Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na
kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick.
Mwenyekiti huyo amedai kuwa alikuwa akipata mbili tatu maeneo ya Temeke,Ndipo walikuja walikuja watu sita na kujitambulisha maafisa wa polisi,
Mwenyekiti huyo alihoji mbona kati yenu mmoja wenu ni mwanachama wa CAHADEMA,baada ya kuuliza hilo kauli hiyo iliwakera na kumvamia kwa pamoja na kumfunika usoni kisha kumpandisha gari na kuondoka nae katika eneo hilo,baada ya hapo alikutwa ametupwa maeneo ya maeneo ya ununio huku akiwa amejeruhiwa vibaya sana
kauli ya CHADEMA
Jeshi la Polisi
lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa kwa
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili ukweli ujulikane na haki
itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment