Friday 28 February 2014

NYALANDU AFIKISHA ORODHA YA WATU 320 WANAOJIHUSISHA NA UJANGILI

Filled under:


PAMOJA na serikali kutotaja majina ya watu 40 ambao Rais Jakaya Kikwete alisema ndio mtandao wa ujangili nchini, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesisitiza kuwa orodha hiyo si ya kutengeneza na kwamba itawekwa hadharani muda wowote. 

Alisema kuwa wanayo majina zaidi ya 320 ya watu wanaojihusisha na ujangili na kuonya wahusika kuachana na biashara hiyo huku akitamba kuwa serikali ina mkono mrefu.

Waziri Nyalandu alitoa msimamo huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari wizarani kwake kueleza juhudi za serikali katika kukabiliana na ujangili nchini.

0 comments:

Post a Comment