Shirika la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na
familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370
kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.
Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za
kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa
siku ya tano bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi
uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia
kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth
mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za
watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana
kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa
taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano
wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege
zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata
chochote.
0 comments:
Post a Comment