Saturday, 18 January 2014

JK AMTEUA PAUL MASANJA KUWA KAMISHINA WA MADINI

Filled under:



Rais Jakaya Kikwete amemteua Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Paul Masanja kuwa Kamishna wa Madini.
 
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliyoitoa  Dar es Salaam jana ilisema uteuzi huo ulianza  Alhamisi wiki hii.
 
Wadhifa wa Kamishna wa Madini ulikuwa unashikiliwa na Dk Peter Kafumu, ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM.
 
Nafasi yake ilikaimiwa kwa karibu miaka miwili na Ali Samaja kabla ya uteuzi wa Masanja.

0 comments:

Post a Comment