Friday, 29 November 2013

MALAWI NA TANZANIA YAWASILISHA USHAHIDI WA UMILIKI WA ZIWA NYASA

Filled under:



                               Mwisho wa mpaka wa ziwa nyasa


Malawi na Tanzania zimewasilisha ushahidi na majibu ya maswali kuhusu umiliki wa maeneo kwenye Ziwa Nyasa, kwa jopo la wasuluhishi linaloongozwa na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano.

Wasuluhishi hao walizitaka Malawi na Tanzania kutoa majibu ya maswali manne muhimu, wakati wakiwasilisha ushahidi wao kuhusu umiliki wa ziwa hilo wenye mgogoro.
Mgogoro huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi bila kushauriana na Tanzania kutoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Malawi la  Nyasa Times, msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Malawi, Quent Kalichero alithibitisha Jumatano wiki hii kwamba nchi hiyo imewasilisha majibu ya maswali hayo na ushahidi uliohitajika.

“Waziri wetu amewasilisha taarifa maalumu ya maandishi kwa wasuluhishi na kwa sasa yuko nchini Msumbiji, kwa ajili ya suala hilo,” alisema Kalichero juzi.
Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Maputo, Msumbiji ikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mazungumzo na wasuluhishi, marais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano na wa Botswana, Festus Mogae jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mkutano huo wa Jumatatu mjini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe aliwaeleza wanahabari kwamba mazungumzo baina ya Rais Kikwete na wasuluhishi hao yalihusu zaidi ushahidi wa Tanzania katika suala la umiliki wa Ziwa Nyasa.
Pia alithibitisha kwamba Tanzania ilikuwa tayari  kuwasilisha ushahidi wake kwa sekretarieti ya ofisi ya waliokuwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) inayoongozwa na Chissano, Jumatano iliyopita.

Baada ya mkutano huo wa Jumatatu, Membe alieleza kwamba nchi zote husika, yaani Tanzania na Malawi zinatakiwa kuheshimu maagizo na kuwasilisha ushahidi huo kwa wakati, na kuwaachia wasuluhishi kazi ya kupitia na kutekeleza wajibu wao wakiwa wamepewa muda unaofikia mwaka mmoja kupata suluhu.

Wasuluhishi hao wa SADC, Chissano na Mogae waliwasili jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mgogoro huo, kama walivyofanya kwa Malawi Julai mwaka huu.
Julai mwaka huu, Rais Joyce Banda wa Malawi alinukuliwa akisema kuwa nchi yake haina nia ya kulegeza kamba katika mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Tanzania.

Alitoa msimamo huo baada ya kukutana na Chissano wa Msumbiji na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ambao ni wajumbe maalumu wa Jumuiya ya SADC katika mgogoro huo.

Posted By Unknown21:58

BERLUSCONI (WAZIRI MKUU WA ITALY) ATIMULIWA BUNGENI

Filled under:








Bunge la Italy limemtimua Silvio Berlusconi aliyehudumu kwa mihula mitatu kama Waziri Mkuu lakini tajiri huyo ameapa kuendelea na siasa.

Seneti ilipiga kura wiki hii kumuondoa katika bunge kwa sababu ya kushitakiwa kwa makosa ya kodi.

Berlusconi alihutubia wafuasi wake Jumatano nje ya nyumba yake Romani Palazzo akiwaambia kuwa ni siku ya kuhuzunikia demokrasia  lakini akawasihi kuendelea kuitetea demokrasia.

Posted By Unknown21:28

BAREGU AIASA CHADEMA IKUMBUKE NA MEMA YALIYOFANYWA NA ZITTO KABWE

Filled under:





Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili."Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama," Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.

Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa 
Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
 
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho

Posted By Unknown06:44

Thursday, 28 November 2013

NELSON MANDELA YUNGALI TAABANI

Filled under:








Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela yupo katika hali thabiti lakini mahututi, ikiwa ni zaidi ya miezi miwili baada ya kurudi nyumbani kufuatia matibabu ya maambukizo ya mapafu.

Serikali ya Afrika Kusini ilitoa taarifa baada ya  Rais Jacob Zuma kumtembelea shujaa huyo wa kupinga ubaguzi nyumbani kwake Jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa , rais Zuma aliwasilisha salamu za pole kutoka kwa raia wote wa Afrika Kusini na kumpa tuzo kutoka taasisi ya Mahathir Global Peace Foundation, ambayo aliipokea kwa niaba yake huko Malaysia.

Hapo jana mke wake wa zamani Winnie Mandela aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiongozi huyo wa zamani yungali mgonjwa sana na hawezi kuzungumza kwa sababu kuna mipira inayotumiwa kuvuta maji kutoka mapafu yake. 










Posted By Unknown06:15

NELSON MANDELA YUNGALI TAABANI

Filled under:






Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela yupo katika hali thabiti lakini mahututi, ikiwa ni zaidi ya miezi miwili baada ya kurudi nyumbani kufuatia matibabu ya maambukizo ya mapafu.

Serikali ya Afrika Kusini ilitoa taarifa baada ya  Rais Jacob Zuma kumtembelea shujaa huyo wa kupinga ubaguzi nyumbani kwake Jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa , Rais Zuma aliwasilisha salamu za pole kutoka kwa raia wote wa Afrika Kusini na kumpa tuzo kutoka taasisi ya Mahathir Global Peace Foundation, ambayo aliipokea kwa niaba yake huko Malaysia.

Hapo jana mke wake wa zamani Winnie Mandela aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiongozi huyo wa zamani yungali mgonjwa sana na hawezi kuzungumza kwa sababu kuna mipira inayotumiwa kuvuta maji kutoka mapafu yake.

Posted By Unknown06:02

KONTENA LENYE FUTI 40 LIKIWA NA PEMBE ZA NDOVU LAKAMATWA ZANZIBAR

Filled under:







Vikosi vya ulinzi na usalama zanzibar kwa kushirikiana na raia wema wamefanikiwa kukamata kontena la futi 40 likiwa na pembe za ndovu zilizohifadhiwa katika mabaki ya mazao ya baharini likiwa katika mpango wa kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Malindi visiwani Zanzibar.

 Kontena hilo limekamatwa majira ya alasiri na askari wa jeshi la polisi kikosi cha kuzuia magendo-KMKM, usalama wa taifa ambao mara moja walianza kazi ya kupasua kila gunia na kufanikiwa kupata pembe za ndovu zikiwa zimehifadhiwa katikati ya mazao ya baharini maarufu kwa jina la Shell.

Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa maliasili na utalii, Khamis Kagasheki amesema wakati umefika kwa Watanzania kupiga vita vitendo vya ujangili vinavyofanywa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi bila ya kutafakari kuwa vitendo hivyo vitawamaliza wanyama ambao ni maliasili ya taifa.

Wakati huo huo waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum, Haji Omar Kheir amesema watu waliohusika na tukio hilo watafikishwa katika vyombo vya sheria baada ya kukamilika kwa taratibu za uchunguzi na kushtakiwa kwa sheria ya uhujumu uchumi.

Hii ni mara ya pili kukamatwa kwa nyara za serikali katika kipindi cha miaka miwili katika bandari ya Malindi mjini Zanzibar ambapo kontena la futi 20 lilikamatwa likiwa katika mpango wa kusafirishwa kuelekea nchini China.

Posted By Unknown05:47