Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, jana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba.
Akitangaza matokeo hayo saa 12:07 jioni Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema Sitta alimshinda mpinzani wake, Hashim Rungwe Sipunda kwa kupata kura 487 (asilimia 86.5) dhidi ya kura 69 (asilimia 12.3) za mpinzani wake.
Dk. Kashililah alisema kuwa Bunge hilo lilikuwa na wapiga kura 629, lakini waliopiga kura ni wajumbe 563 na kwamba kura zilizoharibika ni saba (asilimia 1.2).
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, ukumbi mzima wa Bunge ulilipuka kwa shangwe na vifijo, hali iliyomfanya Rungwe kuinuka katika kiti chake na kumfuata Sitta kumpongeza na kukumbatiana naye kwa furaha.
Baadhi ya wajumbe walianzisha wimbo wa “Tuna imani na Sitta, tuna imani na Sitta”.
Tukio lingine lililosisimua wajumbe ni hatua ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kumfuata Sitta na kupeana mikono.
RUNGWE ASHUKURU WAJUMBE
Baada ya matokeo kutangazwa, Rungwe aliwashukuru wajumbe waliompigia kura na kuonyesha imani juu yake na kwa wale ambao hawakumpigia ana imani siku za mbeleni watamchagua.
SITTA AMPAMBA CHENGE
Kwa upande wake, Sitta aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kwamba kimsingi uongozi unapangwa na Mungu.
Aliishukru CCM kwa kupitisha jina lake kugombea nafasi hiyo. Alisema wakati wa mchakato wa uchaguzi kulizuka maneno kwamba yeye na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, wanavutana katika kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.
Alisema yeye hana ugomvi wowote na Chenge kwani mwaka 1993 yeye (Sitta) akiwa Waziri wa Sheria na Katiba alipendekeza jina Chenge kwa Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Sitta alisema aliamua kupendekeza jina la Chenge kwasababu miaka hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa akitoka nje ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
“Mimi sina tatizo na Chenge, tumekuwa tukishirikiana sana, familia yake na yangu wana uhusiano mzuri, tatizo ni wapambe, na ndiyo maana kuna msemo kwamba wapambe nuksi,” alisema Sitta.
WALIVYOJIELEZA
Kabla ya kupigiwa kura, Sitta na Rungwe walijieleza mbele ya wajumbe wa Bunge hilo na kuahidi kuwa kama watafanikiwa kuchaguliwa watahakikisha inapatikana Katiba bora inayojibu matatizo ya Watanzania.
Rugwe alisema kama atachaguliwa atashirikiana na wajumbe kuhakikisha Katiba bora inapatikana kama wananchi wanavyotarajia.
“Nina uzoefu wa kutosha, nimekuwa mwanasiasa, mwaka 2010 niligombea urais kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na kupata wabunge wanne, kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama cha Ukombozi wa Umma,” alisema.
“Katika katiba hii wananchi lazima tuwavushe kutoka Sinai kwenda Kaanani na lazima tutafika Bahari, nimefanya biashara nikiwa na maarifa ya kutosha, sitaongoza kwa kichwa changu bali kwa kanuni zilizopo,” alisema.
Kwa upande wake Sitta alisema dira yake ni kuwa na Bunge la Katiba lenye mjadala wa kushindanisha hoja kwa hoja, maslahi ya Taifa, ili kuwaletea Watanzania ndani ya muda mfupi Katiba maridhawa inayokidhi matarajio ya wengi na inayojenga matumaini yao ya utawala bora na maendeleo endelevu kwa wote.
Sitta ambaye alikuwa akishangiliwa kwa makofi na wajumbe hao, alianza kwa kujieleza kuwa yeye ni mtu wa kujipanga kwa kuwa amegawa vipeperushi vinavyoelezea wasifu wake na kwamba amekuwa mbunge kwa miaka 29, Waziri kwa miaka 14 na Spika wa Bunge la Tisa la viwango.
“Kuniweka mie kwenye kiti hicho ni kama kumrejesha chura kwenye dimbwi la maji alilozoea ataendelea kuogelea tu, nawaahidi ikiwa kwa kudra za Mungu mkinichagua nitawatumikia kwa uaminifu, sitakubali upendeleo wa aina yoyote, nitasimamia kanuni na nina hulka ya kuwapenda ninaowaongoza, hivyo nitakuwa mtetezi wa mambo mbalimbali yatakayowafanya make vizuri Dodoma,” alisema.
Alisema lengo lake ni kuhakikisha Bunge linatunga Katiba kwa muda mwafaka na kubadili muonekano kuwa wajumbe hao ni wadau wa posho na badala yake Watanzania watawaona wanafaa kupata kiinua mgongo wakati wanaondoka.
Akijibu maswali aliyoulizwa na wajumbe, alisema viwango na kasi ni falsafa yake na maana yake ni kufanyakazi na kwamba kitu chochote kama ni huduma au bidhaa unahitaji iwe kwenye viwango na inayofaa na kwamba katika mchakato wa Katiba wananchi wataelewa iwapo Katiba itakuwa na viwango wanavyotarajia.
Kuhusu kuvunjika kwa Bunge iwapo Kanuni za 37 na 38 inayohusu kura ya siri na wazi katika kupitisha rasimu ya katiba, alisema haina haja kuwa na wasiwasi kwa kuwa atatumia wajumbe wenye busara kuhakikisha linamalizika kwa kuwa kila aliyendani ya Bunge hilo ni kiongozi wa jamii aliyotoka.
Kuhusu Muungano, alisema atautetea na wanataka uvunjike hawatafanikiwa kwa kuwa watashughulika nao kwa busara na kwamba Muungano umekuwepo kwa muda mrefu bila matatizo.
“Wale wanaotaka Muungano uvunjike usiku wa kuamki jana wamenizushia kuwa naumwa, nipo mahututi nimelazwa hospitali, wajumbe siyo kweli mimi nipo fiti na ataendelea kuutetea Muungano,” alisema .

0 comments:
Post a Comment