Afrika Kusini imetoa onyo kali kwa Rwanda huku mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo ukiendelea kutokota.
Hii ni baada ya hali ya kulipiza kisasi kati ya nchi hizo katika kuwafurusha mabalozi wao.
Alikuwa akigusia madai ya njama ya kumuua
Generali Kayumba Nyamwasa, aliyekuwa anahudumu katika jeshi la Rwanda
zamani ingawa sasa anaishi nchini Afrika Kusini.
Rwanda iliwafurusha wanadiplomasia sita wa
Afrika Kusini baada ya serikali ya Afrika Kusini kuwafukuza wafanyakazi
watatu wa ubalozi wa Rwanda na mmoja wa Burundi nchini humo baada ya
kuwahusisha na njama ya kutaka kumuua Nyamwasa.
Wakati huohuo, Mjumbe maalum wa Rais Barack
Obama katika kanda ya maziwa makuu, Russ Feingold amesema kuwa nchi za
Rwanda na Afrika Kusini hazina budi kumaliza mzozo kati yao kwa njia za
kidiplomasia.
Mjumbe huyo aliyasema hayo mjini Kigali baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Feingold amesema Marekani inafuatilia kwa karibu
karibu kundi la FDLR akilitaja kama moja ya makundi hatari katika eneo
hilo la maziwa makuu.
0 comments:
Post a Comment