Tuesday, 25 February 2014

RAIA WA UGIRIKI ATUHUMIWA BAADA YA KUKUTWA NA UNGA

Filled under:

 


Raia  wa Ugiriki, Alexandria Athanasios (30), amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na kilo 5.3 za dawa za kulevya aina ya heroine katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba raia huyo wa kigeni alikamatwa juzi saa 3:00 usiku uwanjani hapo.

Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa, akifafanua zaidi tukio hilo alisema Athanasios alikamatwa wakati akijiandaa kusafiri na ndege ya shirika la Swiss Air kutoka Dar es Salaam kwenda Ugiriki kupitia Zurich.

Alisema mtu huyo alikamatwa na maofisa wa uwanja huo kwa kushirikiana na polisi wakati akikaguliwa mizigo yake.

Kamanda Nzowa alisema mtu huyo anaendelea kushikiliwa na polisi na kwamba uchunguzi wa kujua dawa hizo zina thamani gani unaendelea kufanyika na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kukamatwa kwa dawa hizo kumekuja wiki tatu ndani ya mwezi huu tangu raia 12 wa Pakistan na Iran walipokamatwa na shehena ya dawa za kulevya zaidi ya kilo 201 katikati ya Dar es Salaam na Zanzibar katika Bahari ya Hindi.

Kukamatwa kwa kiasi hicho kikubwa cha dawa kulizua taharuku kubwa katika Jiji la Dar es Salaam na kusababisha wananchi kulazimika kukimbilia katika Bandari ya Dar es Salaam kushuhudia tukio hilo.

Watu hao walikamatwa wakiwa katika jahazi ijulikanayo Aldanial iliyotokea nchini Iran mali ya Raisee, raia wa Iran.

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Muhamad Hassan (30), Abdul Nabii (30), Fahir Muhamad (34) na Rahim Baksh (30), wote raia wa Pakistan.

Raia wa Iran waliokamatwa ni Abdulsamed Badreuse (47), Ayoub Hot (50), nahodha wa jahazi hilo, Hazra Azat (60), Nahim Mussa (35), Khalid Ally (35), Kher Muhamad (75), Said Muhamad (34) na Murad Gwaharam (38).
 

Posted By Unknown11:26

BOKO HARAM KUSHAMBULIA SHULE NA KUUA WANAFUNZI

Filled under:



Wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wametuhumiwa kushambulia shule moja na kuwaua wanafunzi kadhaa.

Polisi nchini Nigeria wameliambia Shirika la Habari la Uingereza, Reuters kwamba wote waliouawa ni wavulana na kwamba baadhi ya miili ya wanafunzi hao imeungua na kubaki majivu.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema shambulio hilo limefanyika katika jimbo la Yobe.

Wakaazi wa mji wa Buni Yadi katika jimbo hilo, wamesema washambuliaji hao walivamia usiku na kuwachinja baadhi ya wanafunzi.

Wamesema baadhi waliuawa kwa kupigwa risasi.
Walimu katika chuo cha serikali ya shirikisho katika mji wa Buni Yadi wameliambia shirika la habari la AP kwamba wanafunzi wapatao 40 waliuawa katika shambulio hilo ambalo lilianza mapema Jumanne asubuhi.

Jeshi limethibitisha kwamba shambulio hilo limetokea katika hosteli za wanafunzi lakini limesema haliwezi kutoa taarifa zaidi kwa sasa.
Kundi la Boko Haram limekuwa likishutumiwa kuendesha vitendo vya mauaji kaskazini mwa Nigeria, yakiwemo mauaji ya mapema mwezi huu katika jimbo la Yobe.
Boko Haram, lina maana ya"Elimu ya Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, mara kwa mara limekuwa likishambulia shule katika siku za nyuma.
Watu kadhaa wameuawa katika mashambulio mawili yaliyotokea wiki iliyopita. Katika tukio moja, wanamgambo hao wa Boko Haram, waliteketeza kijiji kizima na kuwapiga risasi wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakijaribu kutoroka.

Posted By Unknown11:02

Monday, 24 February 2014

MUSEVENI:MAPENZI YA JINSIA MOJA MARUFUKU UGANDA

Filled under:

 Moses mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja atafuta hifadhi nchini Marekan

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa habari.

Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana na hatia ya kuhusika na mapenzi ya jinsia moja.
Mswada huo pia umeharamisha wanaharakati kutangaza misimamo yao hadharani kuhusu au kuwasaidia wanapenzi wengine wa jisnai moja kujitangaza hadharani.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi katika mapenzi ya jinsia moja.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.

Uganda imepuuzilia mbali shinikio za Marekani na nchi zengine za Magharibi kutopitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Mswada huo umeweka sheria kali zaidi dhidi ya uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kwa yeyote atakayepatikana akishiriki.
Usagaji pia umeharamishwa kwa mara ya kwanza na pia ni hatia kumsaidia mtu kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema wanajiandaa kwenda mahakamani kupinga sheria hiyo mpya.
Uganda ni miongoni mwa mataifa 30 Afrika ambayo yameharamisha mapenzi ya jinsia moja. Ni wiki jana tu ambapo Rais wa Gambia Yahyah Jammeh aliyesema mapenzi ya jinsia moja ni sumu kali mno.

Posted By Unknown20:36

WAZIRI NYALANDU ATANGAZA KUWANG'OA VIGOGO KATIKA IDARA YA WANYAMAPORI

Filled under:



Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo ametangaza kuwang'oa viongogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao. Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu,  kama alivyolisoma leo na theNkoromo Blog kupata nakala ya tamko hilo

Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo:

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.

Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.

Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.

Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti.

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara.  Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.

 
Mungu ibariki Tanzania.

Asante.
 
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii

Posted By Unknown20:20

FACEBOOK YATANGAZA DAU YA KUINUNUA WHATSAPP

Filled under:


Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.

Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.

WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

Posted By Unknown10:28

FAHAMU MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOJIANDAA KUFUNGA NDOA

Filled under:



BIBLIA inaonyesha kwamba Ye- hova Mungu—anayewajua wana- damu vizuri kuliko mtu mwingi- ne yeyote—ndiye aliyefunganisha watu wawili wa kwanza katika ndoa. Alikusudia ndoa iwe msingi wa jamii ya wanadamu. (Mwanzo 2:18-24) Na katika Neno la Mungu, Biblia, kuna kanuni mbalimbali zinazoweza kutuongoza tunapopanga arusi.

Kwa mfano, Yesu alisema kwamba Wakristo wanapaswa ‘kumlipa Kaisari vitu vya Kaisari.’ (Mathayo 22:21) Kwa hiyo, wanapaswa kutii sheria ya nchi yao. Ndoa iliyohalalishwa inalinda haki za wale waliohusika, kama vile kuonyesha madaraka yanayohusu watoto (kutia ndani kuwaruzuku na kuwaelimisha) na haki za urithi. Hali kadhalika, kuna sheria zinazowalinda watu wasitendewe au wasitumiwe vibaya na wengine katika familia.

Matayarisho
Watu wawili walioamua kufunga ndoa kulingana na sheria na kanuni za Biblia na vilevile sheria ya nchi, wanapaswa kufikiria mambo gani? Baadhi ya mambo yanayopasa kufikiriwa ni tarehe na sherehe ya arusi.

Kitabu kimoja kuhusu arusi kinasema: “Huenda maoni ya maarusi yasipatane na maoni ya wazazi wao na huenda wakasitasita kati ya kufuata mapendezi yao wenyewe au kufuata desturi za jamaa.” Suluhisho ni nini? “Hakuna suluhisho rahisi, bali ni muhimu kusikiliza wengine kwa busara, kuzungumzia matatizo, na kukubaliana. Watu huwa na hisia mbalimbali wakati kama huo, kwa hiyo kutumia busara na kuwafikiria wengine hurahisisha sana matayarisho.”—The Complete Wedding Organiser and Record.

Ijapokuwa wazazi wenye upendo wanaweza kuchangia sana shangwe ya siku ya arusi, wanapaswa kujihadhari wasiwalazimishe watoto wao kufuata mapendezi yao. Kwa upande mwingine, ijapokuwa maarusi ndio watakaofanya maamuzi ya mwisho, bado kuna faida kusikiliza ushauri unaofaa. Maarusi wanapoamua ni mapendekezo gani watakayofuata, inafaa wakumbuke ushauri huu wa Biblia: “Mambo yote yaruhusika kisheria; lakini si mambo yote yenye faida. Mambo yote yaruhusika kisheria; lakini si mambo yote yajengayo. Acheni kila mmoja afulize kutafuta sana, si faida yake mwenyewe, bali ya mtu yule mwingine.”—1 Wakorintho 10:23, 24.

Matayarisho yanahusisha mambo kama vile kutuma kadi za mwaliko na kupanga karamu. Katika kitabu chake Marriage for Moderns H. Bowman anasema hivi: “Matayarisho yakipangwa vizuri, kwa busara na kwa utaratibu, uchovu na mfadhaiko hautakuwa mwingi.” Anaonya hivi: “Hata kama matayarisho ni mazuri, bado watu watachoka kadiri fulani na ni jambo la busara kujitahidi iwezekanavyo kupunguza uchovu huo.”

Kutakuwa na kazi mbalimbali na ni lazima wageni washughulikiwe. Je, familia na marafiki wanaweza kusaidia? Je, maarusi wangeweza kuwaomba wengine wanaotegemeka wawasaidie na kazi mbalimbali ambazo si lazima wao wenyewe wafanye?

Gharama
Gharama zinapasa kukadiriwa kwa hekima. Si jambo la busara wala la upendo kutarajia maarusi au wazazi wao wajiingize katika deni ili kulipia gharama kubwa ya arusi. Wengi wanaoweza kufanya arusi kubwa wameamua kufanya arusi ya kiasi. Vyovyote vile, maarusi fulani wameona kuna faida kuandika orodha ya gharama iliyokadiriwa na orodha ya kiasi kilicholipwa. Pia, linaweza kuwa jambo zuri kuandika orodha ya tarehe ambazo shughuli mbalimbali zinapasa kuwa zimetekelezwa. Kujaribu kukumbuka mambo yote bila kuandika kunaweza kuleta wasiwasi.

Je, Harusi itagharimu kiasi gani? Bei zinatofautiana mahali-mahali, lakini uwe unaishi wapi, ni jambo la hekima kujiuliza: ‘Je, tunaweza kulipa mambo yote ambayo tumepanga? Je, mambo hayo ni ya lazima?’ Tina, aliyeolewa karibuni, alisema hivi: “Mambo mengine yalionekana kuwa ‘ya lazima’ tulipopanga arusi, lakini baadaye tuliona kwamba hayakuwa ya lazima hata kidogo.” Fikiria ushauri huu wa Yesu: “Ni nani kati yenu atakaye kujenga mnara asiyeketi kwanza na kupiga hesabu ya gharama, ili aone kama ana kiasi cha kutosha kuukamilisha?” (Luka 14:28) Ikiwa huwezi kulipa mambo yote unayotaka, acha mengine. Hata kama una uwezo wa kufanya arusi kubwa, huenda ukaamua kufanya arusi ya kiasi.

Kiasi ambacho bibi-arusi huko Italia anakadiriwa kutumia kwa ajili ya arusi yake kilionyeshwa kwenye maonyesho ya bidhaa za Harusi. Kupaka vipodozi na kutengeneza nywele, dola 450 za Marekani; kukodi gari la anasa, dola 300; kupiga picha ya video ya siku ya arusi, dola 600; kitabu cha kuwekea picha za arusi (bila picha), dola 125-500; maua, kuanzia dola 600; karamu, dola 45-90 kwa kila mtu; nguo ya arusi, kufikia dola 1,200. Kwa kuwa siku hiyo ni muhimu sana, si ajabu kwamba watu wanataka kuifanya iwe ya kipekee. Lakini hata uwe umeamua nini, mambo yote yanapasa kufanywa kwa busara.

Ijapokuwa baadhi ya watu hutumia fedha nyingi sana, wengine hufurahia kufanya arusi ya kiasi—au, hufanya hivyo kwa sababu hawana namna nyingine. Bibi-arusi mmoja alisema: “Tulikuwa mapainia [wahubiri wa wakati wote], nasi hatukuwa na fedha zozote, lakini hilo halikutusumbua. Mama-mkwe wangu alinunua kitambaa, na rafiki mmoja alinishonea nguo ya arusi. Mume wangu aliandika kadi za mwaliko kwa mkono, na rafiki Mkristo alituazima gari. Tulinunua vitu vilivyokuwa vya lazima kwa ajili ya karamu, na mtu fulani alitupatia divai. Arusi yetu haikuwa yenye mambo mengi lakini ilikuwa nzuri.” Bwana-arusi mmoja alisema kwamba familia na marafiki wanaposaidia, “gharama hupunguka sana.”

Hata hali yao ya uchumi iweje, wenzi wa ndoa Wakristo hujaribu kuepuka kupita kiasi, mtindo wa ulimwengu, au kujionyesha. (1 Yohana 2:15-17) Siku ya arusi inapasa kuwa ya shangwe. Ingehuzunisha kama nini, ikiwa mtu fulani angeshindwa kufuata kanuni za Maandiko zinazoonya kuhusu ulafi, ulevi; au, jambo jingine linaloweza kufanya ashindwe kuwa “asiyelaumika”!—Mithali 23:20, 21; 1 Timotheo 3:2.

Epuka mwelekeo wa kutaka kufanya arusi kubwa na bora kushinda arusi nyingine. Fikiria shela kubwa za bibi-arusi wawili katika nchi moja—shela moja ilikuwa na kipenyo cha meta 13 na uzito wa kilogramu 220; ile nyingine ilikuwa na urefu wa meta 300 na wasindikizaji 100 waliibeba. Je, kuiga majivuno kama hayo kungepatana na ushauri wa Biblia?—Wafilipi 4:5.

Je, Mila Zifuatwe?
Desturi za arusi hutofautiana katika nchi mbalimbali, kwa hiyo haiwezekani kuzungumzia zote. Maarusi wanapofanya uamuzi kuhusiana na desturi fulani, ingefaa wajiulize maswali haya: ‘Maana ya desturi hiyo ni nini? Je, inatokana na ushirikina wa kutakia mtu bahati nzuri au uwezo wa kuzaa—kama vile kuwarushia maarusi mchele? Je, inahusiana na dini ya uwongo au mazoea mengine yanayokatazwa katika Biblia? Je, inapita kiasi au inakosa upendo? Je, inaweza kuwaaibisha au kuwakwaza wengine? Je, ingetilia shaka madhumuni ya maarusi? Je, inaudhi?’ Ikiwa kuna shaka lolote kuhusiana na mambo hayo, ni heri kuepuka desturi hiyo inayotiliwa shaka na kuwajulisha wageni uamuzi huo.

Shangwe na Hisia za Moyoni
Katika siku ya arusi watu wanaweza kuwa na shangwe kuu au huzuni. Bibi-arusi mmoja alisema hivi: “Nilifurahi sana kwa kuwa matamanio yangu yote yalitimizwa.” Lakini bwana-arusi fulani anasema: “Ilikuwa siku mbaya na siku nzuri kupita zote maishani mwangu. Wakwe wangu walibubujika machozi kwa sababu nilichukua binti yao wa kwanza, na mke wangu alilia kwa sababu wazazi wake walilia, na mwishowe, hata mimi nililia kwa sababu sikuweza kuvumilia hayo yote.”

Usiwe na wasiwasi iwapo hali kama hizo zitatokea—hizo husababishwa na mfadhaiko. Wala haipasi kushangaza kwamba uhusiano kati ya watu wa familia, au hata kati ya maarusi, huathiriwa nyakati nyingine. Kitabu cha The Complete Wedding Organiser and Record kinasema: “Labda hiyo ni mara yao ya kwanza kupanga tukio kuu pamoja, na bila shaka hekaheka itaathiri uhusiano wao kwa njia moja au nyingine. Hakuna haja kuudhika ikiwa mambo hayatakuwa shwari; ni afadhali kuomba ushauri na msaada.”

Bwana-arusi mmoja alisema: ‘Ningalithamini sana kuwa na mtu wa kunishauri ambaye ningaliweza kumtumaini na kumweleza hisia zangu za moyoni.’ Mshauri mzuri ni rafiki mkomavu au mtu wa ukoo mkomavu, au mtu mwingine mwenye ujuzi katika kutaniko la Kikristo.

Wazazi wataona fahari na shangwe mtoto wao anapoondoka nyumbani, lakini huenda pia wakahisi wasiwasi. Hata hivyo, wanapaswa kutambua kwamba wakati umewadia kwa mtoto wao ‘kumwacha baba yake na mama yake,’ naye ataambatana na mwenzi wake, na hao wawili “watakuwa mwili mmoja,” kama vile Muumba alivyokusudia. (Mwanzo 2:24) Mama mmoja anaeleza jinsi alivyohisi wakati mwana wake wa kwanza alipooa: “Nililia machozi, lakini machozi yangu hayakuwa ya huzuni tu bali pia ya furaha kwa sababu nilipata binti mpendwa, yaani, mke wa mwanangu.”

Ili siku ya arusi iwe ya kupendeza na kujenga, ni lazima wazazi—na vilevile maarusi—waonyeshe sifa za Kikristo za ushirikiano, utulivu, uvumilivu, na kuwafikiria wengine.—1 Wakorintho 13:4-8; Wagalatia 5:22-24; Wafilipi 2:2-4.

Baadhi ya bibi-arusi wana wasiwasi mwingi sana kwamba mambo yatakwenda kombo katika siku yao ya arusi. Wanahofu kwamba gurudumu la gari litaishiwa pumzi na watachelewa, hali ya hewa itakuwa mbaya sana, au nguo ya arusi itaharibika kabisa dakika ya mwisho. Yaelekea mambo hayo hayatatukia. Hata hivyo, kumbuka kwamba mipango yote haiwezi kufanikiwa kikamili. Vikwazo vitakuwapo. (Mhubiri 9:11) Uwe na mtazamo unaofaa, na jambo fulani likienda kombo, usife moyo. Kumbuka kwamba, baada ya miaka mingi huenda ukacheka ukilisimulia. Usiruhusu hitilafu ndogo ziharibu shangwe ya arusi.

Sheria katika nchi mbalimbali inakataza ndoa ya wake au waume wengi, kufanya ngono na maharimu, ulaghai, ujeuri katika ndoa, na ndoa ya vijana ambao hawajafikia umri wa kisheria wa kufunga ndoa.
ORODHA YA MATAYARISHO
Miezi 6 au zaidi kabla ya arusi
❑ Zungumzia mipango pamoja na yule unayetaka kufunga ndoa naye, wakwe, na wazazi
❑ Amua aina ya arusi mnayotaka
❑ Hesabu gharama
❑ Chunguza matakwa ya kisheria
❑ Weka nafasi mapema ya mahali pa karamu
❑ Fanya mpango kuwe na mpiga picha
Miezi 4
❑ Chagua (kati ya nguo ulizo nazo), ununue, au ushoneshe nguo za arusi
❑ Agiza maua
❑ Chagua na agiza kadi za mwaliko
Miezi 2
❑ Tuma kadi za mwaliko
❑ Nunua pete
❑ Tafuta vyeti vinavyohitajika
Mwezi 1
❑ Vaa nguo za arusi ili kuhakikisha zinafaa
❑ Hakikisha kwamba miadi na maagizo yataweza kutekelezwa
❑ Andika barua ili kushukuru kwa ajili ya zawadi ambazo mmepokea tayari
Majuma 2
❑ Anza kuvipeleka vitu vyako kwenye makazi mapya
Juma 1
❑ Hakikisha kwamba wasaidizi wote wanaelewa wajibu wao
❑ Panga jinsi vitu vyote vilivyoazimwa na kukodiwa vitakavyorudishwa
❑ Omba wengine wasaidie na kazi nyingi iwezekanavyo

SOURCE:

Posted By Unknown09:59

MSANII ALIYEMPONDA DIAMOND ATISHIWA MAISHA

Filled under:


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Masige Bukori ‘Cado Baro’, amesema anazidi kutishiwa maisha kwa kupigiwa simu mara kwa mara, zikimtaka asiende kwenye ukumbi wowote kutumbuiza nyimbo zake.

Cado Baro alisema amekuwa akipigiwa simu za vitisho kila anapopata mwaliko wa kwenda kufanya onesho katika mikoa mbalimbali nchini, zikimtaka asithubutu kwenda, kwani maisha yake yatakuwa hatarini.

Alisema kuwa tangu atoe ‘remix’ ya wimbo wa Diamond ‘My Number One’ ile inayomtaka msanii huyo aache wizi, ndipo alipoanza kupigiwa simu za vitisho na mtu asiyemfahamu kila anapoitwa kufanya onesho katika matamasha mbalimbali.

Posted By Unknown09:39