Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

Tuesday, 6 May 2014

JE UNAFAHAMU ACHAWI ANAOTUMIA DIAMOND NA JINSI ULIVYOMFIKISHA ALIPO SASA?

Filled under:

Unajua kwa nini  Diamond anazidi ku-make headlines siku hadi siku?, kama ilivyo kwa msanii yeyote yule mwenye mafanikio duniani, kuna ishu mbili tatu zilizowahi kumtokea katika maisha yake, ambazo ndio zilimpelekea kumsukuma, pamoja na jitihada za kujituma, kuweza kumfikisha hadi kwenye mafanikio yake. Kama ulikuwa hujui, basi bila Diamond kufanya haya, hii leo, hizo tuzo zote, kuanzia ya mtv na kili zingekuwa bado ni ndoto, na kwa hapa Tzee angekuwa na-hit tu kinyumbani nyumbani kama ilivyo kwa wasanii

Kuwako kwa Manager wake wa zamani, hii leo asingekuwa amefikia hapa alipo, manyanyaso aliyoyapata hapo nyuma, akiwa na uongozi wake wa zamani, ndio iliyomsukuma kufanya vitu kwa bidii na kufikia hadi hii leo, mbali na struggle zake za kila siku katika kujitangaza kimuziki.
1diamond
Inasemekana kuwa management yake ya sasa ndio inayompa sapoti kubwa sana katika kufanya vitu ki-international zaidi, na jina lake kuzidi kukua ulimwenguni, hadi kwa hivi sasa watu wamesha msahau Diamond wa mbagala.
Alipoamua kufaya jambo la hatari katika muziki wake.
Cover
Kama ilivyo katika kila biashara, bila risk huwezi kupata kile ulichokuwa unatarajia, na wala huwezi kuendelea, utabaki hapo hapo siku zote, hii ndio mchezo aliofanya Dangote, kuanzia kutoka kufanya video za milioni mbili hadi kufikia mahali na kufanya video za zaidi ya milioni ishirini, kitendo hichi ndicho kilichopelekea Diamond Platnumz aweze kujulikana zaidi nchi mbali mbali, haswa kwa nyimbo yake ya “my Number1”. Ni moja kati ya vitu ambavyo matunda yake yanaonekana hadi leo, kwa kuendelea kukaa on top kwenye charts, hadi kumpelekea tuzo mbalimbali.
Uchawi wake na mashabiki.
Diamond na Ney wa Mitego jukwaani
Ukitasmini vizuri katika game la hapa Bongo, unaweza kusema Diamond anatumia uchawi, jambo ambalo hata watu wengi wasioelewa faida za kufanya kazi kwa bidii na kujituma ndio zinazomfanya Diamond Platnumz azidi kutoa nyimbo kali kila siku na kuzidi kupendwa na mashabiki wake, kitu kinachopelekea kuwa na u-lukuki wa mashabiki kila siku.Diamond ndiye msanii anayesemakana kuwa na heshima na kuwajali mashabiki wake wa kila rika popote pale alipo,Diamond Platnumz ndiye msanii anayeongoza kuwa na mashabiki wengi zaidi hapa bongo na nje ya mipaka ya Tzee.

Posted By Unknown10:28

Friday, 18 April 2014

DIAMOND AFUNGIWA ASHINDWA KUMZIKA MZEE GURUMO

Filled under:

Kuna madai kwamba Nasibu Abdul ‘Diamond’ alishindwa kushiriki zoezi la kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo ‘Maalim Gurumo’ kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake madam Wema Sepetu,
 
Wema Sepetu na Diamond wakiwa faragha.
Imedaiwa kuwa, Wema alimfanyia ‘umafia’ mpenzi wake huyo, Aprili 15, mwaka huu ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa marehemu huyo kuagwa nyumbani kwake Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki, Kisarawe, Pwani.
Itakumbukwa kuwa, Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.
Diamond akimsaidia mzee Gurumo kupanda  stejini kabla ya kumkabidhi gari Agosti 29, 2013.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kitendo cha Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni kama amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.

“Tulitegemea tungemuona msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa gari Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo ukiingizwa kaburini.
Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo, walibaini kuwa, Diamond hakutia ‘maguu’ hivyo shughuli ya kumsaka ikaanza.

Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Mapaparazi hawakuchoka, wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa mwanandani wake Wema, Makumbusho, Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa, Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.
Mzee Maalim Gurumo enzi za uhai wake.
Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia waliambiwa wapendanao hao bado wamejifungia ndani, wakaondoka hadi muda wa jioni baada ya shughuli za mazishi, walirejea na kuambiwa 

Diamond alitoka muda si mrefu pasipo kujulikana alikoelekea.
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda  mrefu bila kupokelewa.

Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
Mzee Gurumo akionyesha ufunguo wa gari alilozawadiwa na Diamond.
“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena tumefika muda huohuo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi amini tulijumuika kuupandisha mwili kwenye gari na sisi tukarudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu,” alisema Babu Tale.
Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.
Diamond na mpenzi wake Wema katika pozi.
“Mh! Nilikuwepo msibani ila sikwenda kuzika tu maana nilikuwa na Babu Tale pale na tulikuwa karibu kabisa na gari la Global Publishers, mara tu baada ya kumaliza kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari tuliondoka na kurejea kwenye majukumu yetu,” alisema Diamond.
Mapaparazi wa Global walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwa nini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!

Source:Global publisher

Posted By Unknown00:30

Tuesday, 8 April 2014

MWASITI:SITAKI MWANAUME

Filled under:

STAA anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva akitokea Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’, Mwasiti Almas, amesema kwa sasa hataki kusikia habari za mwanaume kabisa.
Akizoza na mwandishi wetu, Mwasiti alisema: “Sitaki mwanaume, nahitaji kujipanga kimaisha kwanza. Kama kuna mtu anafikiria kuwa na mimi, aandike maumivu. Hakuna hiyo nafasi.

“Sina mwanaume na sitaki. Bado niponipo sana,…


.
 
Staa anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva akitokea Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’, Mwasiti Almas akipozi.
Akizoza na mwandishi wetu, Mwasiti alisema: “Sitaki mwanaume, nahitaji kujipanga kimaisha kwanza. Kama kuna mtu anafikiria kuwa na mimi, aandike maumivu. Hakuna hiyo nafasi.
“Sina mwanaume na sitaki. Bado niponipo sana, nitabadili uamuzi huu mambo yangu yakikaa poa kimafanikio. Mapenzi si ya kukurupukia.”




Posted By Unknown21:47

Monday, 7 April 2014

BIFU ZITO LAZUKA KATI YA WEMA NA KAJALA KISA!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Filled under:

Kwa muda mrefu sasa, Kajala amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii hasa matusi ambayo hayaandikiki huku akipachikwa jina la ‘Milioni 13 za Wema’ na kuahidiwa…

NI shida! Zile shilingi milioni 13 alizotoa Wema Isaac Sepetu kumlipia msanii maarufu wa sinema Bongo, Kajala Masanja asitupwe gerezani, bado ni tatizo ikidaiwa kuwa sasa ngumi nje nje.
 
Kajala akitoa maelezo kwa uchungu unaodhihirisha uhasama kati yake na Wema.
JINA LA MILIONI 13 ZA WEMA
Kwa muda mrefu sasa, Kajala amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii hasa matusi ambayo hayaandikiki huku akipachikwa jina la ‘Milioni 13 za Wema’ na kuahidiwa kichapo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Kajala, staa huyo hana raha wala furaha kwani ishu hiyo inamtesa kila kukicha.

 
Wema Isaac Sepetu.
Ilidaiwa kwamba Kajala ana mtoto mkubwa aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye anajua kuingia kwenye mitandao hiyo hivyo kufedheheshwa hasa anapokuta mama yake akiitwa fuska wakati yeye anamheshimu.
 
Kajala akizidi kufunguka juu ya kisa cha ugomvi dhidi yake na Wema Sepetu.
KUNDI LA TEAMWEMA
Ilisemekana kwamba Wema ana kundi linalojiita TeamWema ambalo memba wake wamekuwa wakianzisha mada mbaya kuhusu Kajala wakimhusisha na uporaji wa aliyekuwa bwana wa Wema, Clement au CK.

Ilifahamika kwamba shinikizo kubwa la kundi hilo la Wema ni kutaka Kajala arejeshe fedha hizo ndipo mambo yakae sawa.
 
Kajala wakati akiwasili katika ofisi za GPL, Mwenge Bamaga.
“Anamdharau sana Madam (Wema) wakati ndiye aliyemnusuru, sasa hivi angekuwa jela. Kama ana fedha kama anavyotamba basi arudishe milioni kumi na tatu twende sawa,” ilisomeka sehemu ya maoni ya TeamWema kwenye ukurasa wao wa kijamii wa Instagram.
Kuna madai kwamba kumekuwa na mtafutano kati ya kundi la Wema na lingine jipya linalodaiwa ni la Kajala.

TIMBWILI KLABU
Kwa mujibu wa shushushu wetu ndani ya Ukumbi wa Maisha uliopo Masaki, Dar, wiki iliyopita, usiku wa manane, wawili hao walikutana ndipo kukatokea timbwili huku jina la Milioni 13 za Wema likiendelea kutajwa mara tu Kajala alipoonekana ukumbini hapo.


Habari zilidai kuwa wawili hao walianza kwa kushindana kumtuza Snura Mushi aliyekuwa akifanya shoo jukwaani ndipo wapambe wao wakaingilia kati na ‘kuinunua kesi’.

Ikadadavuliwa kuwa tukio hilo lilichochea kundi la Wema kuanza vurugu huku lile la Kajala nalo likijibu mapigo.

 
Kajala Masanja akiwa ndani ya ofisi za GPL.
KAJALA NDUKI
Hata hivyo, ilisemekana kwamba baada ya Kajala kuona hali inazidi kuwa mbaya alitumia busara kwa kutoka nduki lakini kundi hilo la Wema lilizidi kumfuata hadi kwenye gari lake wakitaka kumdhuru.
“Kuna watu walimfuata kabisa hadi kwenye gari na wengine walikuwa wanatafuta mawe walipopoe gari lake lakini Mungu mkubwa hawakufanikiwa,” alisema shuhuda wetu.


Baada ya kunyaka habari hiyo, gazeti hili lilimtafuta Kajala ambaye alidai kuwa yeye hakushuhudia tukio hilo lakini akakiri kuwa hana uhusiano mzuri na Wema.


“Mimi kwa upande wangu sina tatizo na Wema lakini natukanwa sana bila sababu. Sijui nimemfanyia nini kibaya.

 
Kajala Masanja wakati akihojiwa na waandishi wa GPL kuhusu sakata hilo.
“Narudia tena sina tatizo na Wema halafu siyo yeye anayenitukana au kunisakama, ni kundi linalojiita TeamWema. Sina uhakika kama yeye ndiye anawatuma.

“Kuhusu milioni 13, sasa nitazirudishaje wakati hakunikopesha, alinilipia bure? Hata sijui kama nikizirudisha nitakuwa sahihi? Sielewi lakini kama ni matusi, kweli natukanwa sana hadi mwanangu anaona ninavyoitwa malaya,” alisema Kajala kwa uchungu.

Alipoulizwa kama yupo tayari kupatanishwa na Wema, Kajala alisema yeye hana kipingamizi kwani yupo tayari wakati wowote ili aishi kwa amani.
 
Kajala akiondoka baada ya mahojiano na GPL.
Jitihada za kumpata Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
MILIONI 13 KIVIPI?
Wema alimlipia Kajala Sh. milioni 13 kama faini baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano alipopatikana na hatia ya kushirikiana na mumewe Faraji Agustino Chambo katika utakatishaji wa fedha haramu. Katika hukumu hiyo mume wa Kajala alitupwa jela kifungo cha miaka saba.


Source:Global Publisher

Posted By Unknown01:29

Tuesday, 1 April 2014

BIFU ZITO LAZUKA KATI YA LULU NA MSHIRIKI MISS TZ (HUSNA MAULID) KISA!!!!!!!!!!!!

Filled under:

Elizabeth Michael  kwa jina jingine ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Staa Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika pozi.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.

Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”

Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”

Source:Global publisher

Posted By Unknown06:28

Monday, 24 March 2014

BAADA YA KUBWAGANA NA RAY ,MAINDA APATA UJAUZITO

Filled under:

Siku chache baada ya kuliambia gazeti ndugu la hili, Amani kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa chango hivyo inambidi azae, super lady wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ anadaiwa kuwa mjamzito, Ijumaa Wikienda limechimba kila ‘engo’.

MUONEKANO
Habari zilieleza kwamba kimuonekano, Mainda aliyezoeleka kuonekana mwembamba, sasa ameanza kunenepa huku kitumbo nacho kikianza kuwa kikubwa.

Habari kutoka kwa mmoja wa mashosti zake aliyeomba hifadhi ya jina, zilidai kwamba kila amuonapo Mainda anagundua kuwa ana mabadiliko fulani ndani ya mwili wake hasa tumbo lake kuongezeka ukubwa.
“Unajua Mainda ni msiri sana hasa katika kipengele cha kuzungumzia mwili wake, kila tukimuuliza shosti wetu kama ni mjamzito anakataa.

“Anadai eti ana matatizo ya ugonjwa wa chango lakini ukimwangalia tumbo unaona linazidi kukua, binafsi mimi naamini ni mjamzito ila yeye anafanya siri,” alidai rafiki huyo.

APELEKWA HOSPITALI
Habari zilizotufikia zilidai kuwa mwanadada huyo alipelekwa kwenye Hospitali ya Kinondoni maarufu kwa jina la kwa Dokta Mvungi jijini Dar.

Siku hiyohiyo mwanahabari wetu alizama hospitalini hapo ambapo alikutana na vizuizi vingi kwa kuwa moja ya masharti huruhusiwi kuingia wodini bila kufuatana na ndugu wa mgonjwa.

Katika jitihada za kuthibitisha kama Mainda kalazwa hapo na kujua kinachomsumbua, mmoja wa madaktari (jina linahifadhiwa) ambaye anamfahamu mwandishi wetu alimtonya kuwa ni kweli Mainda alifikishwa hospitalini hapo.

UGONJWA, UJAUZITO
Kuhusu ugonjwa uliompeleka hospitalini hapo na habari kuwa ni mjamzito, dokta huyo alisema: “Ninavyojua mimi, ugonjwa ni siri ya daktari na mgonjwa au na ndugu. Nadhani muulize mwenyewe, akipenda atakwambia. Ni kweli alikuwepo na amesharuhusiwa.”

Baadaye mwandishi wetu alikwenda hadi nyumbani kwa Mainda, Kijitonyama, Dar lakini alijibiwa na majirani kuwa hayupo kwa muda mrefu.
h 

APOKEA SIMU
Hata hivyo, juhudi za kumpata, ziliendelea ambapo alitumiwa ujumbe mfupi, alipopigiwa akapokea.
Katika mazungumzo yake na mwandishi, Mainda alikiri kuwa anasumbuliwa na chango na kwenda hospitali lakini alikataa kuzungumzia ishu ya ujauzito.
“Mimi nilishasema nasumbuliwa na chango, huo ujauzito unaosema, hata kama upo, tusubiri kwani huwa haufichiki,” alisema Mainda.

UTATA
Baada ya habari kuwa ya mjini, ishu hiyo iliibua utata kuwa kama ni ugonjwa wa chango, inawezekana mtu akazidiwa kiasi hicho hadi kukimbiza hospitali?
Pia ilihojiwa kuwa kama kweli ni mjamzito, je, baba wa kiumbe hicho ni nani?

NI MIMBA YA PILI?
Kama kweli Mainda atakuwa mjamzito basi itakuwa ni mimba ya pili baada ya kukiri kuwa aliwahi kuchoropoa ya aliyekuwa mtu wake, mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye walishamwagana.

Chanzo :Global Publisher

Posted By Unknown03:32

Saturday, 15 March 2014

JOHARI YUPO MBIONI KUOLEWA

Filled under:

Hayawi hayawi sasa yamekuwa .Hatimaye staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ yuko kwenye mwanga wa maisha ya ndoa kufuatia Kiongozi wa Kundi la Mtanashati, Ostaz Juma Namusoma kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi huku akisema ana mpango wa kumuoa kabisa,

Staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johar
Hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Ostaz alitumbukiza picha inayomwonesha yeye akiwa katika ‘pozi nono’ na Johari huku akimsifu mwandani wake huyo. Hali hiyo ilisababisha maswali kwa baadhi ya mashabiki wa Johari., wawili hao wako ‘klozidi’ tangu kitambo hasa baada ya penzi bubu la Johari na staa mwenzake wa sinema za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuparaganyika.

Kwa sasa Ray anadaiwa kutoka kimapenzi na mcheza filamu mwenzake, Chuchu Hans ambapo nao inadaiwa wako katika mikakati ya kufunga ndoa kama si pingu za maisha.

Johari na Ostaz Juma katika picha ya pamoja.
Chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, Ostaz amekufa kimapenzi kwa Johari, ‘hakohoi, hanywi maji, halali usingizi’ na yuko tayari kwa ndoa itakayokuwa ya kifahari.
“Ukitazama hapo Johari hana kipingamizi, ingekuwa zamani angesema yuko na Ray kuna kikwazo cha yeye kuolewa na Ostaz, lakini kwa sasa kipi kitamzuia?” chanzo hicho kilipayuka.

MSIKIE OSTAZ
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo na picha ya wawili hao kwenye mtandao, mapaparazi wetu walimsaka mwanaume huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu yake ya mkononi na mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kaka kuna tetesi kwamba una uhusiano na Johari, unasemaje?
Ostaz: We nani?
Risasi: Mwandishi wa Risasi Jumamosi.
Ostaz: Ndiyo Johari ni wangu na mimi ni wake, tutafunga ndoa watu watashangaa sana.
Risasi Jumamosi: Huoni kama Ray atakukasirikia?
Ostaz: Kwani yeye ndiyo amemzaa Johari?
Risasi Risasi: Lakini kaka wewe mbona umeoa?
Ostaz: Mbona sikuelewi, Muislam mwisho ni wake wangapi?
Risasi Jumamosi: Vipi mkeo karidhia na lini ndoa?
Ostaz: Na Johari anataka kuslimu kuwa Muislam, tumepanga jina, ataitwa Rahma.
Risasi Jumamosi: Jambo jema. Mmeanza lini uhusiano wenu?
Ostaz: Hayo mengine muulize Johari mwenyewe mi nimeshasahau maana nina mambo mengi ya kujenga taifa.
“Lakini mimi nilianza na Johari kabla ya huyo Ray wenu, wakati huo Johari akiwa anaishi Mburahati (Dar), yeye alikuwa anafanyia mazoezi ya kuigiza pale TZF (baa), Kigogo.”
JOHARI SASA
Kutokana maelezo hayo ya Ostaz, Risasi Jumamosi lilimtafuta Johari kwa simu yake ya mkononi na kumuuliza kama kweli yu mapenzini na mfanyabiashara huyo maarufu jijini Dar.
Johari: “Hamna bwana, kama Ostaz mwenyewe ndo’ kasema hivyo huenda alikuwa anatania tu. Kweli hakuna kitu kama hicho, ila ni mtu ambaye nina ukaribu naye mkubwa lakini si mapenzi.
Risasi Jumamosi: Kama ametutania mbona sisi siyo watani wake?
Johari: Mimi sijui sasa, yeye ndiyo anajua.
Risasi Jumamosi: Kama ni hivyo, wewe huoni kwamba utani wake ni mkubwa sana?
Johari: Mimi sijui chochote jamani, muulizeni yeye.
Baada ya kuzungumza na Johari, Risasi Jumamosi lilimgeukia Ostaz na kuulizwa kama kuna utani ndani ya maelezo yake.
“Jamani, ninyi mnachotakiwa kukielewa ni kuwa, Johari ni wangu na mimi ni wake. Siku ya ndoa tutaitangaza, itakuwa ndoa kubwa sana na Johari nitamfanyia mapenzi ambayo hajawahi kufanyiwa tangu azaliwe.”
 WASEMAVYO MASTAA KUHUSU JOHARI NA OSTAZ
Baada ya kumalizana na wawili hao, Risasi Jumamosi liliwatafuta mastaa wa filamu za Bongo ili kusikia kutoka kwao wanachokijua kuhusu Johari na Ostaz.
Mastaa waliopatikana ni watatu, lakini wote walitoa ushirikiano kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini.
WA KWANZA, MWANAUME:
“Khaa! Mbona siyo siri, kwani nyie mmejua lini? Wale wako tangu zamani sana tena wengine mpaka tukadhani walishaachana, kumbe bado wapo pamoja?”
WA PILI, MWANAUME:
“Oohooo! Mlikuwa hamjui? Wale ni wapenzi. Mimi ninavyojua wana mpango wa kufunga ndoa lakini sijui ni lini na Johari atabadili dini.”
WA TATU, MWANAMKE:
“Mh! nilishasikiasikia, unajua Johari ni msiri sana, hajawahi kuweka wazi lakini ni kweli wana uhusiano wa kimapenzi.”
KAMA NI KWELI, CHEKI SINEMA YAKE
Endapo ni kweli Johari atabadili dini, ina maana atakuwa amekwenda sambamba na Ray kwani yeye anadaiwa kubadili dini kwa ajili ya kumuoa Chuchu Hans, Johari atabadili dini ili aolewe na Ost


Chanzo;Risasi

Posted By Unknown11:26

LULU AFUNGUKA:SITAKUJA KUFANYA KOSA TENA ,NITAZAA TU

Filled under:

STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kama siku yoyote atapata ujauzito kwa bahati mbaya, hatafanya kosa tena, atazaa tu. ,Lulu alisema kwa sasa yuko tayari kuolewa ili awe na familia yake ila si kwa sharti la mwanaume husika kumwambia amzalie kisha ndiyo amuoe.
E‘Lulu
Ijumaa: Kwani kwa sasa si una mpenzi?
Lulu: Ndiyo ila bado sijapanga swala la kufunga naye ndoa. 
Ijumaa: Kwa hiyo umesema ukipata mimba kwa bahati mbaya hutofanya misteki lazima uzae, unaweza kuniambia ni misteki gani?
Lulu:Nadhani maswali yako uliyoniuliza nimekujibu kiufasaha kabisa hilo siwezi kulijibu.
Ijumaa linahisi kosa ambalo Lulu hatalirudia tena ni la kutoa mimba, kitu ambacho hataki kukizungumzia.


SOURCE:GLOBAL PUBLISHER

Posted By Unknown02:38

Thursday, 13 March 2014

ALIKIBA ANUSURIKA KUUAWA,DIAMOND AFUNGUKA KUWA AMEJIANDAA KUHOJIWA POLISI

Filled under:


SAKATA la staa wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana kwa kutumia bastola limechukua sura mpya, safari hii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa amejiandaa kuhojiwa na polisi.
Ally Saleh ‘Ali Kiba’.


Kwa mujibu wa chanzo chetu katika jeshi hilo jijini Dar, Diamond ambaye amekuwa akitajwa sana katika sakata hilo kupitia mitandao ya kijamii ataitwa kuhojiwa.

“Unajua ile kesi ipo hapa Central, awali ilitokea Polisi Msimbazi, sasa mpelelezi wake amekuwa akifikiria kumwita Diamond ili amhoji maana anatajwa sana,” kilisema chanzo hicho.

Hivi karibuni, Ali Kiba alivamiwa usiku na watu zaidi ya watano nyumbani kwao, Kariakoo jijini Dar ambapo waliruka ukuta na kuingia ndani huku kila mmoja akiwa na bastola.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Ilidaiwa kuwa, mmoja kati ya watu hao ambao ilisemekana walitumwa kumuua msanii huyo, aliibua mzozo wa makusudi kwa wenzake ili kumpa mwanya Kiba kutoroka kwa vile hakufurahishwa na kitendo hicho.
Habari zinasema walipoingia ndani huku kelele za mbwa zikasaidia kumshtua staa huyo, ule mzozo ulioanzishwa na wavamizi hao ulimsaidia Kiba kutoroka ingawa walimkosakosa risasi.
Ikasemekana baada ya msanii huyo kukimbia, jamaa ambaye alimkingia kifua alimpigia simu na kumfungukia watu waliohusika huku ikidaiwa kuwa baadhi yao ni mastaa wenzake.
“Alinitajia tu majina lakini nilishindwa kuthibitisha moja kwa moja hivyo nikayafikisha Kituo Kikuu cha  Polisi (Central) kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Ali Kiba huku akikataa kutaja hata jina moja.
Hata hivyo, mengine yaliibuka hasa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, miongoni mwa wasanii waliohusika katika tukio hilo eti ni na Diamond.
Amani lilimsaka afande mmoja ambaye anajua mwenendo wa kesi hiyo ambaye alikiri kesi hiyo kuwepo Central lakini alisema mambo yote ni siri ya kazi.
“Nani atahojiwa, nani hatahojiwa ni siri ya kazi yetu,” alisema.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.

“Nimeshasikia nikitajwa katika hilo, kimsingi ni madai mazito lakini mimi nipo tayari kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake kwani najua si kweli na sijui lolote,” alisema Diamond.
Akandelea: “Mimi na Kiba kuna ugomvi gani hadi nifikie hatua hiyo. Kwanza sina moyo wala uwezo wa kufanya hivyo.”

CHANZO :GLOBAL PUBLISHER

Posted By Unknown01:39

WEMA NA AUNT EZEKIEL WADONDOSHEWA KIPIGO KWEUPEE KISA!!!!

Filled under:

Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani limeinyaka.
Wema Sepetu.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
ALIANZA WEMA
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.


“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
Aunt Ezekiel.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.
HASIRA
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema chanzo hicho.

KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa kibao.
Adam Kuambiana.


KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile sauti yake nzito.
WEMA & AUNT
Kwa upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi  aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.

HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa ‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani Zanzibar.

Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika kujibishana akamuwasha makofi.

HATA MITAANI!
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.

MADAIREKTA WANA TABIA GANI?
Mbali na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya kurekodia filamu.


CHANZO: GLOBAL PUBLISHER

Posted By Unknown00:53

Wednesday, 12 March 2014

WEMA SEPETU ALILIA KIU YA KUTAPA MTOTO

Filled under:


MASKINI! Kilio kikubwa cha Wema Isaac Sepetu ni kupata mtoto, Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Habari zilieleza kuwa Wema amekuwa na kiu ya mtoto kwa muda mrefu na kwamba alishakuwa na wanaume tofauti lakini hawakumpatia mtoto.

Ilisemekana kwamba katika msururu wa wanaume aliominya nao kimalavu, iliwahi kuripotiwa kuwa ni mwanaume mmoja tu aliyefanikiwa kumpa ujauzito lakini kwa bahati mbaya mimba ilichoropoka.

Mwanaume aliyekuwa na mzigo huo ilidaiwa ni Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.

Baada ya kupania kwa muda mrefu bila mafanikio, ilidaiwa kuwa mwanadada huyo mkali wa sinema za Kibongo aligeuzia mapenzi yake kwa mbwa (pets) wake wawili, Van na Gucc ambao mmoja wao amezaa hivi karibuni.
Habari zinadai kuwa, kutokana na mapenzi yake na mbwa hao, amekuwa akiwagharamia mkwanja mrefu katika chakula na shopping za mavazi ya bei mbaya.

WEMA ANAFAFANUA
 

“Nawapenda sana mbwa wangu, nawaona kama ndiyo watoto wangu kwani sina mtoto na ninatamani sana ila najua Mungu atanijalia siku moja muda ukifika,” alisema Wema na kuongeza:

“Kila jambo na wakati wake, nitapata tu, nadhani ni suala la muda tu. Watu wanaweza kushangaa namna ninavyowapenda mbwa wangu, nawathamini kwa sababu wananipa faraja na nipo nao karibu. Nawajali kama binadamu.”

Kabla ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayetoka naye kwa sasa, wengine waliowahi kuonja penzi lake na wakashindwa kumpatia mtoto ni pamoja na marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf na Chaz Baba.

Posted By Unknown04:36

Friday, 28 February 2014

DOGO ASLAY ATIRIRIKA KUHUSU MATOKEO YAKE YA KIDATO CHA NNE

Filled under:

Dogo Aslay

 BAADA ya kupata matokeo mabaya kidato cha nne, kinda wa muziki wa kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ amesema anatarajia kusoma chuo cha muziki ili kukuza kipaji chake.

Akizungumzia matokeo hayo, Aslay alisema hajasikitika sana kupata matokeo hayo na wala hajakata tamaa ya kuendelea kusoma, kwani anataka kusomea muziki kwa lengo la kuongeza ‘mautundu’ katika kazi zake.

“Nimepata 4 ya pointi 32, kwa sababu nilikuwa nachanganya muziki na masomo, hivyo sijayachukia sana matokeo hayo na kwa kuwa muziki ndio kitu ninachokipenda, nataka kusoma chuo cha muziki na si kupoteza muda kuanza ‘kurisiti’, bado sijajua nitakwenda chuo gani kwa ajili ya masomo hayo,” alisema.

“Wengi wamekuwa wakinisema kwamba napoteza muda mwingi kwa kufanya muziki na kusahau masomo, ndiyo maana nafeli, mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale napenda muziki ndiyo maana nafanya vizuri na ndiyo maana nataka nikaongeze elimu katika muziki wangu,” alisema Aslay.

Dogo Aslay ni kati ya wasanii wenye umri mdogo ambao wanafanya vizuri katika muziki huo, huku akitambulishwa na ngoma yake ambayo ilibamba vilivyo ‘Naenda Kusema kwa Mama’.

Posted By Unknown11:12

Monday, 24 February 2014

MSANII ALIYEMPONDA DIAMOND ATISHIWA MAISHA

Filled under:


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Masige Bukori ‘Cado Baro’, amesema anazidi kutishiwa maisha kwa kupigiwa simu mara kwa mara, zikimtaka asiende kwenye ukumbi wowote kutumbuiza nyimbo zake.

Cado Baro alisema amekuwa akipigiwa simu za vitisho kila anapopata mwaliko wa kwenda kufanya onesho katika mikoa mbalimbali nchini, zikimtaka asithubutu kwenda, kwani maisha yake yatakuwa hatarini.

Alisema kuwa tangu atoe ‘remix’ ya wimbo wa Diamond ‘My Number One’ ile inayomtaka msanii huyo aache wizi, ndipo alipoanza kupigiwa simu za vitisho na mtu asiyemfahamu kila anapoitwa kufanya onesho katika matamasha mbalimbali.

Posted By Unknown09:39

Monday, 17 February 2014

KESI YA LULU MICHAEL YAPIGWA KALENDA

Filled under:



KESI inayomkabili staa wa sinema za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ dhidi ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba imeunguruma leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku mtuhumiwa akikiri baadhi ya mashtaka.

Lulu alikiri mbele ya Jaji Temba kuwa alikuwa  na uhusiano wa kimapenzi na  marehemu kanumba ,pia alisema kulitokea kutoelewana baina yao ndipo ulitokea ugomvi  na kusababisha kifo,pamoja na hayo yote Lulu alikana shitaka hilo la uuaji.
Hati ya mashitaka ilisomwa ilisoma na Wakili Mwandamizi mbogo alidai kuwa April7,2012,Sinza Vatikan,Jijini Dar es Salaam,Mshitakiwa alimuua Steven Kanumba bila kukusudia'

Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo watakapojulishwa na mahakama tarehe ya kusomwa kwa shitaka lake la kuua bila kukusudia.

Posted By Unknown08:10

Sunday, 16 February 2014

MAJANGA YAMKUTA WASTARA,APATA AJALI TENA

Filled under:

                       

Maskini Wastara, Siku chache baada ya hivi karibuni kudaiwa kunywa sumu, staa mkubwa wa sinema Bongo, Wastara Juma amepata tena ajali mbaya.

Habari za uhakika zilizolifikia  mwishoni  mwa wiki iliyopita zilieleza kuwa siku ya tukio Wastara alitoka nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar na gari lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili ya kwenda kununua umeme.

Akizungumzia tukio hilo kwa masikitiko, Wastara aliliambia gazeti hili kuwa kabla ya kufika kwenye kituo cha kununulia umeme (Luku) alikutana na lori kubwa lililokuwa kwenye mwendo kasi huku likiwa limewasha taa fulu.


Alisema kuwa alijaribu kulikwepa lakini lilimsukuma na kujikuta akiingia mtaroni kutokana na barabara kuwa nyembamba ambapo aliumia sehemu za kichwani na mguuni kwa ndani.

Wastara alisema baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya TMJ, Dar ambapo alisafishwa majeraha (dressing) kisha akapatiwa matibabu na baadaye aliruhusiwa kurudi nyumbani.

“Nimenusurika kifo, namshukuru sana Mungu kwani ajali ilikuwa mbaya nilihamishwa kwenye siti niliyokuwa nimekaa na kurushwa kwenye siti nyingine huku nikijigonga na kuumia kichwani.

“Pia gari langu limeharibika sana, kioo chote kimevunjika, sielewi kwa nini haya yote yananitokea.
 
“Namuomba Mungu anisaidie maana naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo na kwa nguvu zangu mwenyewe siwezi,”alisema Wastara.

Hata hivyo, Wastara kwa sasa anaendelea vizuri japokuwa bado anaumwa kichwa na mguu.
Wastara ameshapata ajali mara kadhaa ikiwemo ile ya pikipiki aliyopata mwaka 2008 akiwa na aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Pia aliwahi kupata nyingine ya gari akiwa na Sajuki.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Wastara, kuna watu wanamtakia mabaya ili amfuate Sajuki aliyefariki Januari 2, mwaka jana.

Chanzo:Global Publisher

Posted By Unknown20:31

DIAMOND AMPA UJAUZITO WEMA SEPETU, WEMA AFICHUA SIRI YA UJAUZITO WAKE KATIKA INSTAGRAM

Filled under:



MSANII maarufu wa Bongo Movie, mrembo na mwenye pesa pengine kuwazidi wengi na ambaye hivi karibuni amezua mijadala mikubwa baada ya kurudiana na mpenzi wake wa zamani Diamond, ambaye pia ni maarufu katika muziki wa kizazi kipya nchini na mwenye kuongoza kwa mapato nchini, imegundulika kuwa ana ujauzito wa miezi kadhaa.

Wema ambaye alishindwa kuficha hisia zake na hatimae kuweka kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa instagram,” …mmmmmh jamani hichi kitumbo… hakifichiki now…” kuashiria kuwa mabadiliko ya mwili yameshaanza kuonekana (Picha chini inaonesha ujumbe huo kamili).
Mtandao wa huu ulianza kuhisi taarifa hizo na kuamua kuzifuatilia kwa karibu ili kujua nini haswa kinaendelea au ni hisia tu. Ndipo mwandishi alipochukua jukumu la kumtafuta mlimbwende huyo Wema Sepetu na kugonga mwamba.

Hata hivyo jitihada hizo hazikuishia hapo ndipo kilipopatikana chanzo cha karibu na Wema na kudai kuwa “ amekuwa akilalamika mabadiliko hayo na hata kusikika akisema anaihisi ameconsive…” kilisema chanzo hicho bila kutaka kutambulika hadharani.
“Ni kweli itakuwa hivyo na ndio maana Diamond aliamua kumtangaza rasmi siku hile ya chrismas” aliongeza.

Diamond ambaye alimtupilia mbali mpenzi wake Penny na kurudiana na Wema mapenzi yao hayakufichika kwani wakiwa China walipiga picha za mahaba na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia tofauti.

Hivi karibuni wamekuwa karibu sana kimapenzi na kuamua kuonesha siri zao za ndani bila kuficha, “mwenye macho haambiwi ona… juzi tu wameweka video zao wakiwa kitandani kila mtu ameziona, lakni pia Diamond kumnunulia nyumba baada ya kusikia mkataba wake umeisha na kwamba hautoongezwa, na mambo mengine kibao” kiliongeza chanzo hicho

“lakini tusubiri miezi tisa tu sio mingi na mimba huwahaifichiki bana tutaona 

Source:Vijimambo

Posted By Unknown00:51

Friday, 14 February 2014

DUDE AWAPONDA WASANII WA KIKE ASEMA!!!!!!!!!,MASTAA NAO WAJA JUU

Filled under:


 Wasanii wa kike wanaotamba kwenye filamu za Kibongo, hivi karibuni wamembwatukia staa mwenzao, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na kuipinga kauli yake kwamba mastaa wengi wa kike wametokea kwenye uchangudoa na kuvamia tasnia hiyo, shuka na mistari uipate habari hii.

Wakizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamemtaka Dude kuacha tabia ya kuropoka kwani kauli yake imewavunjia heshima mbele ya jamii.

Mastaa waliopinga kauli ya Dude


TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“ Ni heri Dude aache kuzungumza vitu visivyokuwa na maana, ajifunze  mambo mazuri kwani ni mtu mzima sasa. Kila mara anatuponda wasanii wa kike, kila mtu ana maisha yake kama wapo wanaofanya uchangudoa hao ni hulka zao, sina tabia hiyo na sanaa nimeianzia kwenye vikundi .”


UPENDO MUSHI ‘PENDO’
“Kauli ya Dude siyo ya kweli kama wapo ni  baadhi na siyo wote, sijaingia kwenye sanaa kwa rushwa ya ngono na sina tabia hizo, sijaipenda kauli yake.”


BABY MADAHA
“Siyo kweli kwamba sisi ni machangudoa . Wasanii wa kike wenye tabia hizo wanatoka katika maisha duni na wale wanaolipwa malipo duni kwenye filamu lakini wengine tumetokea kwenye familia   za hadhi na tunaishi kwa kufuata maadili.”


HALIMA YAHAYA ‘DAVINA’
“Sijaipenda kauli ya Dude, ametukosea sana ingawa watu wengi wanaona tasnia hii ni kama  ya kihuni lakini siyo wote wenye tabia hizo za kihuni, wengine tunajiheshimu na tuna familia zetu tunaithamini sanaa  tunaichukulia kama kazi.”


SNURA MUSHI
“Dude ameongea uongo, binafsi siko hivyo na sina maisha ya kuzurura, starehe na pombe na sitarajii kuwa na maisha hayo, ili heshima yake iendelee, angetuomba radhi na kuifuta kauli yake.”


MIRIAMU JOLWA ‘JINI KABULA’
“Huo ni mtazamo wa Dude, wasanii wa kike tunatakiwa kumuombea kwa Mungu ili ampe akili za kuweza kuzungumza vitu vya maana na siyo hivyo vya kutushushia heshima kwenye jamii.”  



 Chanzo:Global publisher


Posted By Unknown20:50

LULU AKESHA AKIMWOMBA MUNGU ILI KESI YAKE IENDE VIZURI

Filled under:


STAA wa Filamu za kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hivi sasa anakesha akiomba ili mambo yaende vizuri katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, Ijumaa lina maelezo yake ya kutosha.

Lulu amemwambia paparazi wetu kuwa alishaanza kuyasahau matatizo hayo lakini hataweza kupingana na amri ya mahakama iliyopanga kuanza kusikiliza kesi hiyo kuanzia Februari 17, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar.

“Lazima kesi iendelee na sheria ichukue mkondo wake, pamoja na kwamba nimekaa uraiani kwa kipindi kirefu na kuanza kusahau mambo hayo,” alisema Lulu.

Alipoulizwa anachokitegemea katika kesi hiyo, msanii huyo alidai kwamba hana cha kukitegemea zaidi  ya kukesha akimuomba Mungu.

“Nakesha nikiomba, namwamini Mungu atanisaidia kama alivyosikia kilio changu cha kuomba dhamana,”aliongeza.

Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia aliyepata kuwa msanii nguli katika tasnia ya filamu za Kibongo, Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

Aidha, baada ya kuachana na Lulu, Ijumaa lilizungumza na mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa juu ya kutajwa kwa kesi hiyo na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
 
Ijumaa: Unajisikiaje kuona Lulu akipandishwa kizimbani tena?
Mama Kanumba: Mmmh! Kwa kweli najisikia vibaya sana jamani.
Ijumaa: Unajisikia vibaya  kwa kuwa Lulu anapandishwa kizimbani au...?
Mama Kanumba: Pamoja na hilo lakini kesi hii inanikumbusha machungu ya mwanangu, naona mambo ndiyo yamefufuka upya wakati nilishaanza kuyasahau.
Ijumaa: Unasemaje kuhusu kushtakiwa kwa Lulu?
Mama Kanumba: Binafsi sijamshitaki Lulu ni serikali ndiyo iliyofanya hivyo, tuache sheria ichukue mkondo wake.
Chanzo:Global Publisher

Posted By Unknown05:43

Wednesday, 12 February 2014

WEMA AAPA HATA IWEJE LAZIMA DIAMOND ANIOE

Filled under:


Licha ya mama yake mzazi kupinga kwa nguvu zote, staa wa filamu nchini na mtangazaji wa Kipindi cha Runinga cha In My Shoes, Wema Sepetu ameapa kwamba hata iweje, lazima msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’ awe mume wake, Amani lina stori kamili.

NI CHAGUO LAKE
Akizungumza na Amani katika spesho intavyu hivi karibuni, Wema ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Diamond alifunguka kuwa, amepita kwa wanaume wengi ila anaamini mwanaume huyo ndiye chaguo lake.
Alisema katika uchunguzi wake aligundua kwamba Diamond anampenda kupita maelezo na kwa mapenzi anayomuonesha hana sababu ya kugoma kumpa nafasi ya kuwa mkewe.

“Kwa kifupi nampenda Diamond na yeye ananipenda, that’s it,” alisema Wema.
MKWARA WA MAMA YAKE
Kuhusu mama yake kuchimba ‘biti’ kuwa hamtaki Diamond na kamwe hawezi kukubali mwanaye aolewe na mwanaume huyo, Wema alisema:
“Unajua yule ni mzazi, wakati mwingine si mbaya kuonesha hisia zake lakini nitamseti na naamini kwa kuwa ananipenda atakubaliana na mawazo yangu.”
NDOA LINI?
Alipobanwa kuhusu lini watafunga ndoa kwani wamekaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wakiachana na kurudiana, Wema alionekana kutokuwa na jibu la moja kwa moja ila akaishia kusema kuwa, siku ikifika kila kitu kitakuwa wazi.

NUKUU YA MAMA WEMA!
Katika sakata hilo, kwa upande wake mama Wema alikuwa na haya ya kusema: “Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani, tena wakiwa na ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond.
“Sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga  mkononi, watakiona cha moto.”
 Wema na Diamond katika pozi la kimahaba.
“Yaani watu watasema sana lakini piga, ua, garagaza, lazima Diamond anioe. Amekuwa akilizungumzia hilo na kuonesha kuwa yuko ‘siriasi’ hivyo ipo siku historia itaandikwa bila kujali nani atasema nini.
“Unajua mimi ni mtu ninayejitambua na ninayejali maisha yangu hivyo ninapobaini mwanaume f’lani anaonesha kunijali na kunipa mapenzi ninayoyahitaji, kwa nini nisikubali kuingia naye kwenye maisha ya ndoa…? TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar, Diamond aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wema na ikadaiwa kuwa siku nyingi wangeingia katika maisha ya ndoa lakini haukupita muda mrefu wakaachana.
Baada ya kumwagana, Diamond alikwenda kwa mtangazaji wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema alihamishia penzi kwa yule kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Clement ‘CK’ kabla ya kumwagana hivi karibuni.
CHANZO:GLOBAL PUPLISHER

Posted By Unknown21:30

NABII WA KANISA LA EPHATA MWINGIRA AGOMA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI

Filled under:


MTUME na Nabii wa Kanisa la Efatha, Joseph Elias Mwingira anayekabiliwa na kesi ya kuzaa na mke wa mtu, hatimaye amefunguka mengi kuhusu madai hayo lakini amekataa kabisa kupima Ukimwi.

Uchunguzi uliofanywa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi - Kisutu, Dar, umebaini kuwa Mwingira aliye na kesi mahakamani hapo yenye namba 306 ya 2013, iliyofunguliwa na mlalamikaji Dk. Morris William, amejibu tuhuma zinazomkabili kwa njia ya maandishi.

Majibu hayo yameandaliwa na Kampuni ya Uwakili ya Legal Link, ambapo nakala yake imefikishwa kwa wakili wa mlalamikaji Dk. William, Januari 22, mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, madai yaliyopo katika jalada la kesi hiyo, mlalamikaji Dk. William, ameomba mahakama ikubali Nabii Mwingira apimwe Ukimwi na kipimo cha utambuzi wa vinasaba ‘DNA’.
Nabii huyo amepinga vikali ombi hilo, akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo (la madai ya kifedha).

MADAI YA MAPENZI
Katika majibu hayo (nakala tunayo), Mwingira amekanusha kufanya mapenzi na mlalamikiwa namba mbili, Dk. Phillis Nyambi ambaye ni mke wa mlalamikaji.
“Mlalamikiwa namba moja amefafanua kuwa hakuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mlalamikiwa wa pili,” imeeleza kampuni inayomtetea Mwingira.

AKANA KUBAKA
Nabii huyo pia amekanusha madai ya kumbaka mlalamikiwa wa pili kama alivyosema mlalamikaji katika hati yake ya malalamiko iliyopo mahakamani hapo.

Nabii Mwingira pia amekana madai ya kuzaa na mlalamikiwa namba mbili na kuwepo kwa matatizo ya kitabibu kwa mama huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miaka mitano, akasema mlalamikaji anatakiwa kuthibitisha.

Kuhusu madai ya Dk. Phillis kushiriki kimapenzi na Mwingira hivyo kusaliti ndoa halali na kumharibia furaha ya maisha mlalamikaji, nabii huyo amesema hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke huyo.

Kuhusu madai ya Mwingira kutembea na mke wa mlalamikaji na habari hizo kuandikwa magazetini na kwenye mitandao ya kijamii hivyo kumdhalilisha na kumshushia hadhi, amedai kuwa yeye hahusiki na hilo na atahitaji kuthibitisha.

Madai mengine ya mlalamikaji kwamba vitendo vya walalamikiwa namba moja na namba mbili vya kujihusisha kimapenzi vimemuathiri Dk. Morris kisaikolojia na kiuchumi na kumfanya apoteze biashara zake za kimataifa kwa kukosa wadhamini katika NGO yake, Mwingira amesema kama yametokea hakuyasababisha yeye.

Ameiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo na kumuamuru mlalamikaji kulipa gharama za kesi hiyo, hivyo ameweka pingamizi la awali.
CHANZO:GLABAL PUBLISHER

Posted By Unknown09:16