KUNA mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi
mbalimbali wa kiroho, moja wapo ni hili la kuanzishwa kanisa la wala
nyasi nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa kanisa hilo lipo maeneo ya
Upanga jijini Dar na huduma yao inafanywa kwa kutumia jina la Rabboni
Centre Ministries yenye makao yake makuu jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Mwandishi alifika Upanga kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ndilo kanisa hilo lakini hakuna mtu aliyekutwa hapo.
Hata hivyo, baadhi ya majirani walisema huwa wanawaona watu wakiingia
katika nyumba hiyo lakini ajabu kunakuwa hakuna kelele zozote.
“Mchungaji wao huwakusanya waumini wake wanaopandisha mashetani wakiwa kanisani, hiyo hufanya shetani kumtoka mtu haraka,” kilisema chanzo.
Habari zinasema huduma hiyo ilianzishwa Afrika Kusini na Mchungaji na Nabii Daniel Lesego mwaka 2002.
Imedaiwa kuwa kwa sasa waumini hao wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na baadaye kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo wakisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.
chanzo:global puplisher
0 comments:
Post a Comment