BAADA ya kupata matokeo mabaya kidato cha nne, kinda wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ amesema anatarajia
kusoma chuo cha muziki ili kukuza kipaji chake.
Akizungumzia
matokeo hayo, Aslay alisema hajasikitika sana kupata matokeo hayo na
wala hajakata tamaa ya kuendelea kusoma, kwani anataka kusomea muziki
kwa lengo la kuongeza ‘mautundu’ katika kazi zake.
“Nimepata 4 ya pointi 32, kwa sababu nilikuwa nachanganya muziki na
masomo, hivyo sijayachukia sana matokeo hayo na kwa kuwa muziki ndio
kitu ninachokipenda, nataka kusoma chuo cha muziki na si kupoteza muda
kuanza ‘kurisiti’, bado sijajua nitakwenda chuo gani kwa ajili ya masomo
hayo,” alisema.
“Wengi wamekuwa wakinisema kwamba napoteza muda mwingi kwa kufanya
muziki na kusahau masomo, ndiyo maana nafeli, mwisho wa siku ukweli
unabaki pale pale napenda muziki ndiyo maana nafanya vizuri na ndiyo
maana nataka nikaongeze elimu katika muziki wangu,” alisema Aslay.
Dogo Aslay ni kati ya wasanii wenye umri mdogo ambao wanafanya vizuri
katika muziki huo, huku akitambulishwa na ngoma yake ambayo ilibamba
vilivyo ‘Naenda Kusema kwa Mama’.
0 comments:
Post a Comment