Monday, 9 December 2013

UONGOZI WA CHADEMA MKOANI SINGIDA UMEMPA SIKU 14 WILFRED KITUNDU KUOMBA RADHI

Filled under:



Mjini Singida, Baraza la Uongozi mkoani Singida, limemtaka aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa huo, Wilfred Kitundu kuomba radhi ndani ya siku 14 kutokana na kutoa taarifa ya uongo, uzushi na upotoshaji mkubwa wakati akitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo. 

Taarifa ya Baraza la Uongozi ilisema asipotekeleza agizo hilo, atavuliwa uanachama. Akisoma taarifa hiyo, Kaimu Mwenyekiti, Shaaban Limu alisema tuhuma zilizotolewa na Kitundu kuwa uamuzi uliotolewa na Kamati Kuu ya kuwavua uongozi kina Zitto na wenzake ni za kipuuzi ni zake binafsi na si za Chadema.

0 comments:

Post a Comment