Tuesday 11 February 2014

JINSI YA KUTUNZA NGOZI YENYE VINYWELEO

Filled under:



Kutawaliwa na vinyweleo vingi mikononi na miguuni ni hali ambayo huwakera watu wengi hasa wanawake, ambao huona kuwa ni kikwazo kwao kuonekana warembo.
Wapo waliojaribu kukabiliana na kero hiyo, kwa kutumia njia mbalimbali, hata wengine kuumia na kuiacha ngozi ya maeneo husika ikiwa na michubuko au kuharibika na kuwasababishia madhara.
Wengi hupendelea kuviondoa vinyweleo hivyo kwa kuvinyoa, lakini ili kupata matokeo bora, mambo mbalimbali yanatakiwa kufuatwa ili kufanikisha zoezi hilo na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri.
Jambo la kwanza; hakikisha unatumia mashine yenye wembe mpya ili kurahisisha unyoaji, kwani wembe butu utakufanya utumie nguvu nyingi kujinyoa, hatimaye kuumiza na kujeruhi ngozi.
Kabla hujaanza kuondoa vinyweleo, hakikisha unalowanisha eneo husika, miguu au mikono kwa muda usiopungua dakika mbili ukitumia maji ya baridi.
Unaweza kupaka krimu ya kunyolea au kulainisha ngozi, kisha anza kunyoa kwa kuipandisha mashine toka chini kwenda juu, ili kufanya vinyweleo vyote vitoke kwa urahisi na kuacha ngozi ikiwa laini bila makovu.
Tumia mkono kupapasa ili kukagua kwa umakini eneo ulilonyoa kujua kama umeondoa vinyweleo vyote. Ikiwa bado vipo, rudia hadi uhakikishe umevimaliza vyote.
Baada ya kumaliza, paka mafuta hususan ya maji ili kulainisha kabisa ngozi na kuondokana na mikwaruzo. Hiyo itatoa nafasi kwa matundu ya kupitisha hewa kwenye ngozi yako kufanya kazi yake vizuri.

0 comments:

Post a Comment