NAFASI ZA KAZI IDARA YA
UHAMIAJI
TANZANIA....IMMAGRATION
SERVICES DEPARTMENT JOB
VACANCIES...!
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZIUHAMIAJI
TANZANIA....IMMAGRATION
SERVICES DEPARTMENT JOB
VACANCIES...!
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anatangaza
nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji.
Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa
Uhamiaji, Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa
Uhamiaji.
A. MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI
(Nafasi 70)
SIFA ZINAZOHITAJIKA
Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fanizifuatazo: Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo. Awe na umri usiozidi miaka 35
MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia naKutoka Nchini Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa
B: KOPLO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:
- Awe amehitimu Kidato cha
- Sita na kufaulu
- Awe na umri usiozidi miaka
C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (Nafasi100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:
- Awe amehitimu Kidato cha
- Nne na kufaulu
- Awe na umri usiozidi miaka
D: SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO
WA UHAMIAJI
Cheti cha Ufundi Stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya Umeme na Mitambo
Cheti au Stashahada ya Uhaziri (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali Cheti au Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu(Certificate in Records Management) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statatistics ) Kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali. Cheti au Stashahada ya
Vyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operations) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali Cheti au Stashahada katika fani ya Uchapaji (Printing) Ujuzi na Elimu ya Kompyuta na Uandishi mzuri utazingatiwa Cheti cha Ufundi Makanika,Kozi ya juu ya
Udereva na Leseni ya Udereva Daraja C
E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
Kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji Kuandika Hati mbalimbali
za Uhamiaji Kufanya doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu
zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakaman pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini Kufanya ukaguzi kwenymahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara. Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka
mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji. Kufanya matengenezo ukarabati wa mitambo na
vitendea kazi vya Uhamiaji Kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji
F. MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATISHO VIFUATAVYO:
Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo kwa mujibu wa sifa zilizotajwa Nakala ya Cheti cha KumalizaElimu ya Msingi Nakala ya Cheti cha KuzaliwaPicha mbili (Passport Size) Barua ya Utambulisho kutokakwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
G. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapitie posta na barua za
maombi ziandikwe kwa mkono.
Maombi ya nafasi ya Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji
yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P. 9223, DAR ES SALAAM
Maombi ya nafasi ya Koplo wa
Uhamiaji na Konstebo wa
Uhamiaji yatumwe kwa:
KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P. 512, DAR ES SALAAM
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi
zote ni tarehe 27/02/2014
KUTEMBELEA WEBSITE YA UHAMIAJI. BOFYA
HAPA
0 comments:
Post a Comment