Robert Mugabe amefikisha miaka 90 hii leo na wikendi
hii kutakuwa na sherehe si haba nchini Zimbabwe kusherehekea maisha
marefu ya kiongozi huyo.
Alizaliwa katika kijiji cha Kutama,
kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na wayesuti, na
baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania
uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa
wayajua kumhusu kiongozi huyu-na ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais
kwa muda mrefu mno.
1) Zoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi
mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe
alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi
na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC
idhaa ya dunia.
Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni
kuwa ywapenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha
pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo anapokula.
2) 'Kufufuka'
Ingawa kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe
hana afya nzuri, afya yake na kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema
kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,“
Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa
mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa alilelewa katika familia ya
kikatoliki-mamake alikuwa mcha Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha
habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si
Mkristo anayetumikia dini kwa sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi
ya mchezo wa kriketi. Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa
Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare,
ambapo anaweza kutazama kwa makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia
inawafanya watu kuwa wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya
Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe;
nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”
4) Hapendi kushindwa
Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na
mzuri kabisa katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika
shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo
huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na
Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama
kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012.
“Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani,
hata mimi pia hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote
vilivyoko mbele yangu.”
5) Alipata mtoto akiwa ana miaka 73
Ana watoto watau na mke wake wa pili, Grace
Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka
mmoja baada ya wao kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa
kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe
alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya
mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya
Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley
Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni
hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa
alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980,
Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila
alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda
Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na
waimbaji wa mitindo ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini
Jamaica, wana uhuru wa kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote
wamelewa. Hawataki kuenda shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta.
Kama Zimbabwe, tusielekee hapo.”
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake
visawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Hwavutia sana wanamitindo
nchini Zimbabwe kwa mavazi yake. Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo
zake ,Khalil Parbhoo anasema: “Bado huavlia kama mabwana wa Uingereza
–hivyo ndivyo anavyopenda."
8) Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi
Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika
mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame
Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru;Kwame
aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya
jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake
ya kwanza ni kutoka katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika
Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa
gerezani-shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula”
alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini
Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.
0 comments:
Post a Comment