Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema
kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa
kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni
tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi
wake.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.
0 comments:
Post a Comment