Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana
wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo
hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini
wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na
saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444
wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana
wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza
wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika
kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa
sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi
wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe
wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi
hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau
wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana
kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani
ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume
nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo
huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24
zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya
watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na
wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini
siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya
wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini
mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze
kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili
hii haikuwepo kabisa,” anasema Dk Kahesa na kuongeza.
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Visababishi vya kansa ya koo:
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila
kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya
kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya
hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna
usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa
saratani nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila
sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu
wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza
nchini saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi
wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na
kuendelea hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza ngono ya mdomo muda
mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya
koo; aina ya kwanza ni “Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma,
zote hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu
yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema
kuharibu seli ambazo zipo katika utandu uliopo katika ukuta wa koo
kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni
mwenendo wa maisha yetu kwa kula vyakula vyenye asidi, vyakula
vichachu, vyakula vyenye pilipili, pombe kali na vyakula vigumu ambavyo
hukwaruza koo na hivyo kusababisha saratani.
Anasema asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road wanakuwa na historia ya
kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula
pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.
Dalili za saratani ya koo
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Tafiti zilizofanywa nchini
Magonjwa mengine sehemu za siri
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
NINI KIFANYIKE:
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni
chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa
kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza
hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na
kuona viashiria kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza
chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya
Saratani wanakuwa tayari wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya
mwisho.
“Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku
zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi
hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika
kifua na mgongo na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu
kinachoweza kudumu mwezi mmoja,” anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi
hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa
anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye
amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo
vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo
kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji,
kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti
zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992
kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116
waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu wenye umri wa
miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa
miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo
unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba
iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167
hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana
na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi
zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye
ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha,
ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu
wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea
katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa
kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana
na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati
ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa
huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue
maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
Hepatitis A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana
katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda
kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu
mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi
vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka
katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake
unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo
wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa
ambao hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa
katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa
kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi
vya Ukimwi kwa uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya
kondom ambazo huvaliwa katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza
hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja
unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo
wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
“Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa
baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu
wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili
kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi
zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao
huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam domo”anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia
wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti
na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke
kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za
wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili
hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya
mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu
huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina
madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya
mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.
0 comments:
Post a Comment