Monday, 27 January 2014

KWA WALE WASHABIKI WA MAN U,ANGALIA FAIDA NA HASARA ZA USAJILI WA FEDHA NYINGI

Filled under:



Ferguson ambaye bado ni mkurugenzi katika klabu ya Manchester United alisema hivi sasa klabu ya Manchester City ndiyo inayoonekana kama ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, lakini anaona itashindwa kufanya vizuri katika mechi za mwishoni mwa ligi.

Wiki iliyopita, kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson alisema timu sita ikiwamo Manchester United ndiyo zenye nafasi kubwa ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England ingawa hakuitaja Liverpool.
Ferguson ambaye bado ni mkurugenzi katika klabu ya Manchester United alisema hivi sasa klabu ya Manchester City ndiyo inayoonekana kama ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, lakini anaona itashindwa kufanya vizuri katika mechi za mwishoni mwa ligi.
“Ligi ilivyo bado siyo nyepesi kutwaa ubingwa, unaweza kusema hivi sasa Manchester City wanacheza vizuri, lakini timu ambayo inaongoza msimamo wa ligi hivi sasa ndiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa,” alisema Ferguson.
Alisema, “Arsenal ndiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, lakini nashangaa watu wengi hawaipi nafasi, lakini wamesahau tupo katika mzunguko wa pili wa ligi na bado wanakaa kileleni.”
Ferguson alisema, “Pia zipo timu kama Chelsea, Everton na Tottenham ambazo zinafanya vizuri na zina nafasi ya kutwaa ubingwa, Manchester United kila msimu huwa inafanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi kwa hiyo ninatarajia itafanya vizuri pia kwani ina falsafa na historia nzuri.”
Hata hivyo Manchester United ambayo hivi sasa ipo chini ya kocha mpya David Moyes imekuwa ikisuasua katika Ligi Kuu ya England na hivi sasa inashika nafasi ya saba.
Pia Manchester United imetolewa katika mashindano ya kombe la FA na kombe la ligi (Capital One) ingawa bado wapo katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kutokana na Manchester United kushindwa kupata matokeo mazuri, hivi sasa zipo taarifa mbalimbali kwamba kocha Moyes anaweza kutimuliwa. Hata hivyo kocha Alex Ferguson amemtetea kocha huyo na kusema hatakiwi kutimuliwa ila anahitaji kupewa muda na kufanya usajili.
Tayari kocha Moyes ameanza kusajili, ambapo Manchester United imekubali kumwaga fedha na kumsajili kiungo mshambuliaji Juan Mata kutoka Chelsea ambaye gharama yake ni pauni 37milioni, ambazo ni fedha nyingi.
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji 10 ambao United ilitumia fedha nyingi kuwasajili, ambapo gazeti la Sportstmail linaelezea namna wengine walivyokuwa msaada na wengine kushindwa kuwa msaada kwa klabu hiyo.

1.Dimitar Berbatov Pauni 30.75mil (Tottenham)
Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson hakuwa wazi namna alivyoweza kumnasa mshambuliaji huyo wa Bulgaria, japokuwa rekodi yake ya mabao 56 katika mechi 149 ilikuwa ya kuvutia. Lakini pamoja na ukubwa wa umbo lake, mchango wake haukuwa kama kocha Ferguson aivyotaka, kwa hiyo hakuwa msaada kwa klabu hiyo.

2. Rio Ferdinand Pauni 29 mil (Leeds)
Usajili makini, kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kusajili beki ni kitu kisichoeleweka, lakini Rio amefanikiwa kucheza mechi 300 kwa United na amekuwa ni mtu muhimu katika muda wote katika klabu ya Manchester United. Ni msaada kwa klabu ya Manchester United.

3. Juan Sebastian Veron pauni 28 mil (Lazio)
Ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu. Alianza vizuri, lakini kukosa kwake nidhamu ya mchezo wa United, kocha Ferguson alishindwa kumvumilia akamtimua kwa hiyo hakuwa msaada kwa klabu hiyo.

4. Marouane Fellaini Pauni 27.5 mil (Everton)
Ndiyo kwanza mwanzo, amekuwa akisumbuliwa na majeraha, lakini hakuna ubishi kwamba ameanza kwa kiwango cha chini. Yalitegemewa mambo mengi makubwa kutoka kwake, lakini ameshindwa kuthibitisha kwamba alistahili kununuliwa kwa fedha hiyo. Mpaka sasa siyo msaada kwa Manchester United.

5. Wayne Rooney Pauni 27 mil (Everton)
Pamoja na mafanikio na matatizo yake yote bado unaweza kujiuliza, je amefikia katika kiwango chake cha juu cha kusema kwamba ni usajili sahihi. Rooney ni msaada mkubwa kwa Machester United.

6. Robin van Persie Pauni 24 mil (Arsenal)
Ni jambo zuri kusikia jinsi walivyoangalia usajili wa sasa, lakini kwa United kuna pointi kadhaa za mafanikio kwake. Msimu uliopita Van Persie alitoa mchango mkubwa kwa Manchester United na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, ingawa msimu huu amekuwa akisumbuliwa na hali ya kuwa majeruhi. Ni msaada kwa Manchester United.

7. Anderson Pauni 20 mil (Porto)
Alipoteza kiwango chake na kujikuta akikaa benchi kuliko vile ilivyotegemewa. Amekuwa akitumika kwa baadhi ya mechi, lakini kipaji chake hakijatumiwa vizuri katika klabu ya Manchester United kwa hiyo anaonekana hajatoa msaada wa kutosha katika klabu hiyo.

8. Ruud van Nistelrooy Pauni 19 mil (PSV Eindhoven)
Tabia yake katika msimu wa mwisho ndani ya United haikueleweka. Alikuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao mengi katika klabu hiyo. Bahati mbaya alifunikwa na uwepo wa Cristiano Ronaldo ambaye alifunga mabao mengi zaidi yake. Alikuwa msaada kwa Manchester United.

9. David de Gea Pauni 18 mil (Atletico Madrid)
Alianza kwa taabu Ligi Kuu England, lakini sasa ameonyesha ukomavu na kuwa shujaa mzuri golini. Mpaka sasa kipa huyu ni msaada kwa Manchester United ingawa ana makosa madogo madogo yanayosababisha anafungwa mabao mepesi.

10. Michael Carrick Pauni 18 mil (Tottenham)
Pigo kwake ni fainali ya Ligi ya Mabingwa 2009 dhidi ya Barcelona, lakini Carrick ni usajili bora wa United. Katika misimu saba aliyokuwa na klabu hiyo amecheza zaidi ya mechi 40 na anathaminiwa na kukumbukwa pale United inapopwaya kwenye kiungo kutokana na kukosekana kwake uwanjani. Carrick ana msaada mkubwa katika klabu ya Manchester United.

0 comments:

Post a Comment