Kitunguu saumu ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula hapa nchini, ingawa watu wengi hukitumia kwa kuongeza harufu kwenye chakula bila kufahamu matumizi yake yenye manufaa kiafya
Harufu yake siku za sikukuu, umuhimu wake kwenye chakula kipendwacho na wengi Tanzania yaani pilau, umekifanya kuwa kiungo muhimu cha chakula nchini.
Kwa sasa umaarufu wake umeenda mbali zaidi baada
ya wanasayansi kubaini kuwa kitunguu saumu kina kinga muhimu katika
mwili wa binadamu, kambayo huweza kuzuia maradhi ikiwemo saratani na
malaria.
Wanasayansi walibaini kuwa kitunguu saumu kina
kemikali ya ‘allicin’ ambayo hutoka baada ya kukatwa au kutafunwa na
husaidia kuzuia maradhi ya saratani na malaria.
Inaaminiwa kwamba kitunguu saumu huweza kupunguza
athari za kemikali nyingine zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi
na kuimarisha uwezo wa seli za mwili.
Utafiti umeonyesha pia kwamba huweza kusaidia kwa
wale wenye matatizo ya mafua na hata kuukinga mwili dhidi ya malaria na
saratani.
Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tiba cha Neema
Herbalist & Nutritional Foods Clinic Dk Africanus Boniface anasema,
kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambavyo kwa kitaalamu huitwa Allium
sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani
hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi
makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
“Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu
mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi
mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo
katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
“Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu
vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa
Ugiriki na Roma. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na
faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa
(ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti,” alisema Dk
Boniface.
Uwezo wake kiutendaji;
“Dk Boniface anasema vitunguu swaumu vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation), kwa kubadilisha ‘polysulfides’ zilizopo ndani yake kuwa ‘hydrogen sulfides’ kwenye seli nyekundu za damu.
“Na pia husaidia udhibiti wa kiwango cha sukari
mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya ‘homocystine’ na kupunguza
madhara ya kisukari. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu
hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na
‘phytoncide’ ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali,” alisema.
Alisema harufu mbaya au nzuri ya kitunguu swaumu hutokana na gesi aina ya ‘hydrogen sulfide’ ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Dk Boniface anasema, kitunguu kinatibu maradhi mbalimbali
kama vile: Saratani ya tumbo na utumbo mkubwa, huzuia kusanyiko
la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation),
katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta
yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu.
Athari zake mwilini
Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya
ushauri nasaha, lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu yeye anasema
kitunguu swaumu kina faida nyingi lakini kinaweza kuathiri mwili wa
mwanadamu iwapo kikitumika wakati usiofaa.
“Ukiacha faida zake, vitunguu saumu pia vina
hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na:
Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl
sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa
maziwa au kunywa maji mengi.
0 comments:
Post a Comment