Friday 12 September 2014

OSCAR PISTORIUS ASUBIRI HUKUMU BAADA YA KUUA BILA KUKUSUDIA

Filled under:

 
OSCAR PISTORIUS
Jaji wa mahakama kuu ya Afrika Kusini Thokozile Masipa anaendelea hii leo kutoa hukumu yake dhidi ya kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa Olimpiki Oscar Pistorius huko Afrika Kusini.

Tayari amemuondolea makosa ya mauaji, na badala yake Pistorious anakabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia.

Katika uamuzi wake huo wa kumuondolea Mwanariadha Oscar Pistorius mashtaka ya mauaji ,jaji Thokozile Masipa alisema mwendesha mashtaka hakuthibitisha kesi yake pasi na shaka yoyote.
Hata hivyo itabainika vyema baadae leo iwapo atapatikana na hatia ya mauji pasi na kukusudia wakati jaji atapoitolea kesi hiyo hukumu yakini.

Pistorius amekana mashtaka ya kumua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp hapo mwaka jana katika siku ya wapendao Valentine day pale alipomfyatulia risasi kumuua.
Mwendesa mashtaka amekuwa akisisitiza kuwa Pistorius alimpiga risasi Reeva wakati wa ugomvi baina yao lakini Pistorius amekuwa akijitetea kuwa alidhani ni mwizi aliyevamia nyumba yake.

Jaji amesema wakati wa tukio hilo Pistorius alikosa makini kwa kutumia bunduki yake vibaya.

Mwandishi wetu wa Afrika kusini anasema uamuzi huu wa awali umewashangaza wengi waliokuwa wakifuatilia kesi hii kwa karibu wakisema inavyoelekea anaweza kupewa kifungo chepesi.

Anaepatikana na hatia la Kosa la kuuwa bila kukusudia hupewa kifungo kisichozidi miaka kumi na tano jela na pia kuna uwezekano wa kutumikia baadhi ya mda huo kifungo cha nje.
Hata hivyo mbali na uwezekano wa rufaa baada ya hukumu anakabiliwa pia na shtaka la matumizi mabaya ya bunduki

0 comments:

Post a Comment