KUWA mrembo ni pamoja na kujikubali jinsi ulivyo na jinsi
utakavyojiweka soap soap Hata mtu akikupenda akupende jinsi ulivyo.
Pamoja na hayo kumekuwa na mambo mbalimbali yanayofanywa na baadhi
ya wanawake au wasichana kwa lengo la kufanikisha azma mbalimbali.
Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali
ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata
kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.
Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje
ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.
Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo
ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa
mwanamke na hata kuwa na mnato.
Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa
kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya
Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo
wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho
si kweli.
Mtaalam huyo Anasema Sabuni hizo
zinapunguza tu majimaji yaliyo sehemu za
siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume
kupata ugumu kwenye muingiliano kwa vile
mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni
hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.
Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa
magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani
ukeni lakini haiwezi kurejesha hali ya
maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika
hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi
kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa
kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na
matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na
madhara makubwa kwao.
Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya
Dodoma, Fredrick Luyangi anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi
ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa
taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha
sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa
zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali
inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.
Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina
madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.
Jamani wanawake wenzangu tubadilike Kuna wengine wameshazaa zaidi ya mara mbili lakini bado wanahangaika
kurudisha maumbile yao yawe madogo na kuhangaika na kila aina ya sabuni
inawezekana kweli katika hilo?
Chanzo;sifa yetu
Chanzo;sifa yetu
0 comments:
Post a Comment