Monday, 17 February 2014

KESI YA LULU MICHAEL YAPIGWA KALENDA

Filled under:



KESI inayomkabili staa wa sinema za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ dhidi ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba imeunguruma leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku mtuhumiwa akikiri baadhi ya mashtaka.

Lulu alikiri mbele ya Jaji Temba kuwa alikuwa  na uhusiano wa kimapenzi na  marehemu kanumba ,pia alisema kulitokea kutoelewana baina yao ndipo ulitokea ugomvi  na kusababisha kifo,pamoja na hayo yote Lulu alikana shitaka hilo la uuaji.
Hati ya mashitaka ilisomwa ilisoma na Wakili Mwandamizi mbogo alidai kuwa April7,2012,Sinza Vatikan,Jijini Dar es Salaam,Mshitakiwa alimuua Steven Kanumba bila kukusudia'

Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo watakapojulishwa na mahakama tarehe ya kusomwa kwa shitaka lake la kuua bila kukusudia.

0 comments:

Post a Comment