Wednesday, 8 January 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA TEMEKE ASEMA AMETEKWA NA WANACHADEMA WENZAKE

Filled under:



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick. 
Mwenyekiti huyo amedai kuwa alikuwa akipata mbili tatu maeneo ya Temeke,Ndipo walikuja walikuja watu sita na kujitambulisha maafisa wa polisi,

Mwenyekiti huyo alihoji mbona kati yenu mmoja wenu ni mwanachama wa CAHADEMA,baada ya kuuliza hilo kauli hiyo iliwakera na kumvamia kwa pamoja na kumfunika usoni kisha kumpandisha gari na kuondoka nae katika eneo hilo,baada ya hapo alikutwa ametupwa maeneo ya maeneo ya ununio huku akiwa amejeruhiwa vibaya sana

kauli ya CHADEMA

Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili ukweli ujulikane na haki itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.

0 comments:

Post a Comment