Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.
Inadaiwa Mandla, alimshambulia
mwalimu, Mlamli Ngudle na hata kumtisha kwa bunduki baada ya Mwalimu
huyo kuligonga gari la mmoja wa marafiki zake mwaka jana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari tarehe 24 baada ya kusikilizwa kwa muda katika mahakama ya Mthatha.
Mandla alirithi wadhifa wa babu yake kama kiongozi wa kitamaduni.
Mwendesha mkuu wa mashitaka aliwasilisha
mahakamani mashitaka mawili dhidi ya Mandla,la kwanza likiwa
kumshambulia mtu na pili kumtisha kwa silaha.
Bado hajasema ikiwa anakiri au kukanusha
mashitaka hayo lakini wakili wake aliitaka mahakama kuahirisha kesi
dhidi yake akisema kuwa alipokea mashitaka hayo leo tu na kuwa anahitaji
muda zaidi kuyatathmini.
Bwana Mandela ni kiongozi wa kijamii katika kijiji cha Mvezo,ambako babu yake alizaliwa.
Mandla amekuwa kwenye mvutano na shangazi yake Makaziwe kila mmoja akitaka kutambuliwa kama kiongozi wa familia ya Mandela.
Ni mjukuu wa kwanza wa Mandela wakati Makaziwe ni mtoto wa kwanza wa hayati mzee Mandel
0 comments:
Post a Comment