Waziri wa mambo ya nje nchini Uganda, Sam Kutesa
amesema ana wasiwasi kuwa Marekani huenda ikasitisha msaada wake kwa
taifa hilo baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria dhidi ya
ushoga nchini humo.
A
Bwana Kutesa amesema kuwa watu sharti wawe na maadili na kukubali msaada.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Scott DeLisi, awali aliitaka serikali ya Uganda, kubatilisha sheria hiyo.
Alisema alihitaji kufafanuliwa zaidi sheria
hiyo, kabla ya Marekani kujua ikiwa itaendelea na mipango yake ya
misaada kwa nchi hiyo hasa miradi ya kupambana dhidi ya HIV na Ukimwi..
Sheria hiyo mpya, inatoa adhabu kali kwa watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kupiga marufuku kile inachosema
kusambaza vitendo vya ushoga.
0 comments:
Post a Comment