Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanadaiwa kupigana
huko Malaysia baada ya kukutana hotelini, wakati wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), walipokuwa katika ziara ya kikazi
nchini humo.
Tukio hilo lilitokea siku nne zilizopita baada ya mbunge wa kamati hiyo
kutoka CCM kuvamiwa alipokuwa akipata kifungua kinywa kwenye hoteli
aliyofikia na wenzake wawili mmoja wa CCM na mwingine wa CHADEMA. Majina
ya wabunge hao watatu tunayahifadhi kwa sasa kwa sababu hatukuwapata
kujibu tuhuma hizo.
Hata hivyo, mbunge...