Rais Jakaya Kikwete, amesema mtandao wa majangili unajulikana na
jitihada za serikali zimefanikiwa kukamata vigogo 40 walio kwenye
mtandao mkubwa wa biashara ya nyara hizo za serikali.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC , jana asubuhi alisema watuhumiwa hao wamebainika kuwa wanajihusisha na mtandao kwenye ukanda wa Kaskazini na kwamba tajiri mkuu wa biashara hiyo naye amefahamika na kwamba anapatikana mkoani Arusha .
Akizungumza katika kipindi cha Amka na BBC , alikozungumzia ujangili, alieleza kuwa mtandao umefahamika na kwamba unahusisha matajiri na miongoni mwa watu hao 40 yupo tajiri huyo wa Arusha ambaye hakutaka kumtaja jina redioni.
“Tumeutambua mtandao huo hadi wakubwa zao ni matajari pale Arusha kuna mmoja mkubwa ambaye sitaki kumtaja jina alikuwa akiendesha biashara hiyo naye yupo kwenye kundi hili la watu 40 kazi iliyokuwa ikifanyika ni kuutambua huo mtandao kwa upana,” alisema.
Awali alisema Tanzania ilikuwa na tembo wengi barani Afrika na hata duniani wakati huo baada ya Uhuru walikuwa 350,000 na ilipofikia mwaka 1987 walipungua hadi 55,000.
Alisema hapo ndipo serikali ilipofanya maamuzi ya kuingiza jeshi katika mapambano ya kupambana na ujangili jambo lililosaidia kwa kiasi kupunguza tatizo.
Hata hivyo, alisema ilipofikia mwaka 1989 shirika linaloshughulikia haki za wanyama walioko hatarini kutoweka (CITES) ilifanya maamuzi ya kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani.
Rais Kikwete alisema kwa mambo hayo mawili ikiwamo nguvu ya jeshi kuingilia kupambana na ujangili pamoja na biashara hiyo kupigwa marufuku duniani ilisaidia kupungua ujangili na tembo kuanza kuonekana.
Alisema ilipofika mwaka 2009 hesabu ilikuwa kubwa ambapo idadi ya tembo iliongezeka na kufikia 110,000.
Alipohojiwa juu ya gazeti moja la Uingereza la Daily Maili kumuandika kuwa hajafanya jitihada za kutosha kupambana na ujangili, alisema gazeti hilo limeandika uongo na kwamba serikali imejitahidi kufanya mikakati mbalimbali kuokoa maisha ya tembo na kupunguza ujangili.
Pembe hizo za ndovu wanaouliwa Afrika soko lake lipo katika nchi za Asia ikiwamo China.
Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanywa ndiyo maana mtandao huo ambao unajihusisha na biashara ya meno ya tembo umegundulika.
Wakati Rais akiwa kwenye mkutano nchini Uingereza uliokuwa ukijadili ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, polisi mkoani Singida wamemkamata George James na vipande 21 vya meno hayo.
Polisi ilisema meno hayo yenye thamani ya Sh. milioni 43 yana uzito wa kilo 49.
MAHOJIANO NA CNN
Wakati huo huo, ujangili umemfikisha Rais Kikwete, kwenye televisheni ya CNN ya Marekani, alikohojiwa akitakiwa kueleza vita dhidi ya majangili inayofanyika nchini.
Akihojiwa na CNN jijini London juzi, alisema Tanzania imefanya operesheni nyingi dhidi ya majangili na kuhimiza haja ya mataifa makubwa kusaidia juhudi za kupambana na ujangili huo.
Akijibu maswali ya Christiane Amanpour wa CNN, Rais alitaka dunia kuungana kusimamisha biashara ya pembe za ndovu.
Alieleza kuwa hatua hiyo itaondoa kichocheo cha mtu kuwaua wanyama hao
Alieleza kuwa wakati wa uhuru walikuwepo tembo 350,000 kabla ya kuibuka wimbi la ujangili mkubwa ulioiachia nchi tembo 13,000 pekee.
AHADI YA MSAADA
Akijibu swali kama kuna ahadi yoyote aliipata katika mkutano juu ya ulinzi wa wanyama pori uliofanyika London juzi, Rais Kikwete aliitaja Canada kuwa imeahidi kutoa Dola milioni mbili, wakati serikali ya Uingereza imeahidi kutoa msaada.
ALICHOTARAJIA
Alieleza kuwa kitu muhimu kwake na viongozi wa Afrika ni kufahamisha kuwa ili kuupiga vita ujangili kunahitajika rasilimali watu, kuwajengea uwezo askari wa wanyama pori wa kulinda wanyama.
Rais alisema alikuwa anategemea nchi zilizoendelea hasa Uingereza na Marekani kusaidia upande wa mafunzo ya askari wa wanyama pori na pia kuwapatia vifaa.
Alitaja silaha, magari na vyombo vyenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kwamba ndicho alichotegemea kutoka kwenye mkutano huo na kwamba amepata ahadi za msaada.
AKIBA YA MENO
Rais Kikwete alisema Tanzania ina karibu tani 112 za pembe za ndovu ambazo haijajua itazifanya nini kwa sababu nchi ilizoea kuomba idhini ya kuziuza hatua ambayo inahitaji kuangaliwa upya.
UMASKINI
Akijibu swali kuhusu kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa kulinganisha na nchi nyingine katika kipindi cha miaka michache iliyopita lakini nchi ikiwa na maskini wanaoishi kwenye ufukara, alisema “uchumi unakua kwa asilimia 70 lakini umasikini unapungua kwa asilimia 2.0” akiongeza kuwa mchango huo wa ukuaji wa asilimia 7.0 umetokana na sekta ya mawasiliano na usafiri.

Chanzo:nipashe
0 comments:
Post a Comment