
Kyela. Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Kasumulu eneo la ‘Juakali’,
wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya, jana walimiminika nyumbani kwa mama wa
watoto pacha, Grace Joel ili kushuhudia jinsi walivyotenganishwa baada
ya kufanyiwa upasuaji nchini India hivi karibuni.
Watoto hao pacha, waliozaliwa wakiwa wameungana
eneo la kiunoni, waliwasili na mama yao nyumbani kwao wilayani Kyela na
kulakiwa na wanakijiji wengi.
...