PAMOJA na serikali kutotaja majina ya watu 40 ambao Rais Jakaya
Kikwete alisema ndio mtandao wa ujangili nchini, akiwemo tajiri maarufu
mkoani Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
amesisitiza kuwa orodha hiyo si ya kutengeneza na kwamba itawekwa
hadharani muda wowote.
Alisema kuwa wanayo majina zaidi ya 320 ya watu wanaojihusisha na
ujangili na kuonya wahusika kuachana na biashara hiyo huku akitamba kuwa
serikali ina mkono mrefu.
Waziri Nyalandu alitoa msimamo huo jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari wizarani kwake kueleza juhudi za serikali katika
kukabiliana na ujangili nchini.
0 comments:
Post a Comment