Serikali imesema kuwa hatua iliyoanzishwa na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo imeruhusu raia wake kusafari ndani ya nchi hizo kwa kutumia vitambulisho vya taifa badala ya hati ya kusafiria kuwa siyo tishio.
Pia imesema kuwa Tanzania itaendelea kujivunia
rasilimali zake zinazopatikana nchini pekee ikiwemo vivutio vilivyopo
kwenye mbuga za wanyama hatua ambayo itaendelea kuwavutia watalii wa
kigeni.
Tangu kuanzia Januari mwaka huu nchi za Rwanda,
Uganda na Kenya ambazo ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeanza
kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria kwa raia wake,
hatua ambayo wachunguzi wa mambo wanaona kuwa ni jaribio la kuimarisha
kile kinachoitwa ‘umoja wa hiari’.
Akizungumza na hilo kufuatia hatua ya nchi hizo tatu, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Afrika Mashariki, Bernard Haule alisema kuwa Tanzania haiwezi kuathirika kwa aina yoyote ile.
Alisema kuwa mfumo unaotumiwa nchi hizo bado
unakabiliwa na changamoto za kutokwenda na wakati, kwani baadhi ya nchi
zinatumia vitambulisho vya kupigia kura ambavyo havitoa taarifa sahihi
kuhusiana na raia.
“Sisi hatuna wasiwasi kabisa, wenzetu wamefanya
hivyo nadhani huo ni utashi wao na sisi tunaendelea na utaratibu wetu wa
kutoa vitambulisho kwa raia wetu. Jambo jingine linalopaswa kufahamika
ni kwamba suala la kutumia vitambulisho lipo kwenye itifaki ya pamoja ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini utekelezwaji wake bado.
0 comments:
Post a Comment