Zifuatazo ni njia za kuosha miguu
Chukua mchanganyiko wa maji ya uvuguvugu na chumvi, unapoanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwakusugua hakikisha mabaki ya ngozi yanaisha katika miguu yako
Weka mchanganyiko wa maji pamoja na asali, ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.
Futa miguu yako kwa kitambaa safi kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya wazi kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi.
Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto inayokuwepo ndani ya soksi.
Ongeza kiwango cha kunywa maji, kila siku jitahidi kunywa angalau lita moja ya maji ambayo husadia ngozi yako kuendelea kuwa nyororo.
0 comments:
Post a Comment