MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):
Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja
kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka
huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha
mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu
mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa
siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.
SABABU ZA MARADHI
HUSIKA: (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi
ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula
vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji
ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye
maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.
TIBA: Kanuni ya kwanza:
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili
vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda.
Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya
choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.
Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.
Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.
Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. .
MARADHI YA KUHARISHA: MARADHI ya kuharisha
ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa
huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu. SABABU
ZAKE: (1) Kula chakula kichafu. (2) Kula chakula kilichoingia viini vya
maradhi.
TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua
kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe
cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza
sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho
vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.
Kanuni ya pili: Chukua anisuni
(aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai
cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya
maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa
kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa,
dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.
Kanuni ya tatu: Chukua majani ya nanaa na utayarishe dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu anisuni.
Kanuni ya nne: Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni.
Kanuni ya nne: Chukua zaatar na uandae dawa kama mfano wa hapo juu kuhusu majani ya nanaa na anisuni.
Kanuni ya tano: Changanya kijiko kimoja
cha mafuta ya habat soda ndani ya glasi moja ya maziwa ya mtindi unywe
glasi moja kutwa mara mbili.
0 comments:
Post a Comment