Saturday, 1 March 2014

OXFORD BROOKES UNIVERSITY FOR INTERNATIONAL STUDENT IN UK 2014

Filled under:


Oxford Brookes University is offering three international foundation scholarships. Scholarships of £1000 each are available for international four year foundation programmes. Applicants must have received and accepted an offer on the International Foundation Business and Technology or the International Foundation Arts, Humanities and Law starting in September 2014. Awards will automatically be deducted from the tuition fees. The application deadline is 30 June 2014.
Study Subject (s): Scholarships are awarded for International Foundation Business and Technology or the International Foundation Arts, Humanities and Law programme. Course Level: Scholarships are available for pursuing foundation programmes at Oxford Brookes University. Scholarship Provider: Oxford Brookes University, UK Scholarship can be taken at: UK
Eligibility: To be eligible for the scholarship you will need to have received and accepted an offer on the International Foundation Business and Technology or the International Foundation Arts, Humanities and Law starting in September 2014
Scholarship Open for International Students: International students can apply for these foundation scholarships.
Scholarship Description: Three scholarships of £1000 each are available for international four year foundation programmes. These include a foundation as an integral part of a degree programme so you only need to make one application. To be eligible for the scholarship you will need to have received and accepted an offer on either the International Foundation Business and Technology or the International Foundation Arts, Humanities and Law starting in September 2014 by 30 June 2014.
Number of award(s): Three foundation scholarships will be awarded.
Duration of award(s): These foundation scholarships will be offered for four years.
What does it cover? Three scholarships of £1000 each are available for international four year foundation programmes. Awards will automatically be deducted your tuition fees. There is no contribution to living expenses.
Selection Criteria: The scholarships are awarded based on assessment of your academic potential. The university will take into account your personal statement, references and previous qualifications (academic and English language).
Notification: Successful applicants will be notified by 14 July. If you do not hear, it means you have not been successful.
How to Apply: No additional application is required.
Scholarship Application Deadline: The application deadline is 30 June 2014.

Posted By Unknown10:38

FID Q:MBALI NA MZIKI NAJIHUSISHA NA MADINI

Filled under:



Kati ya mamia ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu Tanzania, ni mwanamuziki mmoja pekee aliyehudhuria katika Tamasha la Sauti za Busara 2014, lililotajwa na Kituo cha Utangazaji cha CNN kuwa ni tamasha lenye nguvu barani Afrika.
Huyu siyo mwingine bali ni Fareed Kubanda (Fid Q), aliyekuwapo mjini Zanzibar kwa siku mbili kushuhudia tamasha hilo lililokuwa la siku nne, lililofanyika katika wiki ya pili ya Februari mwaka huu, Viwanja vya Ngome Kongwe visiwani humo.
Ikumbukwe kuwa Fid Q alianza shughuli za muziki miaka ya 1990. Alitoa wimbo wake wa kwanza mwaka 2000 ulioitwa; Huyu na Yule, alioimba na Mr Paul. Wimbo huu ulirekodiwa na Prodyuza maarufu nchini,  Master Jay katika Studio za MJ Records na kumpa heshima kubwa msanii huyo.
Starehe ilifanya mahojiano na  Fid Q ambaye pamoja na mambo mengine aliweka wazi sababu za yeye kuwapo katika tamasha hilo, kilichomvutia huku akiweka wazi kuhusu biashara ya madini aliyodaiwa kuanza kuifanya mwishoni mwa mwaka jana.
Swali: Nini kimekuvutia ukaamua kuhudhuria katika tamasha hili?
Fid Q: Mimi ni mtu ninayependa kujifunza zaidi, nimeona hili ni tamasha kubwa na zuri kwangu kujifunza. Kubwa zaidi ni kutaka kujua wenzetu wanafanyaje muziki. Huwezi kukaa tu na kwenda kupiga muziki staili moja kila siku; ili ujue, ni vyema ukajifunza kutoka kwa watu unaowaamini.
Swali: Kupitia wanamuziki wa muziki wa asili kutoka mataifa mbalimbali katika Sauti za Busara, unadhani unaweza kupata uzoefu wa kutosha?
Fid Q: Wasanii wote wa mataifa mbalimbali waliofanikiwa hasa Nigeria, wamekuwa wakichukua vionjo kutoka katika muziki wa asili, kisha wakileta katika muziki wa kizazi kipya, inapatikana ladha ya kipekee, ndiyo maana leo unawaona kina P Square wanatamba, walianza kujifunza na kutumia vionjo kutoka katika muziki wa asili.
Swali: Unadhani nini kinachowafanya wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutohudhuria tamasha hili?
Fid Q: Hawapo tayari kujifunza. Mimi nimewahi kutumbuiza katika tamasha hili, ninajua. Huku hakuna ubabaishaji, msanii unatakiwa uimbe kwa sauti yako jukwaani, walio wengi hili hawaliwezi. Idadi kubwa ya wasanii wamezoea kuimba kwa ‘playback’, (kuweka cd ya ala), ndiyo maana hata waandaaji wanashindwa kuwaalika, muziki tunaofanya sisi ni ule wa wenzetu, lakini tunashindwa kuuwakilisha ipasavyo, tumezoea kuimba kwa ‘playback’.
Swali: Unadhani kuna umuhimu gani kwa wasanii kuimba ‘live’ (kwa sauti zao wenyewe pasipo kutegemea CD)?
Fid Q: Ina faida zake. Kwanza inakutangaza na pia unaonekana wewe ni msanii halisi. Haya ndiyo wanayohitaji kuyaona watu wanaoujua muziki, watu wanaohudhuria matamasha ya kimataifa ni wengi, hawawezi kusikiliza kitu walichokisikia kwao, wanapenda kusikia kitu kipya kitakachowateka
Swali: Unadhani ni kwa nini muziki wa asili unapendwa na wageni kuliko wazawa?
Fid Q: Tatizo ni kwamba Watanzania hawapendi wala kuuthamini utamaduni wao. Kinachosikitisha, tamasha kama hili kubwa Afrika, wamejaa wazungu, wanapenda utamaduni wao na hata wapo tayari kujifunza juu ya utamaduni wa watu wengine.
Swali: Kwa nini mwaka huu hukushiriki kwenye tamasha hili?
Fid Q: Waliniita na kutaka nishiriki, lakini sikuwa tayari na ratiba zangu na sikudhani kama nitapata muda, hivyo niliona ni vyema nikikaa pembeni baada ya kupata muda nikaona nije kushiriki tu kama mtazamaji.
Swali: Uliwahi kueleza kwamba unafanya biashara ya madini, tujuze biashara yako inaendeleaje?
Fid Q: Ha ha ha ha; mimi ni dalali tu kwenye ile biashara, mbali na kupata fedha. Ila nimeingia katika biashara ya madini ya Ruby ili kukuza kipato changu.  Unajua huwezi kufanya muziki peke yake, lazima muda mwingine ujikite katika biashara zitakazokuletea faida na kipato kikubwa ili uweze kufanya maendeleo zaidi katika maisha.
Swali: Nani hasa mhusika katika biashara hiyo?
Fid Q: Kwa bahati mbaya sitaweza kumtaja kutokana na makubaliano yetu, lakini ni mfanyabiashara mkubwa tu wa madini Arusha. Mimi nimeingia kati kama dalali, ni fursa kwangu na kwa kuwa nafahamiana na watu wengi ninaweza kufanya vizuri biashara hii.
Swali: Ni mafanikio gani uliyoyapata kupitia biashara hii?
Fid Q: Napata faida kubwa sana, ambayo imeniwezesha  kuanza kufanya mambo kadhaa ya kimaendeleo, ambayo sitakuwa tayari kuyaweka wazi kwa sasa, lakini mambo yakiwa mazuri na kukamilika kwa mipango yangu, wananchi watajua tu.
Swali: Mashabiki wako watarajie nini kutoka kwako?
Fid Q: Nipo ‘chimbo’ nikitayarisha kazi na Prodyuza P Funk, ambaye ni prodyuza wangu wa albamu yangu ya kwanza ‘Vina Mwanzo, Kati na Mwisho’.

Posted By Unknown10:01

TUMIA CHUMVI,ASALI NA MAJI YA UVUGUVUGU KUSAFISHA MIGUU ILI IWE NA MWONEKANO MZURI

Filled under:



Zifuatazo ni njia za kuosha miguu

Chukua mchanganyiko wa maji ya uvuguvugu na  chumvi, unapoanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwakusugua hakikisha mabaki ya ngozi yanaisha katika miguu yako

Weka mchanganyiko wa maji pamoja na asali, ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.

Futa miguu yako kwa kitambaa safi kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya wazi kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi.

Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto  inayokuwepo ndani ya soksi.

Ongeza kiwango cha kunywa maji, kila siku jitahidi kunywa angalau lita moja ya maji  ambayo husadia  ngozi yako kuendelea kuwa  nyororo.

Posted By Unknown06:15

WAZIRI ATOA SIKU 14 KUPATIKANA KWA MIILI YA WATOTO WALIOPOTEA

Filled under:



Waziri wa Afya wa Ghana Sherry Ayittey ametoa siku 14 kwa hospitali moja katika mji wa Kumasi kuonyesha miili ya watoto watano wanaodaiwa kufa baada ya kuzaliwa.

Watu saba wameshitakiwa kwa kuiba na kula njama ya kuiba mtoto kutoka hospitali ya chuo cha Komfo Anokye, mapema mwezi Februari.
Suwaiba Mumuni, ambaye mtoto wake ni miongoni mwa watoto watano waliopotea, ameiambia BBC kuwa anaamini mtoto wake yu angali hai.

Hospitali hiyo ya pili kwa ukubwa nchini Ghana, imekana tuhuma hizo.
Bi Mumuni amesema baada ya kujifungua tarehe 5 Februari, aliambiwa kuwa mtoto wake alikuwa amekufa na hivyo amechukuliwa na wahudumu kupelekwa chumba cha kuhifadhi maiti.

Amesema, ndugu zake walipofika hospitalini hapo kuchukua mwili wa mtoto, hawakuweza kuupata.
Miili ya watoto wengine wanne waliosemekana kuwa wamekufa siku hiyo, nayo pia haijapatikana.

Kutokana na matukio hayo, waziri wa Afya Sherry Ayittey amesema lazima ukweli ujulikane kuhusu tukio hilo.

Bi Ayittey amesema hospitali hiyo ameipa siku 14 za kazi kupata miili ya watoto hao, ili ikazikwe na familia zao.

Posted By Unknown04:35

MTUHUMIWA WA UGAIDI MOAZZAM BEGG AKAMATWA UINGEREZA

Filled under:

 
Moazzam Begg, mtuhumiwa wa ugaid
Mfungwa wa zamani katika gereza la Guantanamo Bay,Moazzam Begg na mwananmke mmoja mwenye umri wa miaka 44 wamefunguliwa mashitaka yanayohusiana na makosa ya ugaidi nchini Syria.

Polisi wa West Midlands nchini Uingereza wamesema Bwana Begg, mwenye umri wa miaka 45, mkaazi wa Hall Green, Birmingham, ameshitakiwa kwa kutoa mafunzo ya kigaidi na kufadhili ugaidi nje

Mwanamke anayeshitakiwa pamoja naye, Gerrie Tahari, wa Sparkbrook, Birmingham, anashitakiwa kwa kufadhili ugaidi nje ya nchi.

Watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya mahakama ya Westminster Jumamosi.

Watuhumiwa hao wawili walikamatwa Jumanne. Watu wengine wawili walikamatwa siku hiyo na kuwekwa mahabusu.

Watuhumiwa hao, mmoja mwenye umri wa miaka 36 anatoka eneo la Shirley, Solihull, na mwenye umri wa miaka 20 anatoka Sparkhill, Birmingham, ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za kufadhili vitendo vya kigaidi nje.

Bwana Begg alikuwa akishikiliwa katika gereza la Marekani lililoko Guantanamo Bay nchini Cuba kwa karibu miaka mitatu.

Ni raia wa Uingereza ambaye alihamia Afghanistan pamoja na familia yake mwaka 2001, kabla ya kwenda tena Pakistan mwaka 2002 wakati vita vya Afghanistan vilipoanza.

Alikamatwa mjini Islamabad Januari 2002 na kupelekwa katika kituo cha Bagram nchini Afghanistan kwa karibu mwaka mmoja na baadaye kuhamishiwa Guantanamo.

Aliachiliwa mwezi Januari 2005 pamoja na raia wengine watatu wa Uingereza na kurejea Uingereza.

Bwana Begg, ambaye kwa sasa anaongoza kampeni ya kusaidia familia za watu wanaoshikiliwa magereza, hakuwahi kushitakiwa kwa kosa lolote.

Posted By Unknown04:26

SHEIKH NA MWANAE WAMWAGIWA TINDIKALI ARUSHA

Filled under:



MWALIMU wa dini Msikiti Mkuu wa Bondeni, Mustapha Kihago (49) na mwanae Khalid Mustafa (10), wamemwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali  sehemu za usoni na shingoni.
Sheikh huyo ambaye ni wa pili kukumbwa na mkasa huo ndani ya wiki mbili mkoani hapa, alimwagiwa tindikali wakati alipokuwa ameongozana na mwanae alfajiri, majira ya saa 11, kuelekea msikitini kwa ajili ya kuswali.

Akizungumzia tukio hilo katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru alikolazwa, Sheikh Mustapha alisema kuwa wakiwa wamekaribia kuingia msikitini akiongozana na mwanae Khalid, ghafla alijitokeza mtu katika eneo la msikiti huo wa Ijumaa uliopo Mtaa wa Bondeni na kuwamwagia maji yenye rangi nyekundu na kuwajeruhi usoni, shingoni na maeneo mengine mwilini.

Posted By Unknown04:14

KIGOGO MMOJA WA UVCCM AMETANGAZA KUJIUNGA NA CHADEMA

Filled under:


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Siha, Godwin Mollel ametangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mollel aliyeachia ngazi kwenye chama hicho tawala mwaka 2012 ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara alitangaza nia hiyo jana wakati wa Operesheni ya kumg’oa Mbunge Siha Aggrey Mwanri (CCM).

Kabla ya kutangaza nia hiyo alisema anakumbana na changamoto katika mazingira yake ya kazi ikiwemo kuundiwa tume mara kwa mara kwa ajili ya kumchunguza kwa kuwa yupo upinzani.

Posted By Unknown04:08