Tuesday 4 February 2014

ALIKIBA AAPA KUTOKUJA KUFANYA KOLABO NA DIAMOND PLATINUM

Filled under:



NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba, amesema haitakuja kutokea kufanya ‘kolabo’ na msanii wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ katika maisha yake.

Kauli hiyo ya Ali Kiba, imekuja baada ya mashabiki wa muziki huo, kumshauri afanye kazi na msanii huyo kwa kushirikiana na msanii mwenzao Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na kubashiri kwamba itakuwa kazi nzuri kutokana na vipaji walivyonavyo wakali hao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ali Kiba alisema amekuwa akipokea maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake, lakini hicho kitu hakiwezi kutokea kamwe.

“Kiukweli sifikirii na sidhani kama itakuja kutokea, kwani kufanya kazi na Diamond ni mfano wa kudeki bahari, haitakuja kutokea kamwe, naomba wapenzi wangu waangalie kazi nyingine nitakazotoa sio kusubiri kufanya kazi na msanii huyo, ni kama ndoto,” alisema.

Ali Kiba ni kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki huo, kutokana na kipaji chake cha kutunga mashairi ambayo yanavutia na kuliteka soko.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake kinachojulikana kwa jina la ‘Kujiinamia’ ambacho ameshirikiana na mdogo wake, Abdu Kiba.

0 comments:

Post a Comment