’ara.
Karoti hujulikana kwa kuwa na vitamini A na C pia ina potasiamu na Asali ina sukari, Enzymes, madini, vitamini na amino asidi ,virutubisho hivi kwa pamoja vinaipa ngozi afya na muonekano mzuri.Natamani ningechambua umuhim na kazi ya kila kirutubisho nilichoainisha apo juu,lakini naogopa tukiingia huko tunaweza badili somo.
Tumia mask hii sio zaidi ya mara 2 kwa wiki,tafadhali zingatia hili.
Mahitaji
Karoti
Asali
Olive oil(mafuta ya maji ya olive)
Otomvu wa jani  la Aluvera
Kipimo cha karoti na asali ni sawa kwa sawa.yaani,mfano:i vikombe viwili asali,basi iwe vikombe viwili karoti.
Njia
1.kwangua karoti (shred) kisha zichemshe kwa mda mfupi sana ili zilainike na pia ili kufufua vitamin A iliyomo ndani ya karoti.usichemshe sana kwani utapoteza virutubisho vilivyomo ndani ya karoti(vitamin A na C).kisha ziponde adi zilainike.
2.Acha karoti zipoe  kabisa,kisha ongeza asali,changanya vizuri,kama mchanganyiko wako utakua mgumu au mzito sana ongeza maji ya baridi kidogo
3.Weka mchanganyiko wako frijini kwa mda wa dakika 10-15
4.Osha uso na shingo kwa maji ya vugu vugu kisha kausha na taulo. upake mchanganyiko kwenye uso wako vizuri na kaa nao kwa muda wa dakika 15-20 kisha ondoa mask hii kwa kuosha kwa maji ya uvuguvugu.
NOTE.waweza ongeza utomvu wa aluvera na olive oil ukipenda,kwa kipimo cha kikombe kimoja cha asali na karoti,tumia kijiko kimoja cha chakula cha olive oil na utomvu wa jani la aluvera.hii huongeza thamani ya maski yako kwa kuipa virutubisho zaidi.
Naamini utapenda matokeo ya maski hii kwenye ngozi yako.mimi imenitendea haki

0 comments:

Post a Comment