Saturday, 11 January 2014

MNYIKA ANG'ANG'ANA MAGHEMBE AJIUZULU

Filled under:

 
Mbunge  wa Ubungo (Chadema) John Mnyika, amerudia kauli yake ya kumtaka Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, kujiuzulu kutokana na tatizo la maji kujirudia katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha pamoja na Profesa Maghembe kuondoka aliwataka wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Mamlaka ya Maji na Kampuni ya Maji Jijini (Dawasa na maji Dawasco) watoe maelezo ya sababu za matatizo ya maji kurejea tena jijini.

Katika taarifa yake aliyoitoa jijini jana pia aliwataka wahusika hao wajieleze kwa umma ni kwanini wananchi wasipendekeze Rais asiwachukulie hatua kwa uzembe.

Alikumbusa kuwa  ni zaidi ya nusu mwaka umepita tangu Waziri Maghembe atoe ahadi za kurekebisha tatizo la maji lakini  ameshindwa kusimamia utekelezaji wake na kumtaka kujiuzulu.

“ Iwapo Profesa Maghembe hatajiuzulu nitaeleza hatua zaidi ambazo nitachukua,”Alisema Mnyika.

Alizitaka Dawasa na Dawasco kurejesha huduma ya maji ndani ya wiki moja hasa maeneo yaliyokuwa yanapata mgawo.

Akizungumzia viongozi hao wa mamlaka kuchukuliwa hatua alisema wanastahili adhabu kwa kuisababisha hasara kwa serikali, kuathiri uchumi wa taifa na maisha ya wananchi waliokosa maji mara kwa mara ambayo ni huduma ya msingi ya binadamu na malighafi muhimu ya uzalishaji.

Taarifa ya Mnyika, ilikumbusha kuwa Februari mwaka jana aliwasilisha hoja binafsi kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji Dar es Salaam na kupendekeza Bunge kuingilia kati ili kuisimamia serikali kuchukua hatua za haraka.

“Iwapo hoja hiyo ingejadiliwa na maazimio yote kutekelezwa matatizo ya maji Dar es Salaam yangekuwa yamepungua katika maeneo kutokana na hatua nilipendekeza zichukuliwe.”

“Hata hivyo, badala ya kuunga mkono hoja hiyo ambayo ingesaidia kurekebisha udhaifu uliokuwepo na kumrejeshea imani kwa umma Waziri Maghembe aliondoa bungeni,”ilisema taarifa yake.

Mbunge wa Ubungo alisema baada ya Bunge Waziri Maghembe alizungumzia masuala ya maji Dar es Salaam; kupitia mikutano ya CCM akiwa kata ya Goba pia alizitaja akiwa kwenye mkutano na wafanyakazi wa Dawasa na Dawasco na kueleza hatua za haraka ambazo angesimamia katika kushughulikia tatizo hilo.

Mnyika alisema serikali haikuchukua hatua hivyo alitangaza kuongoza maandamano ya wananchi Machi 16 2013 kwenda Wizara ya Maji ili kupata majibu na kuisimamia serikali kuchukua hatua za haraka.

“ Hata hivyo maandamano hayo yalizuiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu zisizo za msingi na kuombwa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,”iIlisema taarifa ya Mnyika

Alisema maandamano hayo yangefanyika na hatua kuchukuliwa matatizo yangepungua tofauti na ilivyo sasa, hivyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima,  anapaswa kueleza umma lini rufaa hiyo itashughulikiwa maandamano yaweze kufanyika wananchi wapate majibu ya hatua za haraka nilizopendekeza ndani na nje ya Bunge.

Alizitaka mamlaka ya maji na kampuni ya maji  jijini kuhakikisha kwamba katika kipindi kisichozidi wiki moja huduma za maji zinarejea katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata huduma hiyo kwa mgawo.
 
DESEMBA 26, 1996 mwili wa mtoto JonBenet Patricia Ramsey aliyekuwa na umri wa miaka sita wakati huo, ulikutwa ghorofa ya chini (Basement) ya nyumba yao, ikiwa ni karibu saa nane tangu aliporipotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.
Tukio hilo liliibua hisia tofauti miongoni mwa jamii ya Wamarekani kwa sababu, JonBenet pamoja na kuwa na umri mdogo, lakini alikuwa anashikilia mataji takriban 50 ya urembo kwa watoto aliyoshiriki katika maeneo tofauti nchini humo.
Jina la JonBenet ni muunganiko wa majina ya baba yake John Bennet Ramsey (53), bilionea na mmiliki wa viwanda nchini Marekani na mama yake Patricia (Patsy) Ramsey ambaye naye aliwahi kushikilia taji la West Virginia mwaka 1977, Marekani. Kutokana na mama yake kushiriki mashindano ya urembo enzi ya usichana wake, vivyo hivyo alitaka na mwanaye pia afuate nyayo zake.
Awali, John alifunga ndoa na mwanamke aliyetajwa kwa jina la Lucinda Pasch Ramsey “Cindy” Julai 1966 na walibahatika kupata watoto watatu ambao ni Elizabeth Ramsey ambaye alizaliwa mwaka 1969, lakini alikuja kufariki Agosti mosi, 1992 kwa ajali ya gari huko Illinois, Melinda Ramsey alizaliwa mwaka 1972 na John Andrew Ramsey aliyezaliwa mwaka 1976. Kati ya mwaka 1977 na 1978 John Bennet Ramsey na mkewe Lucinda Pasch Ramsey “Cindy” waliaachana kisheria.
Novemba 5, mwaka 1980 John Ramsey alifunga ndoa na Patricia Paugh Ramsey (Patsy) huko Atlanta Georgia na mtoto wa kwanza, Burke Hamilton Ramsey alizaliwa mwaka 1987 na mtoto wao wa pili na wa mwisho JonBenet Ramsey, alizaliwa Agosti 6, 1990 huko Atlanta Georgia.
Alikuwa ni Patsy Ramsey mama wa mtoto JonBenet aliyeamka asubuhi na mapema, siku ya Desemba 26, 1996 na kukutana barua ndefu sebuleni yenye kurasa tatu iliyoandikwa kwa mkono, ikiwafahamisha kwamba mtoto wao JonBenet ametekwa nyara na watekaji hao walikuwa wanahitaji dola za Marekani 118,000 ili wamrejeshe akiwa salama.
Pia barua hiyo ilikuwa na tishio la kutahadharisha familia ya JonBenet kwamba iwapo watawajulisha polisi au FBI, binti yao hatakuwa salama.
Kwa mujibu wa Patsy Ramsey, haraka sana alianza kuchunguza hapo nyumbani kwao akianzia chumbani alipolala JonBenet na kwingineko, lakini hakuweza kumwona mwanaye zaidi ya kumkuta mwanaye mwingine wa kiume aitwae Burke aliyekuwa na umri wa miaka 9, akiwa amelala.
Alikwenda kumuamsha mumewe na kumpa ile barua ya watekaji. Pamoja na kwamba barua ile ilikuwa na tishio la kuitaka familia ile kutowajulisha polisi juu ya suala lile, John Bennet Ramsey aliwajulisha polisi  na wakati huo huo aliwasiliana na meneja wa benki anakoweka fedha zake ili akamilishe mipango ya kumpatia hizo fedha zinazotakiwa na watekaji haraka iwezekanavyo.
Polisi walifika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kujulishwa. Utekaji nyara na mauaji si jambo la kutarajiwa sana katika mji wa Boulder, Colorado. Ukweli ni kwamba, hadi kufikia tarehe hiyo ya 26, Desemba, kulikuwa hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuuawa kwa zaidi ya mwaka.
Polisi wa Boulder walilazimika kuomba msaada kutoka kwa polisi wa Denver na FBI. Muda si mrefu polisi wale walifika na kwa kushirikiana na FBI walikagua nyumba yote iliyokuwa na vyumba 15, huku ikiwa imezungukwa na eneo la bustani la eka mbili, lakini hawakumpata mtoto JonBenet.
Walipomaliza kukagua nyumba hiyo waliihoji familia ya JonBenet kwa saa kadhaa na pia walikaa na familia hiyo kwa muda kiasi wakisubiri simu kutoka kwa watekaji, ambapo hata hivyo hakuna simu iliyopigwa na ilipofika saa saba mchana maofisa polisi na FBI waliondoka katika eneo la tukio wakiacha maagizo kwa familia ya John Ramsey kuendelea kumtafuta mtoto wao JonBenet, palepale kwenye eneo la nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa maelezo ya John Ramsey ni kwamba aliendesha msako mkali katika nyumba yao kwa dakika 15 baada ya polisi kuondoka. Msako huo ulijumuisha kila kona ya nyumba ile na hatimaye walimkuta mtoto wao JonBenet akiwa amekwishauawa. Mwili wake waliukuta ukiwa kwenye chumba ambacho kilikuwa hakitumiki na ambacho vioo vyake vya madirisha vilikuwa vimevunjika.
Ramsey aliuchukuwa mwili wa mwanaye na kukimbia nao hadi sebuleni ambapo aliulaza karibu na mti wa Mkirismas ambapo mkewe alijaribu kutoa huduma ya kwanza ya kumpulizia hewa mdomoni akidhani labda mtoto amepoteza fahamu tu, lakini kumbe alikwishafariki.
Wakati huo huo majirani waliokuwa pale nyumbani kuwafariji walipiga simu ya dharura na kuwajulisha polisi juu ya kupatikana kwa mtoto JonBenet, akiwa amekwisha kufa.
Kitendo cha Ramsey  kuuondoa mwili wa mwanae kutoka katika eneo la tukio kwa sababu ya kutaka kuokoa maisha yake, kinaweza kueleweka kwamba alikuwa na nia nzuri juu ya maisha ya mwanaye, lakini kwa upande mwingine kitendo kile kilikuwa kimetibua kabisa uchunguzi ambao ulitakiwa ufanyike palepale kwenye eneo la tukio kabla ya kuondoa mwili huo.
Hivyo kitendo cha kuondoa mwili huo kilisababisha kikosi cha uchunguzi kushindwa kufanya uchunguzi wa mwili huo ukiwa kwenye eneo la tukio.
Hata hivyo, Polisi waliuchukua mwili wa mtoto na kuondoka nao na baadaye, usiku huo mwili huo ulifanyiwa uchunguzi katika ofisa ya uchunguzi wa vifo ya wilaya.
Siku iliyofuata asubuhi daktari bingwa anayeshughuka na uhalifu dhidi ya watoto Dk. Charles Wecht alisema JonBenet alifariki saa nne usiku. Alieleza kwamba kifo chake kilitokana na kuzibwa pumzi, kupigwa kichwani na pia alikuwa amenajisiwa.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/mauaji-ya-ajabu-ya-mtoto-jonbenet-ramsey#sthash.yIcbfg82.dpuf

0 comments:

Post a Comment