Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akisoma karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati Msoga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
Mama Salma Kikwete akiweka kura yake kwenye sanduku la kupigia kura kwenye kituo cha Zahanati Msoga.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Ndugu Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1na kusema kuwa Chama chake kitakubali matokea yeyote na pia kama watashindwa watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi Mtendaji Kata namba 1, Bwilingu.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Aziza mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsaidia Baba yake kuweka kura kwenye sanduku la kura ,Ridhiwani alipigia kura yake kwenye kata ya Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze Ndugu Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbali mbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.
wananchi wa jimbo la Chalinze wamemaliza kupiga kura hivi punde na tayari baadhi ya vituo matokeo yameanza kujulikana huku katika matokeo hayo ambayo si rasmi mgombea wa CCM Ridhiwani Jakaya Kikwete anaendelea kuongoza huku vyama vingine vikimfuata kwa mbali zaidi .
Hata hivyo zoezi hilo limefanyika katika hali ya amani na utulivu na hadi sasa wananchi wameendelea kusubiri matokeo hayo kwa hamu kubwa na baadhi ya vituo ambavyo matokeo yameanza kujulikana wafuasi wa CCM wameanza kushangilia .
Mbali ya wafuasi wa CCM kuonyesha kuanza kushangilia bado wafuasi wa vyama vikuu kama Chadema na CUF wameendelea kujipa matumaini makubwa ya kushida katika uchaguzi huo na kuwa mwisho wa zoezi la kuhesabu kura ndipo watakapo jua mbichi na mbivu katika mchakato huo
Tayari Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Bw Ramadhani Mgaya ametangaza msimamo wa chama chake baada ya matokeo hayo kutangazwa kwa kudai kuwa atakuwa tayari kukubali matokeo hata kama atashindwa katika uchaguzi huo .
Mgaya ambae amekuwa mwanasiasa wa kwanza wa vyama vya upinzani kuueleza umma kuwa yupo tayari kwa matokeo hayo na kutangaza kujipanga kwa mwakani 2015 .
Wakati mgombea huyo wa AFP akieleza hayo kwa upande wa mgombea wa CCM Ridhiwan Kikwete yeye leo amefanya kituko cha karne baada ya kujipigia kura katika zoezi hilo na kisha karatasi hiyo ya kupigia kura kumpa mtoto wake mwenye miaka chini ya minne kuitumbukiza katika kisanduku cha kuhifadhia kura
uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Marehemu Said Bwanamdogo aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu .
0 comments:
Post a Comment