Friday, 31 January 2014

JE WAFAHAMU NJIA YA ASILI YA KUTIBU MARADHI YA KUTOPATA CHOO

Filled under:



MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

 SABABU ZA MARADHI HUSIKA: (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.
TIBA: Kanuni ya kwanza:
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.
Kanuni ya pili:
Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.

Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.

Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. . 

MARADHI YA KUHARISHA: MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu. SABABU ZAKE: (1) Kula chakula kichafu. (2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.

Kanuni ya pili: Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.

Kanuni ya tatu: Chukua majani ya nanaa na utayarishe dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu anisuni.
Kanuni ya nne:
Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni.

Kanuni ya tano: Changanya kijiko kimoja cha mafuta ya habat soda ndani ya glasi moja ya maziwa ya mtindi unywe glasi moja kutwa mara mbili.

Posted By Unknown23:26

WAFANYAKAZI WALAZIMISHWA KUSHIRIKI SIKU YA KUZALIWA KWA CCM

Filled under:


Posted By Unknown22:31

ROMANIAN GOVERNMENT OFFERS 85 SCHOLARSHIPS 2014/15

Filled under:


Romanian Government is offering 85 scholarships for citizens of non EU countries. Priority will be given to the candidates applying for: political and administrative sciences, education studies, Romanian culture and civilization, journalism, technical studies, oil and gas, agricultural studies, veterinary medicine, architecture and arts. Scholarships are granted for three levels of study: licenta, master and doctorate. The beneficiaries of the scholarships should study only in the Romanian language. The candidates who do not know Romanian are offered one supplementary preparatory year to study the language. The monthly amount is granted throughout the whole calendar year for full-time students of the 3rd cycle but not during the summer vacation for 1st  and 2nd cycle. The application deadline is 15th February 2014.

Study Subject(s): Priority will be given to the candidates applying for: political and administrative sciences, education studies, Romanian culture and civilization, journalism, technical studies, oil and gas, agricultural studies, veterinary medicine, architecture, arts. Requests for other fields will also be taken into account.  
Course Level: The scholarships are granted for three levels of study:
-for the first cycle (licenta): This scheme is dedicated to graduates of high schools or of equivalent pre-university systems, as well as to candidates who require the equivalation of  partial studies and the continuation of their studies in Romania. The complete cycle of university studies lasts for 3 to 6 years, according to the specific requirements of the chosen faculty, and ends with a final examination (licenta);

-for the 2nd cycle (master): This scheme is dedicated to graduates of university/post graduate studies; it lasts for 1,5 to 2 years and ends with a dissertation;

-for the 3rd cycle (doctorate) this scheme is dedicated to the graduates of university/postgraduate studies (i.e. master); it lasts for 3-4 years, in keeping with the specific requirements of the chosen faculty, and ends with a doctor’s thesis.

Scholarship Provider: Romanian Government Scholarship can be taken at: Romania
Eligibility: -Citizens of non EU countries (irrespective of their country of residence). Priority is given to citizens from non EU states with which Romania does not have cultural and education cooperation agreements. Foreign citizens of Romanian origin and those belonging to the neighbouring historic Romanian communities benefit from other scholarship programmes offered by the Romanian state.

Scholarship Open for International Students: Citizens of non EU countries (irrespective of their country of residence) can apply for these Romanian government scholarships.

Scholarship Description: Scholarships offered by the Romanian State to foreign citizens through the Ministry of Foreign Affairs in keeping with Government Decision No 288/1993 for the 2014-2015 academic year. 85 scholarships for under- and post-graduate studies in Romania, by means of selection of application files organised by the Ministry of Foreign Affairs (MAE) and the Ministry of National Education (MEN), in keeping with Romanian current legislation. In order to promote Romanian language and culture, the Ministry of National Education has decided that the beneficiaries of the scholarships should study only in the Romanian language. The candidates who do not know Romanian are offered one supplementary preparatory year to study the language. The students who declare that they know already Romanian language have to pass a language test organised by the competent  higher education institutions.
Number of award(s): 85 Romanian government scholarships are offered.
Duration of award(s): The monthly amount is granted to the students of the 1st (licenta) and 2nd (master) cycle throughout the whole academic year, the winter and spring vacation included, but not during the summer vacation. For full-time students of the 3rd cycle (doctorate), the monthly amount is granted throughout the whole calendar year.
What does it cover? The scholarship consists of:
-free-of-charge tuition,
-free-of-charge accommodation (depending on availability, accommodation will be offered free-of-charge in students hostels, in keeping with the higher education regulations),
-financial support – a monthly amount representing : the equivalent in Romanian currency of 65 EURO per month, for the under-graduate students (1st cycle), the equivalent in Romanian currency of 75 EURO per month, for post-graduate students (master degrees and specialization) 2nd cycle, the equivalent in Romanian currency of 85 EURO per month, for post graduate students (doctor’s degree) 3rd cycle.
-These scholarships do not cover food,  international and local transport. The candidates must be prepared to support personally any other additional expenses.
Selection Criteria: The selection criteria are: the candidates’ competence (former scholar performances, mentioned in his/her study papers) and the chosen priority field of study. The Boards will approve the list of 85 accepted candidates and a waiting list, in case any selected candidates give up the scholarship.
Notification: The MAE board makes the first selection between 15 and 20 March 2014. By 1 April 2014, MAE sends to MEN the selected files. The MEN Board meets in April 2014 to make the final selection and will send list of successful candidates by 30 April 2014.  The selection results will be announced by 30 May 2014 to each diplomatic mission that submitted application files.
How to Apply: To get all necessary information about the scholarships (conditions, necessary documents, enrolment calendar) and to submit their application files, the candidates should apply directly to :
-the Romanian diplomatic missions accredited to the candidate’s country of origin or of residence or to
-the diplomatic mission of candidate’s state of origin accredited to Bucharest
-Application files submitted by post or directly to the Ministry of Foreign Affairs (MAE) or to the Ministry of National Education (MEN), as well as application files received after the announced deadline will not be taken into consideration.
-Applications files should contain documents in English or French language.
-If the application files contain documents in other foreign languages than English or French, they must be accompanied by authorized translations in one of the following languages: Romanian, English or French. Generally, Romanian universities may require that all enrolment documents should be accompanied by authorized copies and authorized translations in Romanian.
-It is of utmost  importance to fill in correctly all forms.
Scholarship Application Deadline: The application deadline is 15th February 2014.

Posted By Unknown22:24

KINANA AKUTANA NA MADEREVA BODABODA MBEYA

Filled under:





 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa kwa nguvu na madereva wa pikipiki za kubebea abiria maarufu kama Boda boda wakati wa kikao na Boda boda hao kilichofanyika ukumbi wa Mtenda ,Soweto Mbeya ikiwa moja ya sehemu za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.





Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na madereva wa Boda boda kwenye ukumbi wa Mtenda ,Soweto mkoani Mbeya.



Sehemu ya Madereva Boda boda waliohudhuria kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana 


 Sehemu ya Boda Boda zikiwa nje ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya wakati kikao cha Madereva Boda Boda na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Posted By Unknown22:16

GOOGLE EUROPE SCHOLARSHIP FOR STUDENT WITH DISABILITIES, 2014/2015

Filled under:


Google is offering scholarships for students with disabilities who are currently enrolled at a university in Europe for the 2013-2014 academic year. Scholarships are available for pursuing Bachelor’s, Master’s or PhD degree at a university in Europe. Scholarships will be awarded on the basis of strength of the applicant’s academic background, leadership skills and demonstrated passion. Recipients of the Google scholarship for students with disabilities will receive a €7,000 scholarship. Online application must be submitted by February 17, 2014.

Study Subject (s): Scholarship is awarded in Computer Science, Computer Engineering, Informatics or a closely related technical field at a university in Europe.
 
Course Level: Scholarship is for students who intend to be enrolled or accepted as a full-time student in a Bachelor’s, Master’s or PhD program at a university in Europe for the 2014-2015 academic year.
 
Scholarship Provider: Google
 
Scholarship can be taken at: Europe

Eligibility: To be eligible to apply, applicants must:
•Be currently enrolled at a university in Europe for the 2013-2014 academic year
•Intend to be enrolled or accepted as a full-time student in a Bachelor’s, Master’s or PhD program at a university in Europe for the 2014-2015 academic year
•Be studying Computer Science, Computer Engineering, Informatics, or a closely related technical &
•Maintain a strong academic record
•Exemplify leadership and a passion for Computer Science and technology
•Have a disability as a long-term or recurring issue that impacts one or more major activities that others may consider a daily function). This definition also includes the perception among others that a disability exists.

Scholarship Open for Students of Following Countries: Students who are currently studying at a university in Europe are eligible to apply.

Scholarship Description: Google is committed to helping the innovators of the future make the most of their talents by providing scholarships for Computer Science students with disabilities. As part of our commitment, we’ve partnered with Employ ability, a nonprofit organization dedicated to assisting students with disabilities while they pursue education and promising careers.

Number of award(s): Not Known

Duration of award(s): Not Known

What does it cover? Recipients of the Google Scholarship for Students with Disabilities will each receive a €7,000 scholarship for the 2014-2015 academic year.

Selection Criteria: Scholarships will be awarded based on the strength of the applicant’s academic background, leadership skills and demonstrated passion for Computer Science.
Notification: You will receive an email notification once your application is complete and has been submitted online.

How to Apply: Applicants will be asked to complete an online application through Employ Ability which includes:
-General background information (i.e. contact information and details about your current and intended universities for the 2014-2015 school year)
-Resume/CV
-Academic transcripts from your current and prior institutions (if you have earned a prior degree)
-A reference letter from a professor, instructor, adviser or supervisor
-Responses to essay questions
Scholarship Application Deadline: The deadline for applications is February 17, 2014.

Posted By Unknown11:32

JEANNETTE RANKIN FUND (JRF) SCHOLARSHIP FOR WOMEN IN USA, 2014/15

Filled under:



Applications are invited for Jeannette Rankin Fund (JRF) Scholarship to low-income women, 35 and older who are pursuing undergraduate degrees at accredited colleges and universities. These scholarships are awarded without regard to race, creed, religion, color, ancestry, marital status, sexual orientation, gender identity and expression, national origin or disability. These JRF scholarships are for $2,000 each and may be used for tuition, books, transportation, childcare and other living expenses. The deadline to apply for a scholarship for the 2014-2015 school year is March 1, 2014.

Study Subject (s): Scholarships are awarded to learn any of the course available at ACICS accredited school.
 
Course Level: Scholarships are available for pursuing a technical or vocational education, an associate’s degree or a first bachelor’s degree at ACICS accredited school. Scholarship Provider: Jeannette Ran
kin Foundation Scholarship can be taken at: USA
Eligibility: An applicant for a JRF scholarship must be:
-A woman, age 35 or older
-Low-income
-A U.S. citizen or Permanent Resident of the United States
-Pursuing a technical or vocational education, an associate’s degree, or a first bachelor’s degree
-Enrolled in, or accepted to, a regionally or ACICS accredited school
Scholarship Open for International Students: The students of USA can apply for these JRF scholarships.
Scholarship Description: Jeannette Rankin Women’s Scholarship Fund to make financial awards without regard to race, creed, religion, color, ancestry, marital status, sexual orientation, gender identity and expression, national origin, or disability.
Jeannette Rankin Women’s Scholarship Fund has awarded more than $1.8 million in scholarships to more than 700 women.

Duration of award(s): Scholarships will be disbursed over two school terms, starting in Fall 2014.
What does it cover? The scholarships are for $2,000 each and may be used for tuition, books, transportation, childcare and other living expenses.

Selection Criteria: These JRF Scholarships will be awarded on the basis of following factors:
-Students goals
-Students plan for reaching your goals
-How you will use your education to give back to the community

Notification: Scholarship recipients will be notified by phone in June. If your application is disqualified due to ineligibility, you will be notified by e-mail immediately. All other applicants will be notified of their status by e-mail after application review is complete in June. The names of the selected scholars will also be posted on our website by July 1.

How to Apply: The mode of applying is online.
Scholarship Application Deadline: The application deadline is March 1 2014.

Posted By Unknown11:20

JE WAJUA,KITUNGUU SAUMU NI DAWA INAYOPONYESHA MAGONJWA MBALIMBALI

Filled under:



Kitunguu saumu ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula hapa nchini, ingawa watu wengi hukitumia kwa kuongeza harufu kwenye chakula bila kufahamu matumizi yake yenye manufaa kiafya

Harufu yake siku za sikukuu, umuhimu wake kwenye chakula kipendwacho na wengi Tanzania yaani pilau, umekifanya kuwa kiungo muhimu cha chakula nchini.
Kwa sasa  umaarufu wake umeenda mbali zaidi baada ya wanasayansi kubaini kuwa kitunguu saumu kina kinga muhimu katika mwili wa binadamu, kambayo  huweza kuzuia maradhi ikiwemo saratani na malaria.
Wanasayansi walibaini  kuwa kitunguu saumu kina kemikali ya  ‘allicin’  ambayo hutoka baada ya kukatwa au kutafunwa na husaidia kuzuia maradhi ya saratani na malaria.
Inaaminiwa kwamba  kitunguu saumu huweza kupunguza athari za kemikali nyingine zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi na kuimarisha uwezo wa seli za mwili.
Utafiti umeonyesha pia kwamba huweza kusaidia kwa wale wenye matatizo ya mafua na hata kuukinga mwili dhidi ya malaria na saratani.
Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tiba cha Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic Dk Africanus Boniface anasema, kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambavyo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
“Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
“Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti,” alisema Dk Boniface.
 Uwezo wake kiutendaji;

“Dk Boniface anasema vitunguu swaumu vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation), kwa kubadilisha ‘polysulfides’ zilizopo ndani yake kuwa ‘hydrogen sulfides’ kwenye seli nyekundu za damu.
“Na pia husaidia udhibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya ‘homocystine’ na kupunguza madhara ya kisukari. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na ‘phytoncide’ ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali,” alisema.
Alisema harufu mbaya au nzuri ya kitunguu swaumu hutokana na gesi aina ya ‘hydrogen sulfide’ ambayo hutolewa baada ya kuvila.

Dk Boniface anasema, kitunguu  kinatibu  maradhi  mbalimbali  kama   vile: Saratani  ya  tumbo  na  utumbo  mkubwa, huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation), katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu.
Athari zake mwilini
Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya ushauri nasaha, lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu yeye anasema kitunguu swaumu kina faida nyingi lakini kinaweza kuathiri mwili wa mwanadamu iwapo kikitumika wakati usiofaa.
 “Ukiacha faida zake, vitunguu saumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na: Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.

Posted By Unknown08:45

CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUMNYANG'ANYA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA

Filled under:

 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka serikali kumnyang’anya  Mwekezaji wa kiwanda cha sukari Mtibwa rasimali hiyo, kwa kuwa ameshindwa kuwalipa wakulima na Wafanyakazi, hivyo kutishia maisha, ustawi, maendeleo, uchumi na afya wananchi zao.

Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya (CHADEMA), ikiwa ni siku chache baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka, kusimamisha uzalishaji wa kiwanda hicho hadi wakulima na Wafanyakazi hao watakapolipwa Malipo yao sh.Bil. 1.9/-.

Hatua zote hizo zimekuja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,  kumnanga  Mkuu wa Wilaya hiyo Mtaka, kuwa hatua yake ya kukifunga Kiwanda hicho alikurupuka, na kwamba alichostaahili kufanya ni kuhakikisha anapata njia mbadala ya wananchi hao kupata Malipo yao na si siasa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Diwani  Mwakambaya, ameiijua juu Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na watendaji wake, kwamba hawana uchungu na maisha ya wananchi wanaonyanyasika ndani ya nchi yao, kutokana na kushindwa kumuadabisha mwekezaji wa Kiwanda hicho.

“Wananchi wanashindwa kulipa matibabu ya ndugu zao Hospitali ya Bwagala, Wanafunzi wameshindwa kupelekwa shule, wanashindwa kuvaa na kujikimu wenyewe kwa mahitaji, kutokana na mwekezaji kuhodhi Malipo ya wakulima wadogo wa miwa na mishahara ya Wafanyakazi.

“Ninafanya upembuzi yakinifu wa majina ya wastaafu zaidi ya 110 waliokufa bila kupata mafao na haki zao stahili, huku wengine wakiwa wamelipwa kati ya Laki 5/- au Mil.1/- ijapokuwa wamefanya kazi zaidi ya miaka 32 na wengine kufukuzwa bila sababu”. Alisema Mwakambaya.

Mwakambaya alisema, katika ahadi aliyoitoa Meneja wa Kiwanda, Hamad Yahaya, siku ya Mkutano wa hadahara baina ya Mkuu wa Wilaya Mtaka na Wakulima na Wafanyakazi, aliahidi kuingiza fedha sh. 1.9/- bilioni kuanzia leo (jana), lakini fedha iliyoingizwa kwenye chama kimoja cha wakulima ni Mil.70/- tu.

Alisema hali hiyo ni dharau na matusi kwa wakulima na Wafanyakazi wanaoteseka na familia zao nchini kwao, kana kwamba wako Somalia, hivyo akadai anasikilizia kikao cha kesho na Mtaka kitakuwaje laa sivyo, wataiomba Polisi iwalinde mlangoni kwa mwekezaji watakakoweka mikeka.

Katika Kikao na Mkuu wa Wilaya (Mtaka) Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Mvomero na Diwani wa Kata ya Diongoya, John Van Zealand (CCM), pia alimjia Juu mwekezaji kwa kushindwa kuwalipa wakulima na Wafanyakazi hao, na kudai hata Malipo tu ya Halmashauri halipi, je ya wananchi!

Wanaharakati mbalimbali wa ndani na nje ya Mtibwa, wameuunga mkono kusudi la wakulima na Wafanyakazi ambao hadi tunaenda mitamboni hawako kazini, kufanya maandano ya amani ya kuitaka serikali imnyang’anye mwekezaji huyo kiwanda, maana anakiuka haki za binadamu, na kwamba wako tayari kuongoza maandamano hayo kudai haki hiyo.

Posted By Unknown08:14

CCM YAMWANDALIA ZITTO HELIKOPTA KURUKA MIKOANI ILI KUPAMBANA NA CHADEMA

Filled under:



USHINDANI wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umefikia hatua mpya baada ya CCM kuibuka na mkakati wa kumtumia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kupambana na CHADEMA waziwazi.
 
Katika mkakati huo CCM imepanga kukodisha helikopta ya kumpeleka Zitto katika mikoa minne kwa gharama ya sh milioni 50 mara tu baada ya CHADEMA kuhitimisha Operesheni yao ya M4C Pamoja Daima.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vilivyo karibu na Zitto na CCM, yeye na chama hicho sasa wana adui mmoja – CHADEMA; na wameamua kujibu mapigo baada ya kuridhika kwamba kwa vyovyote Zitto amekwisha kupoteza uanachama wake katika CHADEMA.

Nia yao ni kumtumia Zitto kuleta mpasuko katika CHADEMA, na kufunika mjadala wa mgogoro wa CCM, kero za wananchi na mchakato wa Katiba mpya.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA – Naibu Katibu Mkuu Bara, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Baraza Kuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – anatarajia kutumia helikopta yenye uwezo wa kubeba watu wanne, ambayo inadaiwa kukodishwa na wapinzani wa CHADEMA.

Kwa mujibu wa habari hizo, lengo la ziara ya Zitto ni kujibu mapigo ya CHADEMA, hasa katika maeneo ambayo baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho wamepita na kuzungumzia hatima yake kisiasa, hasa walipojibu maswali ya wananchi kuhusu sakata lake kuvuliwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, na hatimaye Zitto kwenda mahakamani kuzuia chama kujadili uanachama wake.

Katika kesi ya msingi, Zitto aliyewahi kuwa maarufu akiwa kiongozi wa CHADEMA, anaomba arudishiwe nyadhifa zake zote, na apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ili aweze kukata rufaa Baraza Kuu.

Taarifa zinasema tayari chama kimempatia nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Zitto amekwisha kujiondoa kwenye chama hicho kwa kupeleka shauri mahakamani.

Taarifa za Zitto kuanza ziara mikoani zilianza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mikoa iliyotajwa ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam, ingawa maandalizi yanaendelea na kuna uwezekano wa kubadili baadhi ya mikoa kulingana na mkakati wao.

Kwa hadhi yake ya sasa, CHADEMA imeshasema haitahusika na mikutano yake, na wanachama wake hawatajihusisha nayo. Uratibu wa mikutano yake unafanywa na viongozi waandamizi wa CCM.

Baadhi yao walizungumza na gazeti hili kwa kujitapa kwamba hii ndiyo njia ya kuimaliza CHADEMA, lakini hawakutaka kutajwa majina gazetini.

Iwapo Zitto atakubali ufadhili huo wa CCM na kuendelea na mikutano yake, ni wazi atakuwa amekamilisha ushahidi wa kinachodaiwa na chama chake kwamba amekuwa akikisaliti kwa masilahi ya CCM.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa CCM walipoombwa maelezo juu ya urafiki wao na Zitto kiasi cha kumkosanisha na chama kilichomlea kisiasa, CHADEMA, walisema kwamba urafiki uliopo si wa Zitto na CCM, bali Zitto na Rais Jakaya Kikwete.

Gazeti hili linafahamu kwamba wakati fulani mwaka juzi Zitto alipobanwa na wabunge wenzake kuhusu tabia zake za kuwasaliti kwa Rais Kikwete, alisisitiza kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake binafsi, kwa hiyo wamwelewe.

Vilevile, wapo wanaohoji nia ya ziara hii wakati kwa muda mrefu amekuwa akikwepa kuambatana na viongozi wenzake katika ziara na operesheni nyingi za kichama.

Wanasema kwa kuwa operesheni ya sasa ya CHADEMA imepewa jina la M4C Pamoja Daima, kitendo cha CCM kuandaa ziara ya Zitto na kumkodishia helikopta, ni uthibitisho kuwa Zitto hayuko pamoja na CHADEMA tena.

Wameongeza pia kuwa kama hilo litafanyika, litakuwa limemwingiza Zitto katika orodha ya makada kadhaa wa upinzani waliotumikia CCM baada ya kufukuzwa au kunyimwa fursa za uongozi katika CHADEMA, kama Tambwe Hiza, Dk. Aman Walid Kabourou na Dk. Masumbuko Lamwai.

Alipotafutwa athibitishe kuhusu ziara hii na kama ni kweli inafadhiliwa na CCM, Zitto hakuweza kupatikana.

Mbowe kuwania tena uenyekiti

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa kamwe hatakiacha chama hicho katika uchanga wa harakati za kulikomboa taifa kama kiongozi wake wa juu.

Akihutubia katika mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima katika sehemu mbalimbali mkoani Morogoro jana, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa, bado atagombea nafasi ya uenyekiti kwa lengo la kuendeleza harakati za ukombozi wa pili wa taifa hili.

Bila kutaja jina, Mbowe alionya kuwa wenye fikra za kuachiwa chama hicho kikiwa katikati ya ukombozi huo hawatapata nafasi, kwa sababu hawana nia thabiti ya kukiendeleza, bali wana nia ya kukibomoa kwa kutumiwa na wapinzani wa CHADEMA.

“Makamanda, kumbukeni kuwa chama hiki na sisi viongozi wake tumepita katika majaribu makubwa na hata kukoswakoswa kuuawa. Mimi nimekoswakoswa kuuawa kwa bomu huko Arusha, lakini pia kuna watu wamepoteza maisha, wamefungwa jela, wengine wamekuwa vilema, halafu watu wengine wanatusaliti kwa kupewa visenti ili wakivuruge chama na wanataka tuwape chama. Huu ni uendawazimu,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema CCM imekuwa ikifanya jitihada za kuihujumu CHADEMA kwa mbinu mbalimbali, zikiwemo za kupandikiza migogoro, jambo ambalo limeshindwa kufanikiwa kwani Mungu ameweka mkono wake ili kisisambaratike.

“Harakati hizi tunazofanya za kuwakomboa Watanzania mjue tunahatarisha maisha yetu, tumejaribiwa kushawishiwa ndani na nje ya Bunge ili tuwe kondoo, tumekataa. CCM wamekuja na mbinu za kupandikiza migogoro wameshindwa na sasa wanaomba nife wakifikiri nikifa na CHADEMA itakufa. Nawaambia CHADEMA haifi kwa kuwa tumezalisha makamanda wengi, watakiendeleza,” aliongeza Mbowe.

Akielezea kwa mara ya kwanza kwa undani zaidi kuhusu mauaji ya Arusha, mwenyekiti huyo alisema wana ushahidi wa kutosha kwamba polisi walihusika na mauaji hayo na kuongeza kuwa waliohusika ni polisi wa kutoka mkoani Morogoro.

“Kwa mara ya kwanza niliseme hili, mauaji ya Arusha yaliyofanyika kwa kurusha bomu katika mkutano wa kampeni za CHADEMA, yalifanywa na polisi ambao walitoka mkoani Morogoro. Ndiyo maana tunaendelea kumwambia Rais Jakaya Kikwete aunde tume ya kimahakama ili kupata ukweli wa jambo hili,” alisema.
Kuhusu Katiba

Akizungumzia msimamo wa CHADEMA kuhusu muungano, Mbowe alisema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ya serikali tatu.

Alisema hata tafiti mbalimbali zilizofanyika, zikiwemo za wanasheria na wachumi zinaonyesha kuwa Muungano utaimalika zaidi chini ya muundo wa serikali tatu.

“Nawaonya Wana CCM wasijaribu kuingilia mjadala wa Bunge la Katiba na kama wanataka nchi ichimbike, basi walazimishe serikali mbili,” alisema Mbowe.

“Zipo tetesi za CCM kutaka kupitisha hoja zao kwa nguvu kutokana na idadi yao ndani ya wabunge zaidi ya 600, wakiwemo 356 wa Bunge la Tanzania Bara, 84 kutoka Zanzibar na 201 kutoka makundi mbalimbali watakaokwenda kwenye bunge hilo. Wasidanganyike kwamba wanaweza kutumia wingi wao kubadilisha maoni ya Watanzania kuhusu serikali tatu,” alisisitiza Mbowe.

Halima Mdee anguruma

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye yuko katika msafara wa mwenyekiti huyo, alisema vijana wengi wanaochipukia katika siasa kupitia chama hicho, wamelelewa na Mbowe, ambao leo wamekuwa chachu ya mabadiliko nchini.

“Ukweli ni kwamba kamanda huyu wa anga (Mbowe), ndiye ametulea vijana wengi nikiwemo mimi, tena wengine hatukuwa na ujasiri tulionao sasa, asiwadanganye mtu, hasa sisi vijana kwamba tuliingia CHADEMA na umaarufu, hawapo hao, tumelelewa na huyo kamanda,” alisisitiza huku akipigiwa makofi.

Posted By Unknown06:28

CHADEMA WASUSIA BUNGE LA KATIBA MPYA

Filled under:


Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema wabunge wa chama chake watasusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ikiwa hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu itapingwa na wabunge wa CCM, Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano.
Akihutubia kwenye Uwanja wa Tubuyu nje kidogo ya Mji wa Morogoro juzi, Mbowe alisema wabunge wa chama chake wataandamana nchi nzima kufikisha ujumbe kwa wananchi kwamba maoni yao yamepingwa na wabunge wa CCM walio wengi.
“Tutawaeleza wananchi kwamba maoni ya CCM ndiyo yameonekana ya maana kuliko ya wananchi ambao ni wengi zaidi,” alisema Mbowe kwenye mkutano huo ambao ni sehemu ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko - M4C Pamoja Daima.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikusanya maoni na kubaini kuwa asilimia 62 ya Watanzania wanataka Serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.
“Serikali ya CCM haitaki kusikia maneno Serikali tatu wanasema sera yao ni ya Serikali mbili, wanafanya kila hila ili kuikataa hoja hiyo. Natangaza kwamba wakifanya hivyo tutasusia na kwenda kuwashtaki kwa wananchi,” alisema Mbowe.
Aliongeza kwamba wataandamana kuanzia Kagera hadi Mtwara kuwaeleza wananchi kwamba hoja yao imepingwa na CCM.
Mbowe alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakitoa kashfa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba amechukua maoni ya Chadema.
“Wanakosea hayo si maoni ya Chadema, bali ni maoni ya wananchi, Warioba amezingatia maoni ya wananchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Katiba inayotafutwa si ya chama, bali ni ya Watanzania na kwamba inashangaza CCM kuipinga hoja Serikali tatu.
“Tunafahamu wanaogopa kuikubali hoja ya Serikali tatu kwa sababu wanafahamu huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa madarakani,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Alisema CCM wanaelewa kwamba kukiwa na Serikali tatu, Chadema kitashinda Tanganyika na CUF Zanzibar katika uchaguzi wowote utakaoitishwa.
“Kwa hiyo hivi sasa wana wasiwasi kweli, wanatafuta kila njia ya kuichakachua hoja ya Serikali tatu lakini wafahamu kuwa Chadema wanaifuatilia hoja hiyo kwa ukaribu,” alisema.
Aliwataka wananchi kufuatilia Bunge Maalumu la Katiba litakapoanza mwezi ujao ili kuangalia wabunge wao wanavyowawalisha katika suala hilo muhimu.
Hata hivyo, Mbowe alisema chama hicho kikishinda katika uchaguzi wa mwaka 2015 hakitahangaika kulipa kisasi kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi, bali kitajikita kutafuta maendeleo.
“Wasituogope tutasamehe kama alivyosamehe aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Hatutalipa kisasi tukiingia Ikulu, kwa sababu hakuna binadamu asiye na makosa. Tutaelekeza nguvu zetu kuwaletea maendeleo Watanzania,” alisema Mbowe.
Jussa na Muungano
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kiembesamaki jana, Jussa alisema hakutakuwa na maendeleo yatakayofikiwa Zanzibar ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautang’oka.
Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF, alisema Zanzibar yenye watu milioni 1.5 haiwezi kuwa na tatizo la watu kukosa ajira lakini sera na mipango ya kiuchumi imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na kukosa mamlaka kamili.
Alisema Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi za kimataifa bila ya kuwekewa dhamana na Waziri wa Fedha wa Muungano wakati Zanzibar ni nchi na kuwataka wananchi kutumia kura zao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuleta mabadiliko ya kiutawala.
“Hakuna sababu ya vijana Zanzibar kukosa ajira, kuna watu wasiozidi milioni 1.5, Muungano umefika wakati ung’oke, ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Zanzibar na watu wake kiuchumi na kisiasa,” alisema Jussa.
Alisema mradi wowote unaobuniwa Zanzibar hauwezi kupata mfadhili bila kuwekewa dhamana na Serikali ya Muungano na kukwama kwa juhudi zote za kujiunga na jumuiya za kimataifa akitolea mfano Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Alisema Rais wa Zanzibar amepoteza mambo muhimu chini ya mfumo wa Muungano ikiwa ni pamoja na kutopigiwa mizinga 21 akiwa nje ya nchi, kupeperusha bendera ya Zanzibar, kutokagua gwaride na kupigiwa wimbo wa Taifa la Zanzibar.
“Haya ya sasa si mamlaka kamili, wapi Dk Shein alikokwenda akapigiwa mizinga 21 au alipeperushwa wapi bendera ya Zanzibar wakati wa safari zake za nje?” alihoji Jussa.

Posted By Unknown03:15

Thursday, 30 January 2014

TFDA IMEINGIA KATIKA KASHFA BAADA YA KUMUAJIRI MTUMISHI ASIYE NA CHETI CHA TAALUMA YOYOTE.

Filled under:



MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeingia kwenye kashfa ya kumwajiri mtumishi asiye na cheti cha kitaaluma kuwa msaidizi wa maabara ya dawa kuanzia Desemba 2, 2013.

Mkurugenzi wa TFDA, Hiiti Sillo, jana alithibitisha kufanyika kwa udanganyifu huo lakini akafafanua kuwa baada ya kujiridhisha na tuhuma hizo, mtumishi huyo, Pilly Komba Kilongosi, amekabidhiwa barua ya kuachishwa kazi rasmi kuanzia Januari 28, 2014.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa TFDA kupitia gazeti la serikali la Daily News la Julai 1, 2013 ilitangaza nafasi za kazi saba ikiwemo hiyo ya msaidizi wa maabara ya dawa ambapo mwombaji alitakiwa kuwa na sifa za elimu ya kidato cha nne na mwenye uzoefu usiopungua miaka mitatu katika kazi hiyo.

Vigezo vingine ni mwombaji kuambatanisha barua ya maombi, wasifu wake (CV), nakala za vyeti na hati ya matokeo (transcripts), picha mbili za pasipoti na majina ya wadhamini wawili.

Vyanzo vyetu vilibaini kuwa Pilly alituma barua ya maombi Julai 5, 2013, akionyesha kuwa amehitimu kidato cha nne katika Sekondari ya Temboni jijini Dar es Salaam na kisha kuhudhuria kozi ya msaidizi wa maabara ngazi ya III na II katika Chuo cha Veta cha Dar es Salaam mwaka 2011/2012.

Katika barua hiyo, Pilly anadai kuwa anao uzoefu katika kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu akifanya kazi kama mfanyakazi wa muda TFDA na TBS wakati ukweli ni kwamba amefanya mafunzo kwa vitendo kwa miezi 12 pekee yaani TFDA mizei tisa na TBS miezi mitatu.

Pilly aliongeza kuwa ameambatatisha nakala za vyeti kikiwemo kile cha kidato cha nne ambacho hana kutokana na kupata daraja sifuri katika mtihani wake wa mwisho, CV na hati ya matokeo ya kitaaluma.

Katika hatua inayotia shaka kwamba Pilly aliandaliwa mapema kupewa ajira hiyo, majukumu saba yanayotajwa katika tangazo kwa mwombaji kuyajua, ndiyo hayo hayo yameorodheshwa na Pilly katika CV yake neno kwa neno kuanzia namba moja hadi saba.

Kwa mujibu wa vielelezo ambayo gazeti hili linavyo, Pilly alihitimu kidato cha nne mwaka 2010, ambapo alifanya mtihani kwa namba S3799/0098 na kupata daraja sifuri la alama 35 akiwa amepata F katika masomo yake yote ya Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili, Kiingereza, Baiolojia na Hesabu.

Pamoja na kukosa vigezo tajwa, Pilly aliajiriwa kama mtumishi wa TFDA tangu Desemba 2, 2013 hadi Januari 28, 2014, alipofukuzwa baada ya kubainika alipenyezwa kinyemera.

Alipohojiwa Mkurugenzi wa TFDA kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa waliofanya udanganyifu huo, alisema kuwa hizo ni taratibu za ndani za utumishi ambazo zinaendelea kufanyika.

“Ni kweli huyo binti aliajiriwa kwetu lakini kama unavyosema baada ya kufanyika uchunguzi tulibaini makosa yalifanyika wakati wa mchakato wa usaili, hivyo jana amepatiwa barua ya kuachishwa kazi rasmi na amehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),” alisema Sillo.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu madai hayo, Pilly alithibitisha kupewa barua ya kuachishwa kazi juzi akielezwa kuwa alikosa sifa ya kutokuwa na cheti cha kitaaluma cha kidato cha nne na kwamba alihojiwa pia na TAKUKURU ili kutoa maelezo.

“Alipoulizwa alipataje kazi wakati hakuwa na vigezo, Pilly alijitetea kuwa: “Kazi zilitangazwa nikaomba na nikapata, hivyo siwezi kujua vigezo gani walitumia katika mchakato wa usaili”.

“Alipoulizwa alipataje kazi wakati hakuwa na vigezo, Pilly alijitetea kuwa: “Kazi zilitangazwa nikaomba na nikapata, hivyo siwezi kujua vigezo gani walitumia katika mchakato wa usaili”.

Posted By Unknown09:35

RAIS JK AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAKE IKULU LEO

Filled under:



Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na waziri na manaibu waziri waliokuwa  waliokuwa wakiapishwa ikulu Dar es Salaam leo


Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Ummy Mwalimu kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais 



Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Boniface Simbachawene kuwa,naibu waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi
Rais akumuapisha kaika  Saning'o Telele kuwa Naibu Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi

Rais akimuapisha Eng.Dr Binilith Satano Mahenge kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira

Posted By Unknown07:43

Wednesday, 29 January 2014

MBOWE ASEMA, DC MTAKA AMEKURUPUKA

Filled under:



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemnyoshea Kidole Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka, akidai uamuzi wake wa kufunga Kiwanda cha Mtibwa hadi kitakapolipa madeni ya wakulima na Wafanyakazi , ‘amekurupuka’.
 
Mbowe alitoa kauli hiyo leo (jana) kufuatia malalamiko ya wananchi walioshitushwa na uamuzi wa Serikali kupitia kwa Mkuu wa wilaya hiyo, kuamua kufunga kiwanda badala ya kumnyang’anya kutokana na Mwekezaji huyo kudaiwa na wakulima na Wafanyakazi zaidi ya Sh. Bilioni 1.2/-
 
Akihutubia umati wa wananchi wa Mji Mdogo wa Madizini na vitongoji vyake, Mbowe alimnyoshea Kidole Mkuu wa wilaya Mtaka akisema, “Madeni anayodaiwa Mwekezaji huyu, suluhu yake siyo kufunga Kiwanda, bali Serikali iltakiwa kutafuta fedha ya kuwalipa wakulima na Wafanyakazi hao.
 
“Katika hili DC amekurupuka, wakulima na Wafanyakazi wanataka Malipo yao, habari ya uamuzi wa kufunga kiwanda, ni kumnusuru mdaiwa asiwajibike, na wala haisaidii dai la msingi la wananchi, hivyo kilistahili ni Malipo na kuiangalia adha hiyo kitaifa maana inahusisha watu wengi”.alisema Mbowe.
 
Mbowe aliwaita viongozi chadema wamwambie malalamiko ya wananchi ili wamtune Kambi upinzani bungeni ikamhoji Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambapo Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, alieleza Manyanyaso, Dhuluma na ucheleweshaji wa Malipo yanayofanywa na mwekezaji dhidi ya wananchi na kuahidi kuyafanyia kazi.
 
Mbali na Mbowe kusisistiza tena kuhusu kuboreshwa kwa daftari la kura na mchakato mzima wa Katiba, ameendelea kudai, lisipoboreshwa daftari hilo Chadema haitakuwa tayari kuingia katika kura ya maoni, ila itarudi kwa umma kuwataka kususia mchakato huo, unaokumbatiwa na CCM.

Halima Mdee awahamasisha akina mama kuikataa CCM.
Aidha Mbunge wa Kawe Halima Mdee, akiambatana na, Suzan Kiwanga, amewataka akina mama wilayani Mvomero kuikataa CCM na Propaganda zake kwa sababu kila adha wanayoipat ikiwa ni pamoja na kupora ardhi kunakofanywa na vigogo wastafu wa CCM na walioko madarakani, madhara yake ni kwao hivyo waungane kuikataa CCM na kuichagua Chadema.

Posted By Unknown20:02

ISLAMIC DEVELOPMENT BANK OFFERS SCHOLARSHIP FOR MUSLIM COMMUNITIES,2014

Filled under:



Islamic Development Bank offers Scholarship Programme for Muslim Communities in Non-Member Countries. Scholarships are provided in the field of Medicine, Engineering, Agriculture and other fields related to these disciplines. The Programme provides scholarship to the academically meritorious but financially needy young Muslim students to pursue undergraduate or first-degree study in professional courses. The Programme covers all relevant expenses during students’ study period, including tuition fees, health and living costs as determined by the IDB.

Study Subject (s): Scholarships are provided in the fields of Medicine, Engineering, Agriculture and other fields related to these disciplines.
 
Course Level: The Programme provides scholarship to the academically meritorious but financially needy young Muslim students to pursue undergraduate or first-degree study in professional courses.
 
Scholarship Provider: Islamic Development Bank
 
Scholarship can be taken at: Applicants home country (Their own countries or in the IDB member countries on exceptional basis)

Eligibility: The applicant must meet the following eligibility criteria:
-Age not over 24 years.
-Completed senior secondary education (pre-university study) with good grades in major science  subjects and  language of instruction.
-Secured admission in one of the disciplines covered under the Programme at a recognized college or university in their own countries (for in-country study).
-Not in receipt of any other scholarship.
-Committed and needy Muslim.
-Recommended by the Counterpart Organization.

Scholarship Open for International Students: The students of Argentina, Australia, Bosnia & Herzegovina, Brazil, Bulgaria, Burundi, Cambodia, Canada, Central African Republic, China, Congo, Croatia, Democratic Rep. of Congo, Eritrea, Ethiopia, Fiji, Ghana, Greece, Guyana, India, Kenya, Kibris, Kosovo, Lesotho, Liberia, Macedonia, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mongolia, Myanmar, Namibia, Nepal, New Zealand, Papua New Guinea, The Philippines, Russian Federation, Rwanda, Seychelles , Singapore, South Africa, Sri Lanka, Tanzania, Thailand, Trinidad & Tobago, U.S. Virgin Islands, Vanuatu, Vietnam, Zambia, Zanzibar(Tanzania), Zimbabwe, Cote d’Ivoire, Guinea Bissau, Mozambique, Palestine, Somalia, Sudan and Togo can apply for these scholarships.

Scholarship Description: The Programme was launched in 1404H (1983G), named “The IDB Scholarship Programme for Muslim Communities in Non-Member Countries” (SPMC). The objective of the Programme is to improve the socio-economic conditions and to preserve the cultural and religious identities of Muslim Communities in Non-member Countries through developing their human capital resources. The Programme provides scholarship to the academically meritorious but financially needy young Muslim students to pursue undergraduate or first-degree study in professional courses. The concept of the Programme is to build a team of professional and committed Muslims as a tool for the improvement of the socio-economic conditions of their communities. Under this Programme, the scholarships are given as interest-free loan to the students but grants to the communities to which they belong. After graduation and gainful employment, all graduates are obliged to repay their loan amount to the community (IDB Local Trusts) for recycling and awarding additional scholarships to the local needy students.

Number of award(s): Not Known
Duration of award(s): Not Known
What does it cover? The Programme covers all relevant expenses during students’ study period, including tuition fees, health and living costs as determined by the IDB.
Selection criteria: Each year, the Programme follows the following selection procedures:
-The Counterpart Organization announces the Programme in the country and invites applications from potential candidates who fulfill the criteria of the Programme.
-The Scholarship Selection Committee (SSC) conducts the interviews of eligible candidates and recommends them through the Counterpart Organization to the IDB.
-The IDB makes the final selection and informs the Counterpart Organizations.
Notification: Not Known
How to Apply: The application form must be properly completed and submitted to the Counterpart Organizations in the country, accompanied by all the requisite documents and not directly to the IDB Headquarters in Jeddah. In countries, where the Programme is being implemented, inquiries can be made and application form obtained from Counterpart Organization in the country. In a country, where the Programme has not yet been implemented, inquiries may be directed to the Scholarship Division, Department of Communities in Non-Member Countries, IDB.
Scholarship Application Deadline: The application deadline is December.

Posted By Unknown12:21