Friday, 21 February 2014

CCM YASISITIZA MGIMWA NI MTANZANIA

Filled under:


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mgombea ubunge wa Kalenga kwa tiketi ya chama hicho, Godfrey Mgimwa, ni raia wa Tanzania anayestahili kuwania nafasi hiyo.

Kauli ya chama hicho imekuja baada ya kuwepo kwa pingamizi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu uraia wa Mgimwa.

Pingamizi la CHADEMA lilidai kwamba Mgimwa si Mtanzania, hivyo hastahili kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment