Maskofu wakuu katika kanisa moja nchini Uingereza
wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa
za jinsia moja,na kusema kuwa hawatakubali viongozi wa dini masenge
kwenda kinyume na maagizo hayo.
Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana
wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini
kwa maelewano kwamba hawatashiriki ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia wamepiga
marufuku maombi yoyote maalum kwa wanadoa wa jinsia moja licha ya ripoti
rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza
kufanya hivyo iwapo wanajihisi.
Hatahivyo amesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasio rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
0 comments:
Post a Comment