MWALIMU wa dini Msikiti Mkuu wa Bondeni, Mustapha Kihago (49) na mwanae Khalid Mustafa (10), wamemwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali sehemu za usoni na shingoni.
Sheikh huyo ambaye ni wa pili kukumbwa na mkasa huo ndani ya wiki mbili mkoani hapa, alimwagiwa tindikali wakati alipokuwa ameongozana na mwanae alfajiri, majira ya saa 11, kuelekea msikitini kwa ajili ya kuswali.
Akizungumzia tukio hilo katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru alikolazwa, Sheikh Mustapha alisema kuwa wakiwa wamekaribia kuingia msikitini akiongozana na mwanae Khalid, ghafla alijitokeza mtu katika eneo la msikiti huo wa Ijumaa uliopo Mtaa wa Bondeni na kuwamwagia maji yenye rangi nyekundu na kuwajeruhi usoni, shingoni na maeneo mengine mwilini.
0 comments:
Post a Comment