Tuesday, 7 January 2014

ZITTO ASHINDA MAHAKAMANI,WAFUASI WATWANGANA NGUMI

Filled under:




Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameshinda maombi yake dhidi ya Chama hicho mahakamani.
 
Katika maombi Hayo namba 1 ya Mwaka 2014, Zitto ambaye Pia Ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, aliiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kuizua Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.
 
Zitto kupitia  Wakili Albert Msando alikuwa akiiomba Mahakama itoe zuio hilo la muda hadi kesi yake ya ya Msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
 
Katika uamuzi wake jana, Mahakama Kuu ilikubaliana na maombi ya hoja za Zitto  kutoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema  au Chombo Chake Chochote cha uamuzi kumjadili  kutoa uamuzi wowote kuhusiana uanachama wake, Hadi kesi yake ya ya Msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa.
 
Awali, Mawakili wa Chadema wakiongozwa na Mwanasheria MKUU, Tundu Lissu  Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala walipinga maombi Hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.
 
Katika uamuzi wake, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi Hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio Hilo.
 
Matakwa hayo nikuwapo kwa mgogoro baina ya Pande Mbili, hasara au madhara yasiyoweza kufidiwa usawa katika athari  kwa Pande zote.
 
Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa iwapo Mahakama haitaingilia kati na kutoa zuio hilo, Mtoa maombi ataathirika Zaidi kuliko wajibu maombi.
 
Akijibu hoja ya Wakili Lissu aliyepinga hoja ya Mtoa maombi kuathirika pamoja na wananchi wa Jimbo kukosa uwakilishi bungeni, kuwa Hata akipoteza ubunge ,Kuvuliwa uanachama utaitishwa uchaguzi mdogo, Jaji alisema Uchaguzi mdogo Huwa unachukua mchakato mrefu.
 
Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya Sheria, kanuni, Amri na uamuzi wa kesi mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na za nje, Jaji alisema anakubaliana Mtoa maombi.
 
"Kwa hiyo ninatoa zuio la muda kaw Kamati Kuu ya Chadema au Chombo Chake Chochote cha uamuzi kwamba kisimjadili au kutoa uamuzi wowote dhidi ya mleta maombi kuhusiana na uanachama wake kusubiri kusikilizwa au kuamuriwa kwa kesi Yake ya ya Msingi," alisema Jaji huyo.
 
Kabla ya kufikia uamuzi Huo, Jaji alitupilia Mbali Hati ya kiapo kinzani ya Chadema iliyotolewa na Wakili Kibatala baada ya kuwekewa pingamizi la Wakili Msando ambaye alidai kuwa katika Hati hiyo, KUNA taarifa za kusikia ambazo hakueleza alipozitoa.

 Huku akirejea vifungu vya Sheria, kanuni, Amri za uamuzi wa Mahakama mbalimbali, alisisitiza kuwa ingawa wakili anaweza Kuapa kwa niaba ya mteja wake, lakini anapaswa kueleza Chanzo cha taarifa anazozitoa katika kiapo hicho.
 
Baada ya kutupilia Mbali kiapo hicho, Jaji alisema Hata vielelezo vya wajibu  wa Mtoa maombi yanabaki Bila kupingwa na kwamba hakuna haja ya kujadili hoja za upande wa wajibu maombi.
 
Baada ya Jaji kutoa uamuzi Huo, Zitto, aliwafuata mawakili wa Chadema na kupeana nao mikono kisha akaongozwa na walinzi wake wa Kutoka nje ya Ukumbi wa Mahakama akipitia Mlango maalumu unaotumiwa na jaji.
 
Kabla ya hukumu
 
Zitto aliyekuwa amevalia suti ya vijivu na Shati la michirizi myeupe  ya vijivu aliwasili mahakamani hapo SAA 7:45 mchana akiongozana na walinzi wake binafsi (mabaunsa), wapambe na wakili wake.
 
Baada ya kufika alikwenda katika Chumba maalumu ambako alipumzika Hadi SAA 9:45 alasiri alipoingia katika Ukumbi wa kukaa katikati ya wapambe wake Huku nyuma YAKE wakiwapo walinzi wake.
 
Jaji Utamwa aliingia mahakamani SAA 9:56 alasiri na kuanza kusoma uamuzi wake akianzia na pingamizi la Zitto kwenye Hati ya kiapo kinzani cha Chadema kisha akamalizia uamuzi wa maombi ya ya Msingi. Hukumu hiyo ilimalizika kusomwa SAA 11:10 jioni.
 
Baada ya hukumu
 
Akizungumza baada ya uamuzi Huo, Wakili Msando alisema wameupokea to Furaha uamuzi Huo wa mahakama na kwamba hiyo nai hatua mojawapo ya Haki akisema anaamini kuwa mteja wake atapata Haki anayoitafuta.
 
Hata hivyo, Lissu Rangi Kibatala kwa nyakati tofauti walisema kuwa ingawa wanakubaliana na uamuzi Huo, hajawaridhika.
 
Maombi Hayo ya Zitto yaliyotolewa uamuzi jana yanatokana na kesi ya ya Msingi aliyofungua mahakamani hapo, January 2, Mwaka Huu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu MKUU wa Chadema.
 
Katika kesi hiyo anaiomba Mahakama izuie Chama hicho, wakala wake wa vyombo vyake vya uamuzi kumchukulia hatua zozote Wala kumjadili kuhusiana na uanachama wake, Hadi hapo rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la Chadema kupinga kuvuliwa nyadhifa zake itakaposikilizwa. Kesi hiyo ya ya Msingi imepangwa kutajwa Februari 13, 2014.

Wafuasi wa Chadema wanaomuunga Mkono Zitto na  Wale wa uongozi wa Juu, jana walipambana Tena mahakamani kwa ngumi na mawe kisha kusababisha watu wawili kujeruhiwa.
 
Vurugu hizo zilitokea SAA 7.55 mchana muda mfupi baada ya Zitto kuingia mahakamani.
 
Katika vurugu hizo, Mmoja wa wafuasi hao ambaye ujaini ziwa halikujulikana Mara Moja, aliumizwa kichwani baada ya kupigwa na Jiwe na mwingine alipigwa Jiwe tumboni na kupelekwa hospitali.
Kutokana na vurugu hizo, Polisi waliyatenganisha Makundi Hayo katika sehemu tofauti ya kukaa.
 
Wakati Zitto akiwasili mahakama hapo, wafuasi wake walikuwa wakiimba `Zitto Zitto KAMA Mandela 'HALI iliyowalazimu wafanyakazi wa Mahakama kuingilia kati na kuwazuia.
 
Makundi Hayo ya wafuasi wa Chama hicho yalifika mapema SAA 6:30 mchana mahakamani hapo kusikiliza uamuzi uamuzi wake.
 
Ulinzi katika eneo  la Mahakama uliimarishwa, Makundi ya Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha Pamoja na mabomu ya Machozi walitanda sambamba na Askari wa Kikosi cha mbwa, MAGARI manane ya Polisi na matatu ya Maji ya kuwasha.
 
KAMA ilivyokuwa juzi, nai wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia Ndani ya Chumba cha Mahakama.
Baada ya mahakama kutangaza uamuzi wake, wafuasi wa Zitto walishangilia kwa nguvu na kuondoka wakiimba nyimbo za kumsifu Kiongozi huyo.
 
Mtei amwonyesha Mlango Zitto
Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde Chama Chake au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa Sasa hana Nafasi.
 
Pia ameshauri kuwa kama ana Ndoto za kuwania urais Ni Vizuri akatafute vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa Ndani ya Chadema Sasa hahitajiki.
 
Mtei alisema kuwa KAMA anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana Shida ... "Lakini huwezi kuwapeleka viongozi Wako kortini na Bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu."
 
Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali Ndani ya Chadema Rangi na kuzua mitafaruku ya hapa na pale Huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa Mwisho.

0 comments:

Post a Comment