Rais wa zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela yupo katika hali thabiti lakini mahututi, ikiwa ni zaidi ya
miezi miwili baada ya kurudi nyumbani kufuatia matibabu ya maambukizo ya
mapafu.
Serikali ya Afrika Kusini ilitoa taarifa baada ya Rais Jacob Zuma kumtembelea shujaa huyo wa kupinga ubaguzi nyumbani kwake Jumatatu.
Kwa mujibu wa taarifa , Rais Zuma aliwasilisha salamu za pole kutoka kwa raia wote wa Afrika Kusini na kumpa tuzo kutoka taasisi ya Mahathir Global Peace Foundation, ambayo aliipokea kwa niaba yake huko Malaysia.
Hapo jana mke wake wa zamani Winnie Mandela aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiongozi huyo wa zamani yungali mgonjwa sana na hawezi kuzungumza kwa sababu kuna mipira inayotumiwa kuvuta maji kutoka mapafu yake.

0 comments:
Post a Comment