Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa uamuzi, dhidi pingamizi zilizowasilishwa na upande wa mlalamikiwa kwa njia ya maandishi dhidi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kinana anamtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema),
Mchungaji Peter Msigwa, kufuta matamshi ya kumkashifu, kumfedhehesha na
kumhusisha na ujangili wa meno ya tembo.
Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Zainabu
Muruke, baada ya Mchungaji Msigwa kupitia wakili wake, Peter Kibatala
kuwasilisha kwa njia ya maandishi, pingamizi lake dhidi ya mlalamikaji
ambapo anaiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kwa madai kuwa ina
upungufu kisheria.
Kwa mujibu wa Msigwa kupitia wakili wake Kibatala
wanadai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na Kinana dhidi yake, haina
mashiko kwa sababu ilikosewa jinsi ya kufunguliwa.
Walidai kuwa kesi hiyo ilikosewa namna
ilivyofunguliwa Ilipaswa kufunguliwa mkoani Mwanza ambapo tukio
linadaiwa kutokea ama mkoani Iringa kwenye makazi ya kudumu ya Mchungaji
Msigwa. Hivyo wanaiomba mahakama kuifuta kwa sababu ina upungufu wa
kisheria.
Kinana anaiomba mahakama iamuru Mchugaji Msigwa
amlipe kiasi cha Sh 350 milioni kutokana na matamshi ya Aprili 21, 2013,
yaliyotolewa katika mkutano wa hadhara.
0 comments:
Post a Comment