Mwanadada anayetamba kimataifa kupitia kazi zake, Baby Joseph ‘Baby
Madaha’, amedai mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul
‘Diamond Platinum’ hamuwezi kwa lolote kwani yeye yupo kimataifa zaidi.
Kauli hiyo ya Baby Madaha, imekuja baada ya msanii huyo kuulizwa
anakichukuliaje kiwango cha Diamond katika tasnia ya muziki huo na
mtangazaji wa East Africa TV.
Alisema yeye yupo kimataifa zaidi na Diamond ni wa hapa hapa
Tanzania, hivyo sio rahisi kufananisha kiwango chake na msanii huyo,
ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake ‘My Number One’.
“Diamond ni wa hapa hapa, mimi huwezi kunifananisha naye, mimi wa
kimataifa, kwanza mimi nina kipaji cha kuigiza, yeye ni msanii wa kuimba
pekee, hana lolote zaidi ya kuuza sura mjini,” alisema.
Mwanadada huyo ambaye nyota yake ilianza kung’ara kwenye shindano la
kusaka vipaji nchini la Bongo Stars Search (BSS), mwaka 2008, ameingia
kwenye bifu na mkali huyo baada ya kurushiana maneno yasiyofaa katika
vyombo mbalimbali vya habari.
“Diamond hana lolote, labda anapata shoo nyingi kutokana na uongozi
wake kumpigia ‘promo’ ya kutosha, lakini ukweli kipaji hana, huwezi
kulinganisha kipaji cha Alikiba na Diamond, Alikiba anaimba sana na ana
kipaji ila hana ‘promo’,” alisema.
0 comments:
Post a Comment