Saturday, 15 March 2014

TUME YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAFTARI LA WAPIGA KURA LITAKALOTUMIKA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

Filled under:

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akisoma taarifa ya tume mbele ya waandishi wa habari inayohusu ufafanuzi kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura litakalotumika  katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Kalenga,kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Himid Mahamoud Himid na upande wa kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akibadilishana mawazo kabla ya kujibu swali kwa waandishi wa habari ambao waliuliza kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na daftari la kudumu na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Himid Mahamoud Himid.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Jaji John Joseph Mkwawa akizungumzia suala zima la vyama kuwa makini siku ya kupiga kura kwani hakutotakiwa kuwe na alama ama kielelezo cha chama fulani katika siku hiyo,kushoto kwake ni Profesa Amon Chaligha .
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana suala la takwimu za daftari la kupiga kura pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu Julius Malaba na Dk.Sist Cariah Naibu Katibu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Tehama ambapo wapiga kura ambao taarifa zao zimetokea zaidi ya mara moja  waliondolewa kwenye daftari hilo na ni wapiga kura hao kwa idadi ni 142.
Baadhi ya maofisa wa Tume ya Uchaguzi wakisikiliza kwa makini kikao cha Tume ya Uchaguzi na Waandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa juu ya daftari la kudumu litakalotumika kwenye uchaguzi wa ubunge Kalenga siku ya tarehe 16 Machi 2014 ambapo taarifa za uhakiki zilizofanyika  zilikuwa 149 tu na wapiga kura walioongezeka  katika daftari lililotumika  katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 ni 7 tu na sio 600 kama ilivyoripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari.

0 comments:

Post a Comment